Balozi Maajar and REX Attorneys

Nchi inachezewa...kiasi hiki????UWT na Jeshi wanalewa bia za bure. Hata hawajuii wamewekwa pale kulinda maslahi taifa si ya alie madarakani.....wapi uzalendo wa vyombo hivii????nasikia uchungu sana sana maana nimeshaamini nchi haina mwenyewe!!!
 
Story yako ni interesting lakini nimeshindwa kuona link ya AG katika scandal hii hasa kuhusu yeye kuwa na hisa. Labda ufafanue kidogo

inawezekana sababu ni kwanini anasisitiza kuwa this case is closed!! Anaficha nini?
 
May I inform my friend Belo that the information he has about ambassador Maajar is out of date; currently that mamakubwa is in USA in the same capacity, but since USA is not a commonwealth country is styled an ambassedor and not high commissioner. As regards the reputation of her law firm, it's one of the biggest beneficiaries of the high state corruption involving questionable contacts during the third phase government. As you may probably know Mrs Mkapa's father and her own father are brothers.

You are probably right on all except the last sentence. Majaar is daughter of Alhaj Sinare(now deceased) of Uru Shimbwe while Mrs Mkapa is daughter of one Mr Maro of Old Moshi.
 
engineer wa mambo yote haya ni mkono yeye anajua mapungufu yote ya sheria zetu ndio maana hukimbilia kupeleka kesi ICC.sheria zetu ktk mikataba ya biashara zina mapungufu makubwa hivyo kupelekea kuingia mkenge kila siku!wanasheria wetu mara nyingi huamua hatima ya chochote kwa kuwa waweza fikiri unatetewa kumbe ndiye uliyemshtaki ni lawyer wako!fikiri TANESCO WANADAI FIDIA 50BN,DOWANS WANADAI FIDIA 185BN WAPI PENYE ULAJI?MUAMUZI NI HUYO HUYO
 
Nimeingia kwenye website ya REX Attorneys na kuona kuwa Balozi Maajar bado ni partner wa hii firm.Hii ni AIBU kubwa kwa law proffesion ya TANZANIA.
Jamani hapa hamuoni conflict of Interests?Nchi nyingi zenye democracy kamili,ukichaguliwa kuwa na nafasi kama hiyo unabidi ukate ties.

Kuna thread hapa kuwa REX attorneys imelipwa whooping Ths 5 billion kuiwakilisha TANESCO against DOWANS!!!!Tukumbuke TANESCO ni chombo cha serikali.It means naye amepata share hii ya Tshs 5 billioni hela za wavuja jasho Tanzania.

Mimi sijui sheria,labda jamaa zetu mliosoma sheria,au mjumbe toka TANGANYIKA LAWLESS SOCIETY atuambie hii ni poa tu kuwa balozi mteule anayewakilisha nchi ya Tz huko USA ,also ni private employed na local firm.

Tanganyika Lawless Society? LOL!!!!
 
dawa hii nchi ukipata chansi bugia tu mahela ya walalhoi. sasa hasira zote hizi halafu unasikia uchaguzi mafisadi wameshinda kwa kishindo tena kwa kra za haohao wananchi wanoibiwa kila kukicha, wakiambiwa hawasikii!

Nakuunga mkono!
 
Hoja zingine zipo very low..!!!

Utasemaje na Watanzania walioajiriwa na Ulaya au Amerika na makampuni ya wazungu?...Hivi hakuna Wazungu wanaoweza kufanya kazi zao? hadi waajiriwa waafrika...? Tusiwe wepesi chukua kila Hoja bila Kupima....!!!

kama Hujui Umuhimu wa Wazungu au Expats..ktk big firm ...Kalale...Ukishakuwa utajua umuhimu wa kuwa na Multiculture/Multinational employees ktk Kampun yako...!!
.


kaka grow up!!!

Unajaribu kujustify ufisadi.
Kulinganisha Ulaya/Marekani na Tanzania hapa ni irrelevant na stupidity!

Ulaya/Marekani ni democracy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Eti sijui umuhimu wa Wazungu katika firm!What a nonsense.Wangekuwa Wakenya au waganda nafikiri ungelalamika mpaka mwisho.

Fact hawa Wazungu wanakula resources za Tanzania.Unakiri mabilioni ya TANESCO/BoT ndio pay cheque zao?
 
Kwani hakuna uwezekano tukawaita hawa hawa Rex Attorneys wakatuokolea hiyo hasara ya mamilioni 185 tunayolazimishwa kuilipa Dowans?
 
Haya ni baadhi tu ya mapungufu katika ofisi ya MWANASHARIA MKUU JAJI WEREMA ambayo siku zote imekuwa ikishindwa kabisa kuishauri Serikali ipasavyo na kuiingiza katika Hasara kubwa nchi hii. Hapa ni sawa na kutuambia kuwa Serikali haina wanasheria wa kuiwakilisha katika masuala mazito kama haya yenye maslahi ya umma badala yake inakodisha Kampuni za Mawakili wa Kujitegemea!!!. Ni kweli kuwa hawapo wanasheria huko Serikalini wanaojua haya??

Hii KAMPUNI YA REX ATTORNEY NDIO ILITUMIKA KUISHAURI SERIKALI KIPINDI KILEEEE KUHUSU SAKATA LA RICHMONDULI NA TANESCO NA HAYA NI SEHEMU TU YA YALE ALIYOBAINISHA MHE. WAZIRI MKUU KWENYE TAARIFA YAKE ILIYOSOMEKA
"TAARIFA YA WAZIRI MKUU, MHE. MIZENGO P. PINDA,
(MB.), KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE
YA MKATABA BAINA YA TANESCO NA
RICHMOND
DEVELOPMENT COMPANY LLC

– 28 AGOSTI 2008"

Mhe. Pinda alisema haya, nanunkuu:

"Mkataba baina ya TANESCO na
RICHMOND (uliorithiwa na

DOWANS
)

Kutokana na utata uliojitokeza katika mchakato mzima kuhusu Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliotiwa saini tarehe 23 Juni 2006, Serikali kupitia TANESCO iliamua kufanyike mapitio ya Mkataba huo na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Wanasheria waliobobea katika masuala ya Mikataba ya Kimataifa wa Kampuni ya REX ATTORNEYS.Uchunguzi wa REX ATTORNEYS ulibaini pamoja na mambo mengine
kwamba:-
(a) Utaratibu mzima wa manunuzi ya huduma ya umeme na kuingia
Mkataba na Richmond Development Company LLC ulikiuka
Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004;
(b) Kutokana na ukiukwaji huo, Mkataba baina ya TANESCO na
Richmond Development Company LLC haukuwa halali na hauna
nguvu ya Kisheria; na,
(c) Vilevile, hata kama Mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji
(assignment)
wa Mkataba huo kutoka RDEVCO badala ya
Richmond Development Company LLC kwenda DOWANS
HOLDINGS S.A. na hatimaye
Dowans Tanzania Limited

haukuwa halali.
Kwa kuzingatia mapungufu hayo yaliyobainishwa katika Mkataba huo,
Serikali iliamua kusitisha huduma za
Dowans Tanzania Limited kuanzia

tarehe 1 Agosti 2008.

Taarifa Kamili bofya hapa: http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdf
 
Back
Top Bottom