BAKWATA Yakataa Serikali 3

BAKWATA Yakataa Serikali 3

Wee waache wafanye hashuo lao tu! Mwisho wa siku huo upuuzi wanaouandika kwenye katiba lazima ukubaliwe na majority ya Tanganyika na majority ya Zanzibar!
Naamini katiba inaweza ikapita Tanganyika, but nauhakika katiba itafeli kwa kukataliwa Z'bar!
Na hapo kitakachofata ni Mungu aturehemu! CCM wanacheza ngoma wasioijua!
Unajidanganya ndugu. Watz wengi hawana shida na serikali 2 including zanzibar. halafu hilo neno uturehemu litoe. hilo hutumika kwa marehemu.siyo mtu aliye hai.
 
Mkisharudisha Tanganyika mtanufaikaje? ili iweje. Hongera bakwata.


Huu muungano tunanufaika nini? how possible unagharamia Mke wa mwenzio na anaegegeda ni mwingine? Shem on you CCM!!! thwuuuu!!" uchafu kabisa.
 
Mnauhakika mnataka Tanganyika yenu? Kwani sisi tunasoma kutoka wapi? Alieiroga nchi hii kashakufa
 
Unajidanganya ndugu. Watz wengi hawana shida na serikali 2 including zanzibar. halafu hilo neno uturehemu litoe. hilo hutumika kwa marehemu.siyo mtu aliye hai.

Mbona hapo nakubali sana?
Sidhani kama ulielewa nilichokiandika pale!
 
hakuna utofaut wa bakwata na ccm,hao mashekh wa bakwata ni wajahanam tu kwa sababu ya unafiki wao....
 
Kuna mtu anaweza kupata taarifa ya hawa BAKWATA walipendekeza serikali ngapi wakati wa kutoa maoni kwa tume?@Barubaru

CCM wawe waangalifu, wanakoipeleka jamii ya Watanzania sio kizuri. ccm wanaamzisha mgogoro ambao hawataweza kuzima. Sio kila mbinu inafaa kwa kila jambo na kwa wakati wote.
 
Naona tunakoelekea itakuwa ni Kura kati ya Wakristo (3) na Waislam (2); maana waislamu wanaona Zanzibar ikijitenga na kuwa serikali kamili mara moja itakuwa nchi ya Kiislam huku Tanganyika ikichagizwa kuwa nchi ya kikiristo. Kazenji kadogo na kanategemea Bara. Haha ha kazi ipo. Ngoja niishie hapa wasije wakakaba wenye Zanzbar yao.
Akili yako ni mbovu, huna Takwimu kichwa cheupe, ulimsikia Kardinari Pengo alitoa msimamo gani?

Ni dhehebu gani la kikiristo linapenda utengano? Linapenda Vita, halina uvumilivu?

Nadhani huwajui Wakristo vizuri wala huwatambui Waislamu kwahiyo wewe ni mchawi.
 
Ukitaka ujue akili zao angalia yafuatayo.
1. Shule bora tanzania hazifungamani na upande wao
2. Mikoa masikini,iliyorudi nyuma kimaendeleo kama mtwara, lindi,Tabora,kigoma,singida,pwani n.k wao ndio wengi.
My take. Hakuna haja ya kupoteza kuwajidili hawa BAKWATA maana hawawezi kufikilia zaidi ya hapo.
 
Bakwata ni ccm no2 ndio maana hata waislam wezao wanawakandamiza
 
Kama ni hivyo unaonaje tukiwa na NCHI MOJA NA SERIKALI MOJA ili tuwe na manufaa ya kweli ya kiuchumi na kijamii?. Pia tutakua na umoja na mshikamano wa dhati na pia tutaokoka gharama za kuendesha serikali tatu. Unaonaje mkuu?
kwa hoja hiyo wazazibar wako tayari muungano ufe,wao sio mbumbumbu kama watanganyika kupoteza jina lao
 
Mimi nlichosikia ni bakwata kutounga mkono maoni na msimamo wa waislam kutaka serikali tatu ikiwa na maana zanzibar kuwa dola huru, hayo ni maoni ya waislam. Sasa bakwata kama vibaraka wa serikali na wao wanahaki yao ya kutoa maoni yao na sio kupinga maoni ya waislam, au ndio wanatekeleza jukumu lao la kuwavuruga waislam? Maana bakwata haikuwekwa ila kuwagawa na kudhoofisha jitihada za waislam. Sasa bakwatakama haiungi mkono serikali tatu itamke inataka ngapi na kwa sababu zipi kama kweli wao ni watu makini
 
Bakwata kiongozi wao ni "MFUMO K...." -Ustadh Ilunga
 
Majority gani wamepinga watu 49 ndiyo majority we waajabu kweli.
Hivi huu ujinga wenu mtaacha lini?maana sasa hivi kazi ni kutukana na kukashifu kazi ya Tume ya Warioba,jana nilimsikia kinana nikasikitika saana nikona kweli CCM nijanga.Hivi kama mlikuwa hamtaki maoni ya wananchi kwanini mliunda tume?maana imetumia kodi zetu. Leo hii inaleta maoni ya wananchi nyinyi kazi yenu ni kuikebehi na kuizalilisha mbele ya jamii hii siyo sawa kabisa
 
Unajidanganya ndugu. Watz wengi hawana shida na serikali 2 including zanzibar. halafu hilo neno uturehemu litoe. hilo hutumika kwa marehemu.siyo mtu aliye hai.

Aliekwambia serikali mbili hazina shida bila shaka ni raisi wako?

Na neno turehemu hutumika kwa yeyote acha kukariri aliekwambia tulio hai hatutaki kurehemewa nani?

(Nataka rehema si sadaka)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom