Bango kitita: Utaifisishaji wa mali za IPTL

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Akiwa amejawa na furaha na bashasha baada ya kuzukiwa na muujiza wa kusamahewa madhambi yake bila kuomba msamaha mdharauliwa, waziri mkuu mizengo pinda, jana jioni alilidanganya bunge kwa kuliahidi kwamba kila kilichoazimiwa na bunge kitatekelezwa kama kilivyoazimiwa kwa ukamilifu.

Pinda,akiwa na nguvu mpya zilizomuwezesha kucheka kwa mara ya kwanza toka siku ile PAC wasome report yao bungeni,akadai atatumia mfumo wa BANGO KITITA katika kuhakikisha utekelezaji wa maadhimio hayo.

Moja ya azimio ni utaifisishaji wa MALI ZA IPTL.

Najiuliza,Pinda atatekelezaje hili kwa ukamilifu?
 
Adhimio sio sahihi bali ni Azimio. itakuwa umesoma wakati wa j.k. na mkapa waliozika Azimio la Arusha.
 
Bado Harufu ya kurudi kwenda kufuga Nyuki Sumbawanga inanukia sana. Asitudanganye na uchawi wa Sumbawanga hapa
 
Akiwa amejawa na furaha na bashasha baada ya kuzukiwa na muujiza wa kusamahewa madhambi yake bila kuomba msamaha mdharauliwa, waziri mkuu mizengo pinda, jana jioni alilidanganya bunge kwa kuliahidi kwamba kila kilichoazimiwa na bunge kitatekelezwa kama kilivyoazimiwa kwa ukamilifu.

Pinda,akiwa na nguvu mpya zilizomuwezesha kucheka kwa mara ya kwanza toka siku ile PAC wasome report yao bungeni,akadai atatumia mfumo wa BANGO KITITA katika kuhakikisha utekelezaji wa maadhimio hayo.

Moja ya azimio ni utaifisishaji wa MALI ZA IPTL.

Najiuliza,Pinda atatekelezaje hili kwa ukamilifu?

Mkuu,
Hakuna sehemu ambayo maazimio ya bunge yameitaka serikali kutaifisha mali za IPTL.

Bunge limeiomba serikali iangalie uwezekano wa kuinunua mitambo ya IPTL.

Nadhani Kununua na kutaifisha ni vitu viwili tofauti.

Mapendekezo ya PAC ikiwa ni pamoja ma kutaifisha mitambo ya IPTL yaliondolewa bungeni na Mwenyekiti wa PAC, Zitto na kuweka mapendekezo ya Kamati ya maridhiano.
 
hiyo january pia aliwaahidi waislamu mahakama ya kadhi....hehehehehehehe
 
Mkuu,
Hakuna sehemu ambayo maazimio ya bunge yameitaka serikali kutaifisha mali za IPTL.

Bunge limeiomba serikali iangalie uwezekano wa kuinunua mitambo ya IPTL.

Nadhani Kununua na kutaifisha ni vitu viwili tofauti.

Mapendekezo ya PAC ikiwa ni pamoja ma kutaifisha mitambo ya IPTL yaliondolewa bungeni na Mwenyekiti wa PAC, Zitto na kuweka mapendekezo ya Kamati ya maridhiano.

Mkuu
Naona unatengeneza maazimio yako sasa.

Na hata kama ni kununua,atawezaje kutekeleza wakati acquisition ya namna hiyo haipo kwenye mipango ya serikali ya mwaka,miaka mitano wala ishirini?
 
Tutawakumbusha hiyo January,muhongo na madalali wenzake lazima wang'oke.
 
Mkuu
Naona unatengeneza maazimio yako sasa.

Na hata kama ni kununua,atawezaje kutekeleza wakati acquisition ya namna hiyo haipo kwenye mipango ya serikali ya mwaka,miaka mitano wala ishirini?

Mkuu ni kweli kua hakuna azimio la kutaifisha mitambo ya iptl...bali kuangalia uwezekano wa kuinunua....hilo swala la kutokuwepo kwenye bajeyi ya serikali....n comment
 
Na wahakikishia Pinda sio mzigo kama mnavochukulia. ALIMPIGA JAIRO CHINI .. Boss wake aliporejea nchini ...Alifanya nini?
Pinda alijifunza .. ! Na kujifunza huko kulimuathiri yeye na taifa.
Hakuna PM yeyote chini ya BOSS huyo huyo anaweza ku perform ... So no need of any replacement .. ni kuitia nchi ghrama na kuwaumiza wanachi. Badilisheni Boss if that is what you're capable.
 
Mkuu ni kweli kua hakuna azimio la kutaifisha mitambo ya iptl...bali kuangalia uwezekano wa kuinunua....hilo swala la kutokuwepo kwenye bajeyi ya serikali....n comment
Refer azimio namba 2
 
Akiwa amejawa na furaha na bashasha baada ya kuzukiwa na muujiza wa kusamahewa madhambi yake bila kuomba msamaha mdharauliwa, waziri mkuu mizengo pinda, jana jioni alilidanganya bunge kwa kuliahidi kwamba kila kilichoazimiwa na bunge kitatekelezwa kama kilivyoazimiwa kwa ukamilifu.

Pinda,akiwa na nguvu mpya zilizomuwezesha kucheka kwa mara ya kwanza toka siku ile PAC wasome report yao bungeni,akadai atatumia mfumo wa BANGO KITITA katika kuhakikisha utekelezaji wa maadhimio hayo.

Moja ya azimio ni utaifisishaji wa MALI ZA IPTL.

Najiuliza,Pinda atatekelezaje hili kwa ukamilifu?
Si tu kwa ukamilifu bali hata kwa robo yake, hatatekeleza!
 
Januari sio mbali.Mbivu ama mbichi zitajulikana.
Jambo ambalo tunasahau ni kwamba ni rahisi sana kikao cha januari ku-postpone issue kama hiyo... kuna issues elfu kidogo ambazo zimeshapata kuwa postponed. Watadanganywa hadi bunge la Aprili... bunge la April litakuwa bize na bajeti na baada ya hapo, bunge la July wabunge wanakuwa washavurugwa tayari... kila mtu anafikiria jinsi ya kurudi mjengoni... ni kwamba watu watakuwa wanaombea kikao cha bunge kiishe warudi majimboni kujisalimisha kwa wananchi na baada ya hapo, kila mtu na lwake!!
 
Mtoto wa mkulima anajua kunoa jembe tu, mwisho wa siku anavuna magugu.
 
Mkuu
Naona unatengeneza maazimio yako sasa.

Na hata kama ni kununua,atawezaje kutekeleza wakati acquisition ya namna hiyo haipo kwenye mipango ya serikali ya mwaka,miaka mitano wala ishirini?

Mkuu

Mimi sina sababu ya kutengeneza maazimio.

Ninalikueleza ni Azimio la saba ambalo linasema,
7. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha jinsi ambavyo TANESCO imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya Shirika hilo;

KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba TANESCO itaendelea kulipa fedha nyingi kwa ajili ya gharama za umeme huo wa IPTL;

HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.
Kama unataka kusoma maazimio yote gongaHAPA
 
Mkuu ni kweli kua hakuna azimio la kutaifisha mitambo ya iptl...bali kuangalia uwezekano wa kuinunua....hilo swala la kutokuwepo kwenye bajeyi ya serikali....n comment

Zitto Kabwe
Azimio kuhusu mitambo ya IPTL magazeti mengi yameandika "Serikali inunue" ama " Serikali itaifishe"

Azimio sahihi ni " Serikali kuichukua mitambo ya IPTL kwa mujibu wa Sheria za Nchi"

Sio kununua. Sio kutaifisha.
2 hrs · Public
4 Comments
 
Back
Top Bottom