BAKWATA Yakataa Serikali 3

BAKWATA Yakataa Serikali 3

Serikali mbili ni mfumo kristo, ila sishangazwi na Bakwata kuwa na msimamo huu kwa sababu ipo kwa hisani ya ccm.
 
Katiba ni ya wananchi siyo ya bakwata nchi Haina dini hatutaki udini wa kupelekwa kwenye suala la katiba
 
Tanzania=Tanganyika+Zanzibar

Mimi mtanganyika,ninaidai tanganyika yetu huru.
 
Nionavyo mm ni heri ya kuwa na serikali 1 yenye nguvu kuliko s. 2 ama 3. Kwann napendekeza s.1 ? Kwanza gharama uendeshaji w s. Zitapungua, Rais 1, wazir mkuu na hata baraza la mawazir litapungua. Nashindwa kuelewa kwann s.1 haikupewa kipaumbele. Unajua kwa serikali 2 lazima kuna upande ktk muungano utaingia gharama zaidi. Iwe n viswn au bara, nawaomba wote wenye mapenzi mema na Tanzania kila mmoja na imani yake amwombe Mungu awape hekima, busara na maarifa ktk maamuzi yote yanayohusu mustakabali wa nchi yetu Tanzania
 
Kama ni hivyo unaonaje tukiwa na NCHI MOJA NA SERIKALI MOJA ili tuwe na manufaa ya kweli ya kiuchumi na kijamii?. Pia tutakua na umoja na mshikamano wa dhati na pia tutaokoka gharama za kuendesha serikali tatu. Unaonaje mkuu?
wazo langu hili
 
Wanaotaka serikali tatu ni wale waliopanga kugawana vyeo wala siyo kuimarisha nchi.

Mkuu, mimi naona kama l engo ni kupunguza vyeo basi tutake serikali moja. Hii itafanya kuwe na rais mmoja. Idadi ya mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi ..nk waliopo katika serikali hizi mbili itapungua karibu kwa asilimia 50%.
Unajua pia kuwa Zanzibar hawataki serikali moja.
Hali hii ndiyo iayotulazimu baadhi yetu kudai serikali tatu na wala si suala la kutaka vyeo. Sina uhakika kama wanaotetea serikali mbili kama lengo lao ni vyeo, kwani walitakiwa watete serikali moja.
Tunapotoa mawazo yetu ni vema kuwa objective badala kuwa na sweeping statements.
 
Hoja zenu za kutaka Tanganyika ni dhaifu na zimetawaliwa na chuki na ulevi.
Ni zao la chuki aliyo ipandikiza mtikila. Hakuna manufaa ya kiuchumi wala ya kijamii yatakayo patikana kwa kurudisha serikali tatu. Achaneni na siasa za chuki na jazba

Sasa wewe mwenye upendo na hekima tufahamishe manufaa ambayo watanganyika tunayapata kwa kuunganika na zanzibar,ukilinganisha na haki na fursa wanazopatapata wazanzibari hususan wapemba huku tanganyika. Kama huna hoja bora kujinyamazia au utakosa hela lumumba?
 
Sasa naanza kuamini kwa nini tasisi nyingine za kiislamu zinaipinga Bakwata,sasa nimeanza kuelewa ila naogopa kutoa maoni yng isije ikanishukia dhahama,ccm bwana matawi hadi kwenye imani?
 
Serikali mbili ni mfumo kristo, ila sishangazwi na Bakwata kuwa na msimamo huu kwa sababu ipo kwa hisani ya ccm.

Kwa siku ya leo unaweza ukashinda tuzo ya juha bora wa siku,maana waliotoa kauli ya kutaka serikali 2 ni taasisi ya kiislamu,na ndiyo uzi unavyozungumzia sasa wewe loh!! Hebu nenda kawa mchungaji mtikila akuombee upone.
 
Mnasema serikali mbili ya Zenj na Serikali kuu ya muungano. Sasa mmeambiwa serikali ya Muungano (ambayo kwa mantiki ndiyo kuu maana inatoa Rais wa muungano ambaye ndiye amiri jeshi mkuu) inaye Waziri wake mkuu lakini hana mamlaka ya kiutendaji ndani ya sehemu fulani ya hiyo jamhuri, ndio nini hiyo?
Nima imani kuwa kama Pinda aliwahi kwenda Zanzibar basi ni wakati wa sherehe za mapinduzi halafu huyo unamwita mtendaji mkuu wa serikali ya Muungano huo sii ni usanii wa kitoto? Huwezi kurekebisha hilo kwa sasa bila kuvunja nguvu za katiba ya Zanzibar ya 2010, na hiyo wenyewe wamesema HAIGUSWI ASILANI. Dawa ni nini? Ni kuunda serikali ya Tanganyika au wakikubali Wazenji kuwa na serikali moja.
Hapa tusidanganyane tatizo linafahamika liko wapi. Ni Zanzibar ila wakubwa wanashindwa kutamka.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Acha ujuha sababu zimeainishwa katika rasimu ya katiba,hivi kwa nini ccm inatetewa zaidi na wapumbavu?

Lugha ni kali sana ila ina ka ukweli ndani yake. Punguza makali mkuu.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Naona tunakoelekea itakuwa ni Kura kati ya Wakristo (3) na Waislam (2); maana waislamu wanaona Zanzibar ikijitenga na kuwa serikali kamili mara moja itakuwa nchi ya Kiislam huku Tanganyika ikichagizwa kuwa nchi ya kikiristo. Kazenji kadogo na kanategemea Bara. Haha ha kazi ipo. Ngoja niishie hapa wasije wakakaba wenye Zanzbar yao.
hujatulia we mtu, akili yako yote ipo katika udini tu basi.
 
Muundo ambao utaimarisha umoja na mshikamano wa taifa hili ni serikali mbili.
Kama muundo wa serikali mbili utaimarisha "umoja na mshikamano wa taifa" kwa nini kuna hili timbwili na mpasuko wa kutaka kubadilisha muundo wa nchi toka siku ya kwanza miaka 50 iliyopita, why?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom