Bangi na Uruguay - Rais wao nae anatumia nini majani?

Ngoja nianzishe ka "EPZ" kangu ka bangi ya kupeleka Uruguay!
 
nashangaa sana tanzania uchumi tunao tunaukalia. kwanini na hapa bangi haihalalishwi?

dini yako inaruhusu hii??umekuaje leo...

angalia unavyojichanganya
 
Wewe ulete mambo ya dini, nikujibu, halafu wewe ndio useme mimi najichanganya? umevuta bangi?
ww ni mtetezi mzuri sn wa dini yako...nashangaa leo unauliza kwa nn tanzania bangi haihalalishwi???
 
ww ni mtetezi mzuri sn wa dini yako...nashangaa leo unauliza kwa nn tanzania bangi haihalalishwi???

Kijana nimeshakujibu, kuwa dini yangu chochote chenye madhara ni haramu. Hata wali kama unakudhuru basi kwako ni haramu. Sijui umenielewa au ni bongo lala?

Nikakwambia hata pombe kwa dini yangu ni haramu lakini mbona kuna viwanda vya pombe vingi tu hapa kwetu? kwa hiyo uharamu au uhalali wa bangi kwa dini yangu hauhusiki na kuruhusiwa na serikali.

Nikakwambia pia mbona bangi hata mimi nnaitumia (lakini si kwa madhara) au kwa kulewa.

Nini ambacho hukielewi? vipi wewe hutumii bangi?
 
Nashangaa sana Tanzania uchumi tunao tunaukalia. Kwanini na hapa bangi haihalalishwi?

1. Kwasababu madhara yake ni makubwa kuliko manufaa.
2. Tuna njia nyingi na nzuri zaidi za kukuza pato lentu bla kutumia bangi.

Wengine wenye mtazamo kama wangu wataongezea.

Swali la kizushi: Wewe unatumia???
 
1. Kwasababu madhara yake ni makubwa kuliko manufaa.
2. Tuna njia nyingi na nzuri zaidi za kukuza pato lentu bla kutumia bangi.

Wengine wenye mtazamo kama wangu wataongezea.

Swali la kizushi: Wewe unatumia???

Hayo madhara ni yepi?

Mimi natumia lakini si kwa kulewea.

Unajuwa bangi ni mboga nzuri tu na ni dawa nzuri sana ya magonjwa mengi na pia ina matumizi mengi sana yenye faida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…