Bara wabebe mzigo umeme Visiwani hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bara wabebe mzigo umeme Visiwani hadi lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MzalendoHalisi, Dec 28, 2007.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,865
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=2279

  Je ni sahihi Visiwani walipie Umeme bei ndogo kuliko bara? Umeme wote unatoka Kidatu! Ni kigezo gani kinatumika Visiwani walipie kiasi kidogo kuliko bara na kwa kwa nini? Je ni faida ya nani?

  Au ndo faida za Muungano Visiwani?

  Je ni nani anabeba huu mzigo? Sii mtumiaji mlalahoi wa umeme Bara?

  Is this fair?

  Could this be ndo maana inabidi bei ya umeme ipande kwa sasa -kwa vile Visiwani wanalipa kidogo kuliko bara?????
   
 2. K

  Komando Member

  #2
  Dec 28, 2007
  Joined: Dec 25, 2007
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wacha wa-znz tule matunda ya MUUNGANO.
   
 3. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri waje wajibu wenyewe maana kila siku ni malalamiko tu.
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,144
  Likes Received: 1,234
  Trophy Points: 280
  Wanatakiwa watupatie Jibu Tanesco hizi tofauti za gharama, WaTZ wa bara ndo tunatakiwa kuchangia ili kuimarisha Muungano au ndo faida za Muungano kwa Zanzibar?

  Mlalahoi ataweza kuweka umeme kwenye kajumba kake ka mbavu za mbwa ambako kana thamani ndogo sana ukilinganisha na geti la nyumba za waheshimiwa wa masaki?

  Hawa mafisadi wataendelea kutubebesha mizigo hadi lini?
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mambo mengine yako wazi sana, sijui kwa nn wengine wanapenda complication?
   
 6. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #6
  Dec 28, 2007
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hili swali naona Karamagi mwenyewe ndie wa kulijibu na sio TANESCO.
  Mimi sijasikia Tanganyika (Serikali)kuchangia Muungano lakini Zanzibar kama nchi inachangia katika Muungano, coz Bara hawana Serikali. Naelewa wananchi wa Bara wanachangia kama wananchi wa Zanzibar katika Muungano, maana hiyo ni kila Mtanzania.
  Zanzibar kuuziwa (sio kupewa bure) umeme kwa bei ya chini imekuwa soo! Mmesahau ya kuwa Bara imechukuwa Serikali yoote ya Muungano na kila kilichomo ndani, chao chao chetu chao. Bara inapata na inafanya mangapi kwa jina la Tanzania na wakati hata Zanzibar hawajui kinachoendelea, yanaishia hukohuko.
  Hata Zanzibar ikitaka bure huo umeme amini watapewa tu, coz BARA inaelewa haitaathiri chochote kutokana na wanachoingiza kwa Zanzibar kuwepo kwenye Muungano huo.
  Wakati umefika wa kudai Tanganyika yenu, ili tu Zanzibar ipumue.
  Na kwa nini hamdai?
  Serikali tatu na kero kwisha.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani inabidi tuuangalie huu muungano wetu kwa macho makavu. Tuainishe wazi gharama zake na mchango wa kila upande halafu mjadala uanze kuhusu namna ya muungano tunaouhitaji au hata kama Muungano wenyewe unahitajika. Wazanzibari waseme wazi kama wana nia na muungano na wale wa bara vilevile. Ni heri tukiwaiga iliyokuwa Czechoslovakia kuliko Yugoslavia. Canada walifanya referendum kuhusu Quebec na watu wa Quebec "blinked". Kama kweli ndugu zetu waZNZ hawafaidiki kwa namna yeyote na huu Muungano ni bora tuurekebishe au tukubali kuachana bila shari. Ni vizuri Muungano wetu uwe wa hiari kuliko huu wa kutupiana madongo kila kukicha. Leo wote ni maskini wa kutupwa, itakuwaje hapo mmoja wetu atakapogundua mafuta?
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wako waliodai serikali ya Tanganyika na wote tunajua yaliyowasibu. Hizi mbili zinatusumbua tatu tutaweza kweli? Tutachangia vipi hiyo ya tatu? Mgawanyo wa madaraka utakuwaje? 50,50? Kama ni hivyo basi na uchangiaji uwe hivyo hivyo bila kuangalia ikubwa wa nchi. Au tufuate wenzetu, anayechangia zaidi ndiye anayenufaika zaidi. Tukifika hapo ya nini hii serikali ya tatu, si wote tu wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki? Kwa nini tuongeze gharama ya serikali ya tatu? Kama walivyosema wachina," be careful what you pray for, for you might get it!"
   
 9. K

  Komando Member

  #9
  Dec 28, 2007
  Joined: Dec 25, 2007
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kula 5 mkuu manake hiyo ndio solution hamna zaidi.
   
 10. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hii mikataba ingekuwa imeingiwa na wazanzibari nina huakika mto wake kule akuna wa kuuzima,wazanzibari wanaumoja pole maslahi yao yanapochezewa.kwa sababu standerd ya maisha yao hayapishani sana kati ya mtu na mtu.lakini wa bara wanajifanya wajuaji ndio maana gharama za maisha ni tofauti na wazenji.siku zote na wapongeza wazenji kwa mshikamano wao ktk kutetea maslahi yao hapo huwa hakuna cuf wa ccm.
   
 11. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2007
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mchundo vipi?

  Kwa ukubwa wa Tanzania bara, idadi yake ya watu na rasimali zake sioni uzito wa madai ya bei za umeme na muungano. Tanganyika ina watu zaidi ya millioni 35 na Zanzibar millioni 1. Kwa hesabu za haraka wazanzibar wakilipa sawa na bara, bado hesabu zitakuwa zile zile.
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kama muungano ni between equals hakuna sababu ya mmoja kumbebea mzigo mwenzie. Tatizo lililopo ni kuwa hatujaukubali huu muungano kwa dhati. Kama ingekuwa hivyo, watu wa bara wasingeona tatizo la kuwapiga jeki wenzao na wale wa znz kutingisha kibiriti kwa kudai hata tungetaka bure mngetupa tu! Inabidi kwanza tukubali kuwa huu muungano ni muhimu kwetu sote na kwa hali hiyo tuko tayari kusacrifice kwa ajili yake. Hata kama ZNZ wako milioni moja subsidy yeyote inayofanyika huko inapunguza uwezo wa kuwatendea hivyo hivyo wenzao wa bara. Hili walikubali na wa'appreciate' na sio kubeza kila wakati. Kwa mfano, kwenye hili la umeme. Kwa nini EWURA wasitangaze bei moja kwa pande zote mbili halafu serikali ya ZNZ iwauzie wateja kwa bei nafuu wakilipia wao tofauti hiyo ya bei? Au serikali ya Muungano ilipie hiyo tofauti badala ya kujificha nyuma ya hawa Ewura! Kufanya hivi kutafanya suala zima liwe wazi kwa wote.
   
 13. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2007
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nadhani Fundi inabidi uelewe kuwa umeme unapotumia nyumbani una gharama nyingi zikiwemo za uzalishaji, uzambaji na maintanance. Hivyo bei ya umeme inalipa vitu vyote hivyo. Sijuhi mchundo umechulia wapi, kama ni Dar basi kamuulize MKUU.

  Zanzibar ni Compact hivyo gharama za usambaji na maintanance ni ndogo kuliko za bara. Na hii inatokana na kuwa unauzia shirika la usambaji Zanzibar hivyo gharama za usambaji na maintanance ni ndogo kule. Kwa mtaji huo walaji wa umeme :) wa Zanzibar hawahitajiki kulipa gharama za usambazaji kwa walaji wa umeme bara :) (walaji = watumiaju).

  Hesabu za usambaji wa umeme ni sawa na hesabu za bima ya magari. Sehemu yenye wezi wengi wa magari wanalipa bima kubwa kuliko sehemu yenye wezi wachache.
   
 14. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #14
  Dec 28, 2007
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  TANESCO wanawauzia umeme SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR, na shirika ndilo linawauzia Wazenji kwa bei waitakayo wao, TANESCO haihusiki na usambazaji, ununuzi wa vifaa au metengenezo ya aina yoyote ndani ya Zanzibar, wao wanachojua ni kuuza na malipo yao tu, faida mia kwa mia.
  Huko BARA wajameni TANESCO inahusika na madudu yote, tokea wizi, usambazaji na ukarabati na ndio maana mnalipia zaidi kufidia hayo madudu.
  Nadhani mtanielewa
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ouch, Mkuu Bin Maryam! Naruhusiwa kukosea ndiyo maana sikuupata uhandisi. Unachosema, Bin Maryam kinaelekea isipokuwa kwa kitu kimoja. Kama Ewura wanapanga bei ya kumuuzia msambazaji wa Zanzibar wangesema hivyo, ili bei atakayolipa mteja iwe baina yao na msambazaji wao. Hii itaondoa dhana kuwa Tanesco wanahusika na bei anayolipa mteja. Au Ewura nayo ni ya muungano kwa hiyo wanahusika kuwapangia bei wenzetu wa ZNZ? Mbona inaelekea nguvu zote wamemuelekezea Tanesco? Hilo la wezi lina ukweli, siwezi kupinga. Asante kwa kunielewesha.
   
 16. K

  Kigeugeu Member

  #16
  Dec 28, 2007
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii hoja is so weak!

  Zenj wana tofauti gani na mji kama Moshi au Iringa ktk umeme?

  You can argue better than this! Acha siasa ktk umeme!

  Ukweli Visiwani wanalipia kidogo kwa kubwebwa na walala hoi Bara!

  Kwanza garama kuleta tu umeme toka Kidatu/Kihansi to Zanzibar ni kubwa mara nyingi kwani unapiata baharini- which is another cost!

  Ukweli ni kuwa Visiwani wanabebwa na kusaidiwa umeme na Bara!

  Tupunguze ushabiki na siasa!
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa wanaojua kimombo, huyu bwana anataka kutueleza nini? Pamoja na majibu mazuri ya Bin Maryam na SiDe naona badop kuna jambo limejificha. SiDe mbona hukujibu hivi tokea mwanzo badala ya lugha ya ubabe ya kuwa hata kama znz wakitaka bure watapewa tuu?
   
 18. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2007
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa uhalali bei ya Moshi na Tanga ni tofauti kabisa. Lakini kwa sababu miji hiyo inategemea msambaji mmoja ni lazima gharama zichangiwe. Na kuna vijiji Tanzania bara ambavyo kuna watumiaji watano tu wa umeme. Watumiaji hawa hawaingizi faida na hili shirika lipate faida basi watumiaji wa miji mingine ni lazima wachangie.

  Mkoa wa Kagera unapata umeme kutoka Uganda lakini bei ni sawa na mtu anayetumia wa Kidatu/Kihansi. Piga hesabu hapo. Kwanini asilipe sawa na mtu wa Uganda.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Huu Muungano una kasoro nyingi sana mojawapo ni hili la umeme. Wanasiasa hawataki kuliweka wazi ili tuzijadili kwa mapana na marefu kasoro mbali mbali zilizoko katika muungano ili kuuboresha muungano huo (kama itawezekana). Wanataka kuzifukia kasoro zote zinazolalamikiwa pande zote mbili ili muungano uonekane kama uko shwari kabisa, kitu ambacho si cha kweli.
   
 20. K

  Kigeugeu Member

  #20
  Dec 28, 2007
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks,
  Unasupport watumiaji wote wa umeme Tanzania walipie sawa- wawe Zenj au Moshi au Tanga! This is fair! Kwa nini Bara waibebe Zenj kulipia umeme? Why?

  Sasa swali ni kwa nini Zenj wanalipia kidogo????

  Je huu sii upendeleo?

  Tuache siasa tuangalie uchumi!
   
Loading...