Bara la Afrika na maajabu yake

Unakufa kukosa drip ya maji ya elf 20, kwenye msiba wako ndugu wanakoga bia, mapilau mabiriani, kukuzika kwa heshima zote
Ni hatari sana. Watu watakula, watavimbiwa. Ukishafukiwa kama kuna mke machali wataangalia namna ya kuruka naye chapu.

Alafu watoto wako wanaendelea kubaki kuwa omba-omba.....😑😑
 
Kweli kabisa. Afrika tumekuzwa na ukatili, ulimbukeni, maonyesho ya hovyo, kutaka kundi fulani liabudu wenye nacho. Ukitaka kujiinua unapigwa mawe hadi unabakia kuwa omba-omba. Bara la laana hili.
Hili ni bala la laana kweli
Chukulia mfano unafanya kazi sehemu fulani na kila siku bosi wako
Ana kuchukulia mbugila mbugila
Sasa itokee siku aje agundue kumbe umejiwekeza kwa jambo fulani pengine umefungua hata ka biashara kako aloooo atakuchukia atahisi umemuibia
Na kazi unaweza kufukuzwa

Na hii na kwasababu anahisi hupaswi
Kufanana nae wala kua juu yake
 
siyo afrika tu bali ni all non-Christian world kuna mambo ya kishetani, ukienda india ndio utashangaa ya kina ambani ambaye anafanya harusi ya mamilioni usd harusi (harusi peke yake 400 million usd vs mgodi wote wa dhahabu buzwagi thamani yake ilikuwa ni 300 million usd )huku kazungukwa na slums na mafukara wasio weza hata kupata mlo mmoja, tena mbaya zaidi ni watoto.

ukiondoa Christian world sehemu yote ya dunia iliyobakia ni ushetani, mateso na vilio kila mahali, ndiyo maana all poor muslims wanakimbilia Christian world kuishi kwa maana wanajua angalau they will be treated with respect na human dignity hata kama ni masikini lkn hawaendi kwa ummah wenzao saudi arabia ...
 
Dunia haina usawa hii 😢
 
Tajiri usimuombe pesa bali mpelekee fursa ya kutengeneza pesa, peleka wazo lako la mradi share naye faida utaona kama hujatoboa, roho mbaya kwanza inaanza na sisi wenye shida wengi wanakopa kisha hawalipi na halafu tena kwanini sisi tunajiona kuwa tuna haki ya kusaidiwa?
 
Mkuu, hivi Ukiristo upi unazungumzia? Huu wa hapa Afrika ya matapeli? Ambao waaumini wanahangaika ila pesa zao wanazimalizia kwenye majumba ya ibada?

Wenye kuthamini lishe ya Mchungaji, Padre, Nabii, na Maaskofu ila ikitokea hata mtoto wa jirani anaumwa, anakaa mbali mita 1000?

Ukiristo upi unaowazungumzia mkuu?
 
Ni hatari sana
 
Hivi wewe, ulishaandika proposal ukapeleka kwa individual person or company hapa Afrika, alafu wakazingatia na wewe ukanufaika?

Kama wakikupendelea utakuwa mtumwa wake au mtumwa wa Kampuni vinginevyo atachukua atakukatisha tamaa alafu ana implement kimya kimya. Wewe unabaki huna pa kwenda. Hiyo ndio Afrika.
 

usichanganye mambo, afrika Christians ni wachache sana, wengi wao ni mila mila na muslims, nchi pekee iliyokuwa Christian bara lote ilikuwa south afrika kabla ya communist anc kuchukuwa na leo hii siyo Christian tena ...
 
Hapo cha kufanya ni wewe kutafuta hizo pesa nyingi ili wewe ndo ukawe tajiri wa kwanza kugawa mitaji kwa watu.

Inaonekana wewe unapenda sana vya kupewa
 
Hapo cha kufanya ni wewe kutafuta hizo pesa nyingi ili wewe ndo ukawe tajiri wa kwanza kugawa mitaji kwa watu.

Inaonekana wewe unapenda sana vya kupewa
Changamoto, unasoma na huelewi cha kujibu. Kuna mambo ukitaka kujibu inatakiwa utulize akili.
 
Sijawahi, kwani kama nikitaka mkopo huwa naenda benki. Sidhani hata matajiri wa Europe au America huwa wanatoa mikopo kirahisi hivyo.
 
Hii inaumiza sana, ila watu wanaanza kubadilika taratibu. Kuna koo sasa hivi mtu akilazwa ndani ya siku kadhaa wanajichangisha na kutoa msaada kwa mgonjwa.
Ni vyema , hao wanajitambua. Na nakubali watu wanazidi kubadilika.
 




Unakufa kukosa drip ya maji ya elf 20, kwenye msiba wako ndugu wanakoga bia, mapilau mabiriani, kukuzika kwa heshima zote


MAAJABU MENGINE NI KUWA MASIKINI KUPENDA KUOMBAOMBA PESA KWA MATAJIRI NA WAKINYIMWA WANALALAMIKA KAMA VILE WALICHANGIA KUUPATA UTAJIRI HUO.
WATU wengi huweka siri walitumwa wengine hali zao za uchumi siri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…