Balozi Kijazi: Udhalilishaji wa msichana wa Kitanzania sio Ubaguzi wa rangi

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,675
Balozi wa Tanzania nchini India ndugu Kijazi amesema ameridhika na hali ya usalama iliyopo mjini Bangalore,na kuwa kitendo cha msichana wa Kitanzania kupata kisa cha kuvuliwa nguo ni kitendo cha "sintofahamu" tu na si kukihusisha na mambo ya ubaguzi wa rangi.Balozi Kujazi amnukuliwa akisema ameridhishwa na hatua za kiusalama zilizochukuliwa na serikali ya India
image.png
image.png
 
Hili si tukio la kwanza kwa Waafrika
Mheshimiwa aeleze 'sintofahamu ' ni kitu gani katika udhalilishaji aliofanyiwa binti yetu

Kwamba, balozi anasimama na serikali ya India kuita uhalifu 'sintofaham'

Balozi hajaona mahojiano na kamishna wa bangalore na jinsi alivyoshindwa kujibu maswali na kujichanganya

Balozi pengine kwa hofu tu ya kazi anajikuta akiungana na wahindi katika kadhia hii

Hapana, mheshimiwa balozi kwa hili tunakupinga na tunaeleza shaka juu yako
 
Aondoke huko India kama ameshindwa kutuwakilisha sintofahamu ndio nini? Angevuliwa nguo mkewe au mwanaye mbele ya umma angesema hivyo?
 
Back
Top Bottom