Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 19
- Balozi wa Afrika Kusini nchini, Sindiso Mfenyana, ameishauri Tanzania kujifunza namna bora ya kunufaika na sekta ya madini kutoka nchi za Botswana, Namibia na Afrika Kusini, ili sekta hiyo iweze kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.
- Alisema nchi yake imenufaika kwa madini kwa kuwa sera yao ilieleza bayana kwamba wawekezaji wanapaswa kwanza kuimarisha huduma za kijamii katika maeneo yanayozunguka miradi ya uchimbaji.
- Balozi Mfenyana alisema sera ya madini ya Afrika Kusini inaeleza kwamba jamii inayozunguka migodi inapaswa kuwa mwanahisa wa mgodi husika na kwamba mwekezaji analazimika kujenga shule, hospitali na huduma nyingine za kijamii.
- Alisema sera yao pia hairuhusu wawekezaji kuendesha shughuli za uchimbaji katika jamii masikini jambo linalowalazimisha kuwasaidia kwanza wananchi.
- Alitoa mfano kuwa Botswana imeweka utaratibu wa kuwafanya wawekezaji katika sekta hiyo kujenga viwanda vya kusafisha madini ndani ya nchi hiyo jambo lililoisaidia kunufaika na rasilimali hiyo.
- Mengi alimwambia Balozi huyo kuwa Tanzania imekuwa ikipata asilimia tatu ya mrabaha katika migodi yake kiasi alichosema ni kidogo na kueleza kuwa wawekezaji wamekuwa wakichimba na kuondoka na madini huku wakiacha mashimo.
.......................................................................
Kwa bahati mbaya sina weledi wa masuala ya uchumi na hisabati, naomba mnaoelewa masuala haya mnitanabaishe.....ina maana makampuni ya madini yanachukua asilimia 97? Kama ndio ukweli, kuna haja ya kuendelea kuchimba hayo madini? Tunamnufaisha nani? Inanikumbusha kauli ya JKN kuwa kwa kuwa madini yako ardhini na hayaozi, basi tusubiri tukiwa na utaalamu wa kuyachimba ndio tuyachimbe. Haraka ya nini? Kwa mahesabu na tafsiri yoyote, 3% ni sawa na hakuna. Vigezo gani vinatumika kwa wataalam wetu kukubali mgawo huu?