Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Tangu mwanzo niliona uwezekano mkubwa kwamba Tanesco/Serikali haikuwa na uwakilishi makini kwenye kesi iliyofunguliwa ICC, kadri muda unavyopita ndivyo wasiwasi wangu unazidi kudhihilishwa kuwa ulikuwa na chembe ya ukweli.
Hauhitaji sayansi ya nyukilia kuona tatizo kwenye uteuzi wa Rex Attorneys (kama kweli walikuwa mawakili wa RDC na waliiwakilisha Tanesco kwenye kesi na Dowans). Dowans waliletwa nchini na RDC na kwa kuwa hapakuwepo na tender ya wazi kumpata mrithi wa RDC kwa vyovyote vile RDC na Dowans wanauhusiano ambao unatia madoa makubwa juu ya umakini wa viongozi wa Tanesco/Serikali kuwateua Rex Attorneys wawe wawakilishi wao kwenye mgogoro unaotokana na mteja wao wa mwanzo. Tanzania tuna mawakili wengi wenye weledi na hapakuwa na sababu yoyote ya kuwateua Rex