Bank teller alivyotapeliwa

Bank teller alivyotapeliwa

fdizzle

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,902
Reaction score
2,405
Iko hivi..

Jamaa mmoja alikuwa na Dola za kimarekani elfu kumi (kama milioni 20 za kitanzania). Akafika bank na kwenda dirishani moja kwa moja.

Baada ya kufika dirishani akampa pesa hizo dola ili abadilishe na kuwa pesa za kitanzania. Yule teller akapokea na kuzihesabu pamoja na kuhakiki kama ni halali. Baada ya kuridhika nazo kuwa zipo sawa wakati anataka kuanza kuhesabu za kitanzania yule jamaa akauliza exchange rate ipo vipi?

Akatajiwa akasema ndogo sana naomba dola zangu. Akarudishiwa akajifikiria kama sekunde kadhaa akamrudishia tena yule teller basi nipe hivyo hivyo tu.

Yule teller bila hata kuzikagua tena zile Dola akapokea na kuanza kumuhesabia jamaa pesa zake na kumpatia.

Jamaa akaondoka, kufika muda wa kufunga hesabu anafungua zile dola anakuta ya juu na ya chini ndio pesa halisi. Yaliyobaki yote makaratasi.

Maoni yangu:
Matapeli wawe wanachomwa moto maana wanaharibu maisha ya watu fikiria pesa zaidi ya milioni ishirini unaenda kumtapeli mwenzio ni sawa na kutaka kumuua.

Nawasilisha.
 
Stories ya kutunga haiwezekani. Yani upewe kibunda bila kuzifungua.
Otherwise tuambie ilitokea wapi?
Wizi kama anaosimulia uliwahi kutokea mwaka 2008 branch mojawapo ya Dar, tena ya benki kubwa tu hapa bongo. Yaani ilikuwa hivyo hivyo ila wale walikuwa na begi liko chini miguuni waliporudishiwa wakainama na kuchukua mzigo feki then wakasema tupatie tu kwa hiyo rate. Baada ya uchunguzi wa CCTV kamera ikabidi asamehewe tu, wizi mdogomdogo unatokea sana ndani ya mabenki na hutosikia kwa vyombo vya habari.
 
At least asante.
 
Iko hivi..

Jamaa mmoja alikuwa na Dola za kimarekani elfu kumi (kama milioni 20 za kitanzania). Akafika bank na kwenda dirishani moja kwa moja.

Baada ya kufika dirishani akampa pesa hizo dola ili abadilishe na kuwa pesa za kitanzania. Yule teller akapokea na kuzihesabu pamoja na kuhakiki kama ni halali. Baada ya kuridhika nazo kuwa zipo sawa wakati anataka kuanza kuhesabu za kitanzania yule jamaa akauliza exchange rate ipo vipi?

Akatajiwa akasema ndogo sana naomba dola zangu. Akarudishiwa akajifikiria kama sekunde kadhaa akamrudishia tena yule teller basi nipe hivyo hivyo tu.

Yule teller bila hata kuzikagua tena zile Dola akapokea na kuanza kumuhesabia jamaa pesa zake na kumpatia.

Jamaa akaondoka, kufika muda wa kufunga hesabu anafungua zile dola anakuta ya juu na ya chini ndio pesa halisi. Yaliyobaki yote makaratasi.

Maoni yangu:
Matapeli wawe wanachomwa moto maana wanaharibu maisha ya watu fikiria pesa zaidi ya milioni ishirini unaenda kumtapeli mwenzio ni sawa na kutaka kumuua.

Nawasilisha.
kwa namna ulivyo malizia hapo mwisho ni wazi kuwa wewe ndiyo huyo Teller 98%
 
At least asante.
Yaani mkuu ukisoma hivyo utafikiri uongo, kuna mdada tena wa benki hiyohiyo tawi jingine la hapo Dar. Alikuwa anaishi na mshikaji tu watoto wa mishen town hawajaoana rasmi. Akampanga demu, kila subuhi anakwenda anachukua mzigo anafanya mishe zake jioni anarudisha. Mara ya mwisho kapewa 30 M jamaa hakurudi hadi branch inafungwa, sister kubanwa kasema kila kitu na jamaaa sidhani kama walimpata.
 
Stories ya kutunga haiwezekani. Yani upewe kibunda bila kuzifungua.
Otherwise tuambie ilitokea wapi?
katunga hii niliskia zamani sana nayo ilikuwa ya kutungwa.
 
Mkuu mimi nina ndugu yangu dada kabisa yupo mahabusu katapeliwa milion 30 kwa mtindo huu huu, unaweza usiamini maana adi mimi mda huu sijaamini ila ndo uhalisia ila wanatumia dawa maana adi uje kujua ni wakati unafunga hesabu au kesho yake, nasubiri weekend nikamsalmie gerezani japo kachanganyikiwa kabisa, daah
 
katunga hii niliskia zamani sana nayo ilikuwa ya kutungwa.
Sasa mimi nakwambwia hiyo ya 2008 ilitokea kabisa nakuhakikishia kwa asilimia mia, tena wale walikuwa na kama USD 20K. Tena waliokuwa wafanyakazi miaka ile walisomewa hadi email toka HQ kuwatahadharisha
 
Mti ashachoka na kazi unafanya vitu vila umakini na mshkaji lazima atakuwa alienda jioni hivi wakati umakini wa teller umepungua sanaa...!! Anafanya faster awahi kumalizaa
Yaani sababu ni hiyo ila pia na kufanya kazi kwa mazoea, ila hizo mateller wazoefu huwapigi kabisa kwani zishatokea mara kadhaa huko nyuma.
 
Back
Top Bottom