Banza Stone yu mahututi tena, TUMUOMBEE

Banza Stone yu mahututi tena, TUMUOMBEE

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,127
Reaction score
165,991
HALI YA MSANII BANZA STONE NI MBAYA...


1668190733551.png
NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone' ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani.

Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba.



"Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa," alisema Banza na kuongeza:

"Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee."
 
banza stone a.k.a roho ya paka get well soon.
 
Si ndo huyu ambae anatajwa kwenye magazeti kuhusu Madawa ya Kulevya? Nasikia ni mteja mzuri tu wa haya madawa. Kama ni kweli madawa yatamuua.
Akiacha madawa Mungu ampone!!!!
 
Get well soon;ni malaria kweli? Au ngada? TB? Au hii kitu hii kitu hii kitu hii?
 
Tunamtakia afya njema hit maker wa songi la Kumekucha akishirikiana na Patcheko na Maluu Stonch "Nuhu" pona haraka utuletee vibao vikali kama hicho.Kila nikisikiliza wimbo huo najiuliza banza huyu yuko wapi?amka bwana
 
Back
Top Bottom