Bandari ya Bagamoyo ijengwe kama Bandari ya kimkakati isifanye kazi zinazofanywa na bandari ya Dar

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,952
12,526
Bandari ya Bagamoyo ijengwe kama bandari ya kimkakati iwekewe gari(berth) ambazo bandari nyingine hazina. Pia ujenzi wake kama utapitishwa itabidi tenda itangazwe upya na mzabuni atakayeshinda ndio atajenga tusimkumbatie mchina hata kama ni rafiki yetu.

Tanzania tangu tupate uhuru hatuna bandari yenye gati za kupaki meli za uvuvi na cruise ship(meli kubwa za abiria).
Kama bandari ya Bagamoyo itajengwa ianze au iwekewe gati(berth) hizi;-

1.Gati ya meli za uvuvi
Bandari zote tulizo nazo hazina sehemu ya kuhudumia meli za uvuvi, hivyo bandari ya Bagamoyo inatakiwa iwe na Gati la meli za uvuvi na iwekewe facilities zote za kupokelea meli za aina zote za uvuvi na kutunzia samaki.

2. Gati ya meli kubwa za abiria(Cruise Ship)
Bagamoyo ni mji mkongwe na una historia kubwa Katika utalii, endapo itawekwa Gati ya kupokea meli za kitalii itafanya vizuri zaidi. Mpaka sasa hatuna bandari yenye Gati la kisasa kea ajili ya meli hizi ambayo Ina sehemu kubwa ya kupokelea na kupumzika wasafiri(lounge). Meli hizi huja chache sababu hatuna bandari yenye uwezo wa kuhudumu na zikija bandari ya Dar es Salaam husitisha matumizi ya Gati za kawaida ili meli hizi zifunge.

3.Gati kwa ajili ya bidhaa zinazohitaji unarudi(Refrigerator containers).
Bandari ya Bagamoyo pakijengwa Gati ambayo Ina sehemu kwa ajili ya contena za refrigeration au cold room kwa ajili ya bidhaa zinazoharibika upesi. Itasaidia Sana kwa wakulima na wafanya biashara kusafirisha bidhaa Zao kwenda nje ya nchi na zinazoingia.

Bandari ya Bagamoyo haitakiwi kuja kufanya kazi ambazo tayari bandari za Dar es Salaam,Tanga na Mtwara zinafanya ili kutowalazimisha wateja kuingia gharama zaidi katika usafirishaji na serikali kuweka miundo mbinu mipya.

Bandari ya Dar es Salaam itaendelea na kupokea mizigo ya meli za Ngano maana facilities zipo, Container, Mbolea,Sukari na Mafuta. Meli ambazo wateja wanaweza wakatumia bandari ya Bagamoyo ni General Cargoes ambazo zinaweza kuwa zimebeba Steel product kama nondo,steel coils,plates,pipes na construction materials ambazo waagizaji wengi viwanda vyao vipo ukanda wa Bagamoyo,Tegeta,Mwenge.

Bandari ya Bagamoyo hakuna haja ya kuingia mkataba wenye masharti ya kuzuia ufanyaji kazi wa bandari zetu nyingine. Kwa Mapato ya Bandari zetu zote tunaweza tukawa tunajenga kwa awamu Gati moja au mbili au na kuongeza mikopo yenye riba nafuu.

Bagamoyo should be specific and strategic port.
 
Unajenga ww ama unasubiri kujengewa na mchina?
Wajengaji wapo wengi ukiacha wachina, kuna waholanzi hawa wapo vizuri sana kuanzia tafiti(research) za masuala ya Bandari mpaka ujenzi. Kuna Germany, Norway,Turkey, Egypt na Japan.

Pia Consultant Engineering inabidi wawe wazawa.
 
Back
Top Bottom