Ninavyofahamu mimi, mtu akiwa na ngoma huwa hafanyiwi operation kubwa hata ile ya uzazi. Lakini kama ambavyo inavyojulikana leo, Balali alifanyiwa operation kubwa huko Boston. Kwangu mimi huo ni uthibitisho tosha kuwa kweli hakuwa na Ngoma.
Ndugu zangu kwa mtazamo huu tutaondoka wengi sana na hii ngoma! Nani kawadanganya ati mtu mwenye ngoma hafanyiwi operesheni kubwa, ati hata ile ya uzazi! Jamani mna uhakika na haya mambo? Operesheni watu wenye ngoma wanafanyiwa sana, na wanapona vizuri tu, kulingana na hali aliyokuwa nayo kabla ya operesheni hiyo. Binafsi nimeona watu wawili ninaofahamu wana ngoma, kinamama (si wa kificho, waliweka wazi hali zao), na walifanyiwa operesheni za uzazi, na walishauriwa na madaktari wao kuwa hiyo ni njia bora ya kupunguza uwezekano wa watoto wao kuambukizwa. Tena hiyo ilikuwa 1996, kabla hata matumizi ya hizi dawa za ARV hayajashika kasi kama sasa hivi. Na marafiki zangu madaktari (MD's) wamenithibitishia kwamba mtu kuwa HIV positive si kipingamizi cha kumfanyia operesheni kama inahitajika. Na nina uhakika wako MD's pia kwenye hii forum naomba nao waseme, maana nikisema mie peke yangu wengine mtadai "ngwini"! Sasa nyie danganyaneni ati mtu akifanyiwa operesheni kubwa basi ndo hana ngoma, kalaghabaho!