Balozi Ngaiza Afariki dunia!

TUKUMBUSHANE TOKA JAMII FORUM
kesi ya uhaini iliamuliwa na Jaji Kiongozi Nassoro Mzavas[r.i.p].

..kulikuwa na vifungo tofauti, lakini cha juu kabisa ilikuwa maisha. pia wapo washitakiwa walioachiwa huru.

..kesi ile ilitusisimua sana tuliokuwa tukiifuatilia. upande wa utetezi ulikuwa na mawakili machachari sana kama Murtaza Lakha, Hussein Muccadam, Tarimo,...

..nadhani wengi tulikuwa tunastaajabu jinsi mawakili hao walivyokuwa wakiwahoji mashahidi wa serikali. kwetu sisi ilionekana kama wanaihoji serikali yenyewe!! kwangu mimi ilikuwa ni kitendo cha ajabu kwelikweli.

..upande wa mashtaka nao ulikuwa haujachacha. nadhani mwendesha mashtaka mkuu alikuwa William Sekule, akisaidiwa na wengine kama Mwanyika[ ag wa sasa].

..kwa mtizamo wangu upande wa mashtaka ukiongozwa na William Sekule made very strong closing arguments na hilo lilisaidia ktk kushinda kesi.

..washitakiwa ninaowakumbuka ni: Thomas Lugakingira, Hatibu Gandhi/Hatty McGhee, Suleiman Kamando, Badru Rwechungura Kajaja, Deutrich Mbogoro, vijana wawili wa familia ya Hans Pope. wengine walikuwa Banyikwa[if not mistaken walikuwa mtu na mkewe], na Ngaiza.

..Hans Pope alikuwa ni afisa wa Polisi ambaye alitekwa nyara na majeshi ya Amini na kuuwawa Uganda. mwili wake nadhani ulipatikana baada ya majeshi yetu kuingia Uganda. vijana wake ndiyo hao walioshtakiwa kwa uhaini.

..washitakiwa wa Uhaini waliachiwa huru wakati Raisi Mwinyi anaondoka madarakani.



Quote:
Originally Posted by son-of-alaska
nilisikia one uncle tom,alitoroka gerezani kwa kutumia presidential motorcade,

..Uncle Tom Lugakingira, pamoja na Hatibu Gandhi, walitoroka toka rumande[ukonga au keko]. walitorokea Kenya, na nadhani walipitia mpaka wa horohoro[sina uhakika].

..Uncle Tom alikuwa na pesa hivyo moja kwa moja akakimbilia UK. Hatibu Gandhi aliendelea kuzubaa Kenya, akaja kuwa exchanged na wahaini[ochuka,...] wa Kenya waliotorokea Tanzania.

..ni kipindi hicho hicho Moi alipinduliwa na askari wa jeshi la anga. kiongozi wao alikuwa ni Mjaluo. tuliofuatilia redio kenya tulijuwa it was over for Moi, lakini baadaye tukasikia tangazo toka kwa Maj.Gen.Joseph Mulinge kwamba jaribio limezimwa.


Quote:
Originally Posted by son-of-alaska
alaafu nikasikia,katika hawa kulikuwa na commando,ambaye aliuwawa baada ya gunfight kubwa mitaa ya kinondoni.

..Commandoo aliyeuawa alikuwa akijulikana kama Mussa Tamimu. maofisa usalama walijaribu kumkamata maeneo ya mwananyamala lakini akawaponyoka. baadaye walimkimbiza akarukia pickup iliyobeba bia na kuanza kuwarushia maofisa usalama. baada ya hapo alipigwa risasi na kufariki.


NB:

..FMES amemchanganya Cpt.Tamimu na jambazi sugu aliyekuwa akiijulikana kwa nickname Nyau. jina lake lilikuwa Hamisi .... "nyau."

..Nyau pamoja na majambazi wenzake 19 walitoroka gerezani Ukonga. sina uhakika walitoroka vipi. serikali ilifanya shake up kubwa sana Magereza ambapo Mkuu wao alipoteza kazi.

..baada ya hapo vitendo vya ujambazi na hali ya wasiwasi ilitawala jiji zima la DSM na vitongoji vyake. road blocks zilikuwepo kila mahali, na msako mkubwa ulifanyika.

..ujambazi ulitokana na matokeo ya vita vya Kagera. maisha yalikuwa magumu sana, na kulikuwa na askari wengi, haswa mgambo, waliorudi nyumbani na kuwa-released toka jeshini.

https://www.jamiiforums.com/277244-post409.html

Asante sana kwa historia hiyo.

Hans Pope aliwahi kuwa Regional Police Commissioner, Iringa, na aliuawa Mutukula, karibu na mpaka wetu na Uganda, na askari wa Amin waliovuka mpaka na kutushambulia. Ilikuwa ni mwanzoni mwa 1972.
 
alishawahi kuwa balozi wa kwanza umoja wa kimataifa enzi ya tanganyika na ni mwnaharakati aligombea ubunge mleba kaskazin 2005 kwa chama cha CHADEMA na ailkuwa natarajiwa kugombea tena mwaka huu alifariki usiku wa kuamkia jana NAIROBI ( R I P) tupamoja wanachadema na watanzania

Nilidhani balozi wetu wa kwanza Umoja wa Mataifa alikuwa ni Akili Daniel. Nikumbushe zaidi.
 
Sikubahatika kukutana na huyu mzee ila nadhani ni baba wa Soggy Dog na pacha wake Aniceth (sijui yuko wapi huyu aliyekuwa anajiita Gaza uwanjani).

Mungu awape amani yake nasi kama jamaa zenu wa karibu tuko pamoja na nyinyi katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi!!
 
- Wakuu JF, tuna habari za huzuni kwamba Mwanasiasa wa siku nyingi sana toka enzi za Mwalimu, amefariki dunia leo asubuhi sana. Tutawaletea habari zaidi za msiba na matayarisho ya mazishi.

- Mungu amuweke mahali pema peponi na poleni sana kwa familia na hasa Mkulu Oscar, tupo pamoja sana mkuu katika maombolezo.

Respect.


Field Marshall Es.

Pole sana mkulu Oscar; bahati mbaya hatujaonana tena toka tulipomaliza shule Kibaha.

Rest in Peace Balozi Ngaiza; Amen
 
Pia huyu jamaa alikuwa mshauri wa Chadema na aliwahi kugombea ubunge kupitia chadema, Mungu awarehemu wafiwa wote Amina
 
CHADEMA Kagera wamepata pigo la kuondokewa na kiongozi muhimu sana.
KAMACHUMU wamepata pigo kubwa sana kwani huyu bwana alikuwa chachu ya maendeleo katika eneo hilo. Alijenga hotel ya hadhi ya juu na kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha maji ya kunywa. Alikuwa ni chanzo kizuri cha ajira kwa watu wa eneo lake.
Mungu awatie nguvu ndugu jamaa wanae, wana CHADEMA na watanzania wote kwa msiba huu.
 
Mungu ailaze roho yake, mahala pema peponi, namkumbuka Alikua mpambanaji mpigania haki, ni mzalendo wa kweli mpenda maendeleo ya wananchi wenzake, wa Muleba KAskazini, alikuwa Mjumbe mwenzetu wa Kamati Kuu CHADEMA, hadi mauti yanamfika alikua ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA, tutamkumbuka kwa mengi sana Balozi Ngaiza hasa yalipokuwa mazito yanatokea ndani ya chama alikuwa mhimili mkubwa sana, Mzee Ngaaiza umetuacha tangulia nenda salama tupo nyuma yako na sisi tutakufuata Mungu ailaze roho yako mahala pema Peponi.

- Mkuu heshima sana na ubarikiwe!

Respect.


FMEs!
 
RIP Mzee Ngaiza............Poleni sana wafiwa




wamekwishaiondoa.............Well done Moderators/JF Admin...............

- Nafikiri ujumbe ulishafika tayari, pole sana kwa wafiwa na hasa Mkulu Oscar tupo pamoja sana katika maombolezo.

Es!
 
Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mzee wetu mahali pema. Nimepata bahati ya kufanya kazi na mzee wetu mara kadhaa hususani wakati nikiwa katibu wa vikao vya kamati ya wazee. Marehemu Mzee Ngaiza alikuwa mtulivu, mwadilifu na mpatanishi-kielelezo cha uanadiplomasia wake. Lakini nitakumbuka zaidi masimulizi yake kuhusu historia hasa katika medani ya diplomasia wakati wa kipindi cha vita baridi; nilipata bahati ya kuzungumza kwa kirefu katika safari yetu ya Mkutano wa vyama vya kidemokrasia Afrika uliofanyikia Namibia yeye akiwa kiongozi wetu wa msafara. Nilitamani Mzee wetu aandike historia yake kwa kirefu kabla ya mauti kumfika. Apumzike kwa amani.

JJ
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Yesu libarikiwe.

Poleni sana Wafiwa

Mke wa Marehemu "Magdalena" Mungu akutie nguvu na akuwezeshe kupokea na kujua kuwa imempendeza Mungu iwe hivyo. Amen.
 
R.I.P. Balozi Ngaiza, wafiwa poleni sana, M/Mungu awape subira katika wakati huu wa msiba, kazi ya Mungu haina makosa.

Poleni wanaCHADEMA kwa kuondokewa na kiongozi, lakini kumbukeni msemo wa Mzee Madiba; 'unapokata mti mkubwa, basi miti mingine mingi huchipua kwenye shina lake'.
 
RIP Balozi Ngaiza.

Poleni sana Oscar pamoja na familia yote ya Balozi Ngaiza. Mwenyeezi Mungu awafariji katika kipindi hichi kigumu.


- Wakuu JF, tuna habari za huzuni kwamba Mwanasiasa wa siku nyingi sana toka enzi za Mwalimu, amefariki dunia leo asubuhi sana. Tutawaletea habari zaidi za msiba na matayarisho ya mazishi.

- Mungu amuweke mahali pema peponi na poleni sana kwa familia na hasa Mkulu Oscar, tupo pamoja sana mkuu katika maombolezo.

Respect.


Field Marshall Es.
 
pole kwa wafiwa na watu wote tulio/walio guswa na msiba huu.
lakini wakati huo huo najiuliza mbona hii habari haijaandikwa kwenye gazeti lolote la tanzania?????
 
sasa mbona unatoa habari roborobo? ngaiza gani? amewahi kuwa ktk nafasi gani. kama ulimlenga oscar si unemPM ingetosha?

kama umeleta jamvini basi sema japo kidogo na wengne tujue tunamuongelea nani?

kama hujui vitu usikurupuke ku comment..kwani kama humjui si ukae kimya...ndio matatizo ya kujiunga JF hamsomi hata dos and donts mnakurupuka tu....kwani akimpa pole Oscar hapa kuna shida gani....
 
Nawapa pole wafiwa.

Nilikuwa namfahamu sana Ngaiza na alikuwa jirani pale chole road Masaki.Nakumbuka siku alipoachiwa kutoka kesi ya uhaini na furaha ya ndugu zake iliyokuwepo-(nilikuwa dogodogo wakati ule na nilimuona personally), ingawa alifungwa miaka yote hiyo, aliedelea kufanya shughuri zake kama kawaida alipoachiwa. Wengi waliousishwa kwenye kesi ya uhaini wamekwisha aga dunia, Rugakingira, kama Ngaiza, alikuwa ni mtu wa kamachumu, yeye alifariki miaka ya tisini mwishoni.

Sijui hatima ya hao wengine waliousishwa kwenye kesi hiyo, sijui ni wangapi wamebaki. Ni vizuri kama kitabu kingeandikwa kuhusu kesi hiyo na matukio hayo muhimu katika histiria ya taifa letu kabla hatujapoteza kumbukumbu!
 
.................Sijui hatima ya hao wengine waliousishwa kwenye kesi hiyo, sijui ni wangapi wamebaki. Ni vizuri kama kitabu kingeandikwa kuhusu kesi hiyo na matukio hayo muhimu katika histiria ya taifa letu kabla hatujapoteza kumbukumbu!

Ni kweli Mkuu..............hivi yule wakili Murtaza Lakha naye yuko wapi?
 
Back
Top Bottom