Bango la walimu kwa shemeji yao Rais Kikwete

Bango la walimu kwa shemeji yao Rais Kikwete

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Katika maadhimisho ya sherehe za mei mosi
1430479874561.jpg


BANGO lililobebwa na walimu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi jana likiwa na maandishi yanayosomeka "Shemeji unatuachaje?", limezua gumzo katika maeneo mbalimbali nchini, hususan katika mitandao ya kijamii.

Jana katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, walimu walipita mbele ya Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi huku wakiwa wamebeba bango hilo.
Wakipita mbele ya Rais Jakaya Kikwete, walimu hao walilielekeza bango hilo upande wake ili aweze kulisoma vizuri.

Picha zilizochukuliwa za walimu hao wakiwa wamebeba bango hilo, zilisambaa kwa kasi jana hiyo hiyo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, hususani ule wa WhatsApp.
Walimu wamekuwa wakimuita Rais Kikwete shemeji kutokana na mke wake, Mama Salma, kutoka katika kada hiyo.

Mama Salma Kikwete kabla ya mume wake hajawa Rais alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi, akiwa amefundisha shule kadhaa, ikiwemo ya Mbuyuni, jijini Dar es Salaam.
Mara nyingi walimu kupitia Chama cha Walimu Tanzania (CWT), wamekuwa katika mgogoro na Serikali kutokana na kudai malimbikizo ya madeni yao.

Chama hicho, ambacho kinaongoza walimu wa shule za msingi na sekondari wapatao 206,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010, kimekuwa pia miongoni mwa vyama vinavyopinga mchakato wa Katiba mpya.

Bango hilo jana limeibua mjadala mkali, huku wengine wakiwapongeza walimu kwa ubunifu wao, wengine wakisema Kikwete atawaacha kama alivyowakuta.
Tofauti na mtazamo wa wengi, hata hivyo, Rais Kikwete alisema anaondoka madarakani akiwa amefanikiwa kuboresha mishahara ya wafanyakazi nchini, ikiwemo ya walimu.

Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, kima cha chini cha mshahara kilikuwa Sh 65,000 na sasa kimefikia Sh 265,000.

Alisema katika bajeti ijayo kima cha chini kinaweza kikaongezeka na kufikia Sh 300,000.

Kwa utani Rais Kikwete alisema huku akicheka; "Shemeji zangu baada ya hayo nawapongeza kwa kufungua benki ya walimu…kuoa mwalimu ni tatizo".

Chanzo: Gazeti la Mtanzania

 
Hawa walimu choka mbaya halafu wanamuita mtesaji wao kwa jina la heshima kiasi hiki?
 
Aaaaah waalimu na shemeji yenu mulimpigia kura nyingi lakini ndio hivyo
 
"SHEMEJI UNATUACHAJE?" Maneno mawili lakini mazito, yenye maana kubwa na ya kihisia. Ktk matumizi ya lugha, waalimu wameonesha ujuzi wao katk kufikisha ujumbe.

Maneno haya mawili ni mazito ukilinganisha na wale waliojiita umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu walioandika "waraka" kwenye bango lao na kujaza maneno mengi ambayo si rahisi kusomeka kwa haraka.

Kwa Kifupi walimu wameonesha ubora wao katika matumizi ya lugha na weledi wao. Ikiwa nitaanzisha kampuni fulani leo nitapenda mtu mwenye taaluma ya ualimu awe Marketing Officer wangu. Waalimu wanajua Marketing strategies kuliko hata baadhi ya waliosoma Marketing.

Wanajua targeted audience wao, wanajua branding, wanajua media relations, wanajua PR, wanajua event management, wanajua namna ya kucapture attention ya audience na ujumbe wao ukafika kwa watu wengi tena bila gharama.

Unakumbuka walipojenga jengo lao la kitega uchumi Mbeya? Hawakutumia fedha yoyote kulitangaza ila walitafua a good marketing strategy ya kutangaza na walifanikiwa sana. Walisema tu JENGO LA KWANZA LENYE LIFT MBEYA. Ujumbe ukasambaa kama mafuta ya taa.

Leo wamekuja na SHEMEJI UNATUACHAJE. I like the Marketing stategy of teachers. I like their spirit, I like their solidarity, i like their creativity.

Nami nasema SHEMEJI wakumbuke, angalia namna ya kuwaacha. Usibaki kucheka tu. Let it touch your heart as it touches theirs. Respect to all teachers. The hidden heroes. The Pride of Tanzania.

Happy Worker's day.!
 
atawaachaje? mngemuuliza wifi enu. kwa nn miaka kumi shemeji hajafanya kitu kikubwa kwenu.
 
Nawe ni muandishi mzuri sana bwana chichimizi, una mpango wa kuwa mwanahabari (journalist)? maneno mazuri na yamenyooka!
 
shemeji unatuachaje ?
 

Attachments

  • 1430557531200.jpg
    1430557531200.jpg
    23 KB · Views: 1,223
Walimu siasa zimezidi, kama hakuwasaidia miaka 9 na miezi 8 ataweza miezi 4????. Walitaka kuchekesha watu na waonekani kwenye media. Hata mwaka jana uwanja wa Uhuru walisikika shemeji tusaidie , je alifanya hivyo???. Wasikate tamaa wachape kazi watusaidie watoto wetu. Mafanikio au maisha bora majaariwa.
 
Walimu wa nchi hii wameshndwa kutumia idadi yao ipasavyo!
 
wanataka hisani, badala ya kudai haki zao zamsingi.

walimu wengi wana hali mbaya kiakili hadi kimazngira..
 
Back
Top Bottom