Balozi Awakumbuka Watanzania Kwa Ujio Wa Membe!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Awakumbuka Watanzania Kwa Ujio Wa Membe!!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Chupaku, Jan 7, 2010.

 1. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ifuatayo ni taarifa ya kutoka Ubalozini kwa Watanzania waishio Canada..........................................


  Kwa niaba ya Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, naomba kuchukua fursa
  hii kuwajulisha kuwa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje
  na Ushirikiano wa Kimataifa anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini
  Canada kuanzia tarehe 11 Januari hadi 15 Januari, 2010.

  Akiwa Ottawa Mhe. Waziri Membe atapenda kukutana na Watanzania walioko Canada. Ubalozi unafanya utaratibu wa kupata ukumbi kwa ajili ya
  mkutano huo ambao utafanyika siku ya tarehe 12, Januari, 2010 jioni
  saa Kumi na Mbili na Nusu hadi saa Tatu na Nusu usiku (6:30Pm-9:30Pm).
  Tutawajulisha sehemu ya mkutano na anuwani ya shughuli hiyo kabla ya
  mwisho wa juma hili hivyo tunaomba muweke shughuli hii katika ratiba
  zenu.

  Aidha, tunaomba kila atayepata ujumbe huu atusaidie kumjulisha/kuwajulisha Watanzania wenzetu ambao hatukuweza kuwatumia
  barua pepe hii kutokana na kutokuwa na anuwani zao.

  Kama mnavyojua shughuli ni watu na watu ndiyo sisi sote hivyo tunaomba
  tujitokeze kwa wingi kuja kukutana na Mhe. Waziri Membe ambaye kama
  wengi mnavyokumbuka aliishi hapa Ottawa wakati akifanya kazi kwenye
  Ubalozi wetu huu.

  Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu,

  Kny Balozi​
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Nyie watu wa Canada bwana . Nini kinaufanay Ubalozi uje hapa JF kupeleka taarifa hizi ina maana hamna touch na watanzania siku zote hizo ? Je mna uhakika kwamba watu wa Canada wote wanasoma JF amakuna kitu kinatokea mie sijui?
   
 3. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Katumwa huyo kwenda kuchukua mchango kwa Sin bin Clair?
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Yaani haya majungu kumbe yapo kila mahali, sasa mkuu hebu fafanua hapo balozi huwa hawakumbuki kutokana na kifungu kipi cha sheria ya jamhuri yetu?

  - Au mliwahi kwenda huko ofisini mkafukuzwa na kukataliwa kusaidiwa, I mean balozi wetu hakupelekwa huko kuwakumbuka wabongo, wabongo wanatakiwa wajiandikishe ubalozini wao wenyewe kwa hiari yao wanapofika tu kwenye nchi je mmetimiza hayo au ni majungu tu haya ya kukumbukana?

  Respect.


  FMEs!
   
 5. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu Membe anakwenda chukua per diem yake Canada na kupumzika!
  Kama mbongo uko Canada ni wastage of time,bora ufanye shughuli zako !Ni hawa wanatetea serikali ya kifisadi ya CCM.Gharama za usafiri na masurufu zinaweza kununua vitanda pale Temeke hospital.

  Kama wewe ni mtoto wa mafisadi bongo na watu wako kwenye system,good for you to attend.
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0


  - Duh! Very interesting!

  Respect.


  FMEs!
   
 7. b

  bnhai JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Duh aliyoiandaa hiyo taarifa!!! Yaani hata wahudhuriaji wenyewe inabidi wafikirie kwanza. Anakuja kukutana kufanya nini? Ajenda au ni kukusanyana tu na kutazamana? Halafu mhh shughuli ni watu .......... (nt attractive)
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I guess atawaambia Tanzania Wasomi warudi Tanzania kuchangia maendeleo ya nchi!
  What a cock up!
   
Loading...