Balozi aishauri Tanzania ijifunze kwa Botswana inufaike na madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi aishauri Tanzania ijifunze kwa Botswana inufaike na madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Oct 31, 2009.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  • Balozi wa Afrika Kusini nchini, Sindiso Mfenyana, ameishauri Tanzania kujifunza namna bora ya kunufaika na sekta ya madini kutoka nchi za Botswana, Namibia na Afrika Kusini, ili sekta hiyo iweze kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.

  • Alisema nchi yake imenufaika kwa madini kwa kuwa sera yao ilieleza bayana kwamba wawekezaji wanapaswa kwanza kuimarisha huduma za kijamii katika maeneo yanayozunguka miradi ya uchimbaji.

  • Balozi Mfenyana alisema sera ya madini ya Afrika Kusini inaeleza kwamba jamii inayozunguka migodi inapaswa kuwa mwanahisa wa mgodi husika na kwamba mwekezaji analazimika kujenga shule, hospitali na huduma nyingine za kijamii.

  • Alisema sera yao pia hairuhusu wawekezaji kuendesha shughuli za uchimbaji katika jamii masikini jambo linalowalazimisha kuwasaidia kwanza wananchi.

  • Alitoa mfano kuwa Botswana imeweka utaratibu wa kuwafanya wawekezaji katika sekta hiyo kujenga viwanda vya kusafisha madini ndani ya nchi hiyo jambo lililoisaidia kunufaika na rasilimali hiyo.

  • Mengi alimwambia Balozi huyo kuwa Tanzania imekuwa ikipata asilimia tatu ya mrabaha katika migodi yake kiasi alichosema ni kidogo na kueleza kuwa wawekezaji wamekuwa wakichimba na kuondoka na madini huku wakiacha mashimo.
  .......................................................................
  Kwa bahati mbaya sina weledi wa masuala ya uchumi na hisabati, naomba mnaoelewa masuala haya mnitanabaishe.....ina maana makampuni ya madini yanachukua asilimia 97? Kama ndio ukweli, kuna haja ya kuendelea kuchimba hayo madini? Tunamnufaisha nani? Inanikumbusha kauli ya JKN kuwa kwa kuwa madini yako ardhini na hayaozi, basi tusubiri tukiwa na utaalamu wa kuyachimba ndio tuyachimbe. Haraka ya nini? Kwa mahesabu na tafsiri yoyote, 3% ni sawa na hakuna. Vigezo gani vinatumika kwa wataalam wetu kukubali mgawo huu?
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  HII POINT IMEPUUZWA KWA WINGI SANA! Hii ingekuwa sera No.1 ya nchi. Ni nafuu kufunga migodi kama madini yanaenda kusafishwa nje. TUNAIBIWA!!
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu sio tu imepuuzwa miaka mingi ni kwasababu watu wameamua kujifanya hawajui kabisa kama kuna kitu hicho.

  Mwaka 2006 baada ya JK kushinda Urais alipeleka timu ya watalaam Botswana kujifunza juu ya wanavyofaidika na madini, Binafsi nilipata faraja sana kwasababu nilijua watatoka na kitu huko na wakitoka na hicho kitu kitakuwa cha manufaaa, Kumbe mweee Khaaa!

  De Beers Kampuni mbia wa kuchimba Almasi Botswana ndio wamekuwa wabia wetu wa Almasi ya Mwadui miaka mingi sana. Lakini nakwambia huko Botswana Terms ziko tofauti sana.
  1. De Beers hawakupewa tenda pekee yao kuwa wawekezaji kwenye sekta ya madini, kilichotokea ni kuwa Serikali iliunda kampuni ambayo ni kama agence na hii agence imeunganisha share na De Beers kwa uwiano wa 50:50 na kampuni mpya inaitwa Debotswana ikiwa ni muunganiko wa majina mawili De Beers na Botswana

  2. Kwa vila hizo kampuni mbili zina uwiano sawa wa hisa kwa hiyo top menejiment ipo sawa, yaani wana wakurugenzi wawili, menegers wili (mmoja wa De Beers and mwingine wa Botswana) mpaka level fulani.

  3. Wafanyakazi wa kigeni imewekwa level ambayo ni mwisho kuajili, huwezi kuona sijui chini ya mgodi shift supervisor sijui plumber eti ni mgeni, hata mara moja, wageni ni kwenye nafasi ambazo kweli zinahitaji wageni na hakuna wenyeji wenye potentials za kujaza.

  4. Wageni wote walioko kwenye senior position wanapewa wazawa chini yao kama wasaidizi wao na jukumu la kuwatrain ili waje wachukue nafasi za wageni siku wanaondoka.

  5. Mgeni akishindwa kuprove kuwa mwenyeji aliyekuwa chini yake alimfundisha akaelewa, na ikaonekana kuwa mgeni hakutoa msaada kwa mwenyeji kuelewa ili aweze kuresume position yake siku mkataba ukiisha basi mkataba wake huwa hauwi re-newed ana mgeni mwingine anakuwa hired kujaza nafasi ya mgeni huyu aliyeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kumtrain mwenyeji.

  6. Mgawanyo wa rasilimali wanzopata ni De Beers wanachukua 60% na Botswana Government wanachukua 40%

  7. Baada ya mgawo huo (60:40) De Beers wanatakiwa kulipa kodi, kwa hiyo katika asilimia zao 60 za mgao wakiwalipa kodi wanajikuta wanabaki na 50:50

  8. Baada ya kodi wanatakiwa kulipa Mrahaba (ambazo ni kuendeleza maeneo ya jirani na jamii zinazozunguka mgodi) asilimia 3-5

  9. mwisho wageni (De Beers) wanajikuta wanaondoka na kitu chini ya asilimia 50.

  Kwa ujumla Botswana ni mfano wa kuigwa africa kwa jinsi walivyotumia madini yao, kuna maji safi yasiyokatika mjini Gaborone yanatoka kilomite 600 north karibu na Francis Town, angalia mabasi yao (mpaka yale marefu na hata ya ghorofa kama Uk) Bara bara four ways kila kilomita 50 kuanzia mwishoni mwa gaborone kwenda nje ya jiji. Mji mzima wa gaborone umezungushiwa barabara kubwa za four ways pembeni kwa ajili ya wale wenye haraka wasipite kati kati ya jiji na mgari ya city to city (Northen by Pass, Sourth bypass, east bypass)

  Kuna umeme na maji mpaka vijijini kabisa kama Tutume ni mbali sana mji wa Francis Town lakini kuna umeme na maji safi,

  Kila mtoto wa botswana anasomeshwa na serikali bure mpaka sekondari, baada ya hapo ndio kuna selection ya watoto wa kwenda University, secondary education ni universal.

  Vitabu kila mwaka vinagawiwa kwenye mashule ya serikali na vilivyotumika tayari serikali huvikusanya na kuvipeleka private schools kwa hiyo hakuna anayekosa kitabu Botswana.

  Kila kijiji kina dispensary (wenyewe wanaita clinic) na ambulance (labour inatoka nje ya nchi)

  Serikali hubadri magari ya idara zake kila miaka minne, na mgari yalitumika huuzwa kwa mnada wa wazi kwa wakulima, first priority ni mkulima, hakuna suala la kujuana wala nini, mkulima anakuja na document zake anaonyesha kuwa yeye ni mkulima (kila mtu ana kitambulisho na anafahamika kwa chief wake, Kota)

  Kwa ujumla Madini ya Botswana yameisaidia ile nchi, huwezi kujua kiasi gani wale jamaa wamefaidika mpaka ufike huko. Ndio maana sikubaliani na msemo "Miafrika ndivyo tulivyo" kwani wenyewe wakaumbia ukienda kwao kuwa africa ni North of Zambezi sio kwao, maana haya matatizo ya umaskini ni nyinyi.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  That's it Mbogela in short Gaborone is one of the fiew cities if not alone where barabara ni nyingi kuliko watumiaji, I mean general traffic magari, watu, pkpk you name it.

  Suprisingly most of the govt and private institutions are run by Tanzanians!!!

  He! Mbogela by the way Mogho/ Mogo hotel bado ipo??????????
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  This is no-man`s-land guys!..who cares?..Personal interests are superceeding the mass interests!..The president is on Safaris day-in, day-out!...huh! shame on us!!
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wanaochimba madini wamekwisha lipa 10% kwa viongozi wa CCM sasa mnataka nini zaidi??

  Kama tunataka mabadiriko labda tuanzishe vikosi vya wapiganaji kama Niger delta vinginevyo CCM hawaambiliki.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wizara ya nishati na madini anahitajika magufuli labda things can change
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Na jinsi wanavyofaidika hawawezi kuthubutu kumweka huko...atawadhalilisha kijinsia!
   
 9. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mzee, huu ulikuwa uendelezaji wa usanii!! Study za mwanzo za namna wenzetu wanavyoendesha uwekezaji ktk madini ndio zilizaa Meremeta na hao kina Mwananchi et al.

  Tanzania imekuwa nchi ya Chukua Chako Mapema, unless system yote na mindset za watu zibadilike,hakuna cha maana kitakachofanyika!!
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu sina uhakika siku nyingi sijaingia Botswana lakini nadhani kwa mara ya mwisho nilisikia wale Watanzania waliiachia alafu walikuja wakafungua nyingine pale njia panda ya Mochudi na Gaborone - Pilane
   
 11. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ...ZOEZI LINAENDELEA MPAKA KILA KITU KIISHE CHINI YA ARDHI....


  • RAIS Jakaya Kikwete ameitaka serikali mkoani Mbeya kufanya uwezekano wa kuhamisha gereza la Songwe na kulibomoa ili kuanza uchimbaji wa madini ya alminium ambayo yamebainika kuwepo katika ardhi ya gereza hilo.

  • ''Ni muhimu viongozi wa serikali ya mkoa kuchukua jukumu la haraka kutekeleza hili na si kuacha rasilimali za kukuza uchumi zikakaa bila kuzalisha na kubaki kwenye ardhi,'' alisema Kikwete. Aliongeza kuwa; ''Kwa sasa tunapaswa kufanya mikakati ya kubomoa gereza la Songwe na kujenga eneo lingine kisha kuanza uchimbaji rasmi kutokana na eneo hilo kuonekana kuwa na madini mengi ambayo yanaweza kuongeza pato la nchi na kukuza uchumi''.
   
Loading...