Bar ndani ya Gereza

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Baa gerezani
Mamlaka katika gereza moja nchini
Mexico wamekuta wafungwa
wamefungua baa ndani ya gereza.
Mtandao wa China Daily umesema katika baa
hiyo wamekuta vinywaji vikali, bia na hata
meza ya kuchezea pool. Polisi wa Ciudad
Juarez waligundua baa hiyo siku ya
jumatatu katika gereza hilo lililopo katika
jimbo la kaskazini la Chihuahua, imesema
taarifa kutoka ofisi ya mwendesha
mashitaka mkuu.
Walikamata chupa ishirini za vodka, chupa
ishirini za tequila na makopo mia mbili ya
bia. Polisi pia walikuta bunduki tatu, simu 20
za mkononi, bangi misokoto mia moja na
themanini na dozi tisini za dawa za kulevya
aina ya heroin. Mkuu wa gereza hilo
alifukuzwa kazi siku ya Jumatano, na
maafisa wengine wa magereza
wanachunguzwa, amesema Jorge Chaires,
msemaji wa mwendesha mashitaka wa
serikali kwa magereza.
 
Kuna tatizoo sehemu fulani labda posho za askari jela hao maana wale waahalifu wana pesa sana za madawa kule na wana makundi makubwa sana yenye nguvu ni ngumu kuyazuiaa kwa mishahara na hali duni za wafanyakazi wa mexico na nchi zoote za america kusini
 
Mramba na Yona walipotiwa gerezani mbona walikuwa wanapewa kila kitu hadi watoto wa shule?
Bongo pia haya mambo yapo licha ya kuwa hayasemwi
 
mi ni askari magereza, na picha za video zipo, nikikaa kwenye computer ntazi upload youtube dunia nzima ione mafisadi wanavyokula raha magerezani

Me naisubili kwa hamu mkuu tuwekee tujionee uchafu wa viongozi wetu.
 
hawakukuta na makahaba kweli?....lkn ni uzembe wao yan had gereza linakuwa na vtu vyote hivyo eti hawajui then wanakuja kumfukuza kaz mkuu wa gereza....na wenyewe wajiuzulu kwa uzembe uliokithiri.....:confused2:
 
mi ni askari magereza, na picha za video zipo, nikikaa kwenye computer ntazi upload youtube dunia nzima ione mafisadi wanavyokula raha magerezani

Taratibu kaka, hiyo ni kubwa mno! Kama unaogopa ilete sisi tuifanyie kazi; you'll remain anonymous!
 
Back
Top Bottom