Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Alhaj Nuru Mruma, amesema baraza hilo linawahimiza Waislamu na Watanzania kwa ujumla kulinda amani iliyopo nchini, kwani bila uwepo wa amani shughuli za kimaendeleo katika jamii haziwezi kufanyika, na hata ibada pia hazitafanyika.
Akizungumza mara baada ya kuswaliwa kwa swala ya Eid al-Adh-ha kitaifa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Alhaj Mruma amesema:
"Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linatoa wito kwa kila Mtanzania, kwa nafasi yake, kuilinda na kudumisha amani ya nchi yetu, kwani bila amani hakutakuwa na maendeleo yoyote katika jamii, na hata fursa ya kufanya ibada haitakuwepo."
Alhaj Mruma ametoa wito pia kwa wote watakaoshiriki katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kufanya siasa safi na kutumia vizuri haki hii ya kikatiba kupitia ushiriki wao wa kuchagua viongozi au kuchaguliwa kuwa viongozi.
Amehimiza pia kuwa mamlaka zinazohusika na kusimamia uchaguzi zitende haki wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi huu mkuu, ili haki hii ya kikatiba ipatikane kwa kila mwananchi.