John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Mchezo wa Simba dhidi ya Mbeya Kwanza umemalizika na kuna kelele nyingi kuhusu bao la Simba lililofungwa na Clatous Chama kuwa kabla ya kufunga mshambuliaji wa timu yake Meddie Kagere alikuwa ameotea (offside).
Picha za video zinaonyesha kuwa winga wa Simba, Sakho kabla hajapiga shuti lililosababisha bao hilo ni kweli Kagere alikuwa katika nafasi ya kuotea, lakini kwa kuwa shuti hilo lilimgonga beki wa Mbeya Kwanza wakati akitaka kuokoa, ndipo hapo akavunja offside kwa Kagere.
Kagere ambaye alikuwa katika nafasi ya kuotea, kwa kitendo hicho cha beki wa Mbeya Kwanza inamaanisha alikuwa sahihi kuuwahi mpira na kuucheza kisha Mugalu akaugusa na kisha Chama akafunga.
Hivyo, bao la Chama ni halali kwa sababu offside ilivunjwa kwa mujibu wa kanuni ya kuotea na ndiyo maana mwamuzi ameruhusu bao hilo kuwa halali katika mchezo wa Jumapili Februari 6, 2022.