Sioni ubaya wa kuwa na Bango limeandikwa kwa lugha yao. Ila nakushangaa kwanini ujawahi kulalamika kuwa kuna mabango mengi yameandikwa kwa lugha ya kiingereza, kiarabu na nyinginezo au unadhani hizi ni lugha zetu?
Kama utakuwa ni wa umri wangu, utakumbuka mwaka 1972 Tanzania ilipigana vita fupi na Uganda. Wahindi waliokuwa wanaishi Bukoba Mjini, ilibidi wahame mji na kukimbilia vijijini, tatizo lao ilikuwa ni lugha. Baada ya hapo Wahindi walioendelea kuishi Bukoba walijifunza Kihaya na wengine walikimbia kimoja. Hapa ninachotaka kusisitiza ni kuwa wageni WOTE wanaoingia hapa kwetu Tanzania tufanye juhudi za kuwafundisha kiswahili na siyo wao kutufundisha lugha zao.
Ilo bango, kama lilivyotafsiriwa na Kitia,linaweza kuendelea kuwepo kama limefuata taratibu za kuwepo, lakini kama halina manufaa kwa mtu yoyote, basi mwenye kulimiliki hatokuwa na sababu ya kuliweka. Kwani wote tunaongea kiswahili basi litabadilika kuwa Kiswahili - Iwapo tutafanya ulazima wa kuwafundisha wageni Kiswahili. Sasa hivi Tanzania kuna vijana wengi wamesahau kuwa Kingereza na lugha nyinginezo ni vi-lugha tu kama Kichagga, Kinyamwezi n.k
Mpenzi wangu A, wa UK, nakupa ongera kwa kuendelea kuwaelimisha vijana juu ya Lugha yetu, japokuwa umeishi nje ya nchi kwa muda mrefu kuliko umri wa mtoto wa darasa la saba.