Ban Ki moon aomboleza kifo cha Muhammad Ali

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
  • 4bk6ee5157b2c88c0d_800C450.jpg
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mkono wa pole kufuatia kifo cha bingwa na nguli wa ndondi duniani, Muhammad Ali.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa hapa mjini Tehran imenukuu taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa umoja huo akielezea kusikitishwa sana na kifo cha bingwa huyo wa masumbwi duniani na kusema kuwa, Muhammad Ali alikuwa bingwa wa dunia aliyepigania usawa na amani kwa watu wote ulimwenguni.

Ban Ki moon ameongeza kuwa, Muhammad Ali alipigania dunia iliyo bora na alitumia nafasi yake kwa ajili ya kustawisha ubinadamu duniani.

Katibi Mkuu wa Umoja wa Mataifa amegusia pia kazi mbalimbali za kupigania amani na haki za binadamu zilizofanywa na Muhammad Ali na kubainisha kuwa, mwaka 1998, bingwa huyo wa mabingwa katika ndondi aliteuliwa kuwa balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa na alifanya kazi kubwa ya kuwasaidia watoto na watu wanaoteseka katika vita na machafuko duniani.

Muhammad Ali alifariki dunia siku ya Ijumaa ya tarehe 3 Juni akiwa na umri wa miaka 74, baada ya kuugua ugonjwa wa kuetemeka kwa muda mrefu.

Chanzo: parstoday
 
Kwa kweli, hata mimi nilikuwa namkubali sana huyu mzee, na nimeyatazama mapambano yake mengi, ni ya kuvutia sana, yaani sikuchoka kuyatazama, mara kwa mara.

Hasa mapambano yale aliyopigana na marehemu (naye, kwa sasa) Joe Freizer.

Apumzike kwa Amani. Amina!

Ahsante
 
Back
Top Bottom