Bango la walimu kwa shemeji yao Rais Kikwete

Bango la walimu kwa shemeji yao Rais Kikwete

Walimu hawako serious... wanaenda kiutani utani badala ya kukomaa... Dai haki kwa kukomaa sio shemeji shemeji...
 
CCM na serikali yake huwatumia walimu kwa kila jambo ikiwemo kufanya hila za kushika dola. Wanavijiji wote wanarubuniwa na walimu ambapo wanaitwa wataalamu

CWT na CCM ni ndugu we waache wakigombana shika jembe ukalime
 
Bango la walimu lazua gumzo Mei Mosi


Pg-1-21-300x296.jpg


BANGO lililobebwa na walimu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi jana likiwa na maandishi yanayosomeka "Shemeji unatuachaje?", limezua gumzo katika maeneo mbalimbali nchini, hususan katika mitandao ya kijamii.

Jana katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, walimu walipita mbele ya Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi huku wakiwa wamebeba bango hilo.
Wakipita mbele ya Rais Jakaya Kikwete, walimu hao walilielekeza bango hilo upande wake ili aweze kulisoma vizuri.

Picha zilizochukuliwa za walimu hao wakiwa wamebeba bango hilo, zilisambaa kwa kasi jana hiyo hiyo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, hususani ule wa WhatsApp.
Walimu wamekuwa wakimuita Rais Kikwete shemeji kutokana na mke wake, Mama Salma, kutoka katika kada hiyo.

Mama Salma Kikwete kabla ya mume wake hajawa Rais alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi, akiwa amefundisha shule kadhaa, ikiwemo ya Mbuyuni, jijini Dar es Salaam.
Mara nyingi walimu kupitia Chama cha Walimu Tanzania (CWT), wamekuwa katika mgogoro na Serikali kutokana na kudai malimbikizo ya madeni yao.

Chama hicho, ambacho kinaongoza walimu wa shule za msingi na sekondari wapatao 206,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010, kimekuwa pia miongoni mwa vyama vinavyopinga mchakato wa Katiba mpya.

Bango hilo jana limeibua mjadala mkali, huku wengine wakiwapongeza walimu kwa ubunifu wao, wengine wakisema Kikwete atawaacha kama alivyowakuta.
Tofauti na mtazamo wa wengi, hata hivyo, Rais Kikwete alisema anaondoka madarakani akiwa amefanikiwa kuboresha mishahara ya wafanyakazi nchini, ikiwemo ya walimu.

Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, kima cha chini cha mshahara kilikuwa Sh 65,000 na sasa kimefikia Sh 265,000.

Alisema katika bajeti ijayo kima cha chini kinaweza kikaongezeka na kufikia Sh 300,000.

Kwa utani Rais Kikwete alisema huku akicheka; "Shemeji zangu baada ya hayo nawapongeza kwa kufungua benki ya walimu…kuoa mwalimu ni tatizo".

Chanzo: Gazeti la Mtanzania


 
Nadhani jibu alilowapa JK lilikua lilikua sahihi maana alitumia ile formula ya GIGO
 
Walimu hawako serious... wanaenda kiutani utani badala ya kukomaa... Dai haki kwa kukomaa sio shemeji shemeji...

Shida ni moja tu,wengi wao uwalimu wameupata kwa kuungaunga na mbaya zaidi most of them ni failure hawawezi komaaa.
 
Wez wa nchi hii wanamashmo ya kujfchia kuleee magogon! Ndo mana walimu wametuma salam kwa wez hao
 
NITAMKABIDHI RAIS AJAYE 'VIPORO' VYOTE - KIKWETE
Katika hotuba yake ya mwisho kwa wafanyakazi aliyoitoa jana katika maadhimisho ya Mei Mosi jijini Mwanza, Rais Kikwete alisema wafanyakazi wasiwe na hofu kwa kuwa mambo yote ambayo atakuwa ameshindwa kuyatekeleza atayakabidhi kwa Rais ajaye.
"Nawaahidi kuwa Rais ajaye nitamkabidhi orodha ya yale ambayo bado ni kiporo. Ni imani yangu kwamba mtaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Tano itakayokuwapo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015".
 
Shida ni moja tu,wengi wao uwalimu wameupata kwa kuungaunga na mbaya zaidi most of them ni failure hawawezi komaaa.

Kikwetu shinji ni popo, naona umechukua tabia ya popo ya kujaribu kumnyea mavi muumba wake wakati ndiye aliyemuumba kwa kumgeuzia makalio juu kichwa chini. Si ajabu ni divission 5 wewe.
 
Hivi janga la kitaifa ni walimu au matatizo yao yanayotokana na madai yao ya msingi ndio janga la kitaifa??.

wameshindwa kujitambua na kupambana dhidi ya anayewatesa,Leo wanamwita shemeji MTU zero kabisa,badala ya kudai khaki wanaendekeza ushemeji ili wapate hisan,HV kila aliyeoa mwalim ni shemej Wa walimu?mbona kuna walimu wameoana,nan shemej ya nan hapo?kuna shule Mbez kwa musuguri Mei mosi walilazimishwa kufundisha hadi saa 8 mchana na wakakubali.je wataweza kufundisha watoto juu ya ukombozi?kama siyo janga nini sa sa?
 
Back
Top Bottom