BAKWATA ni taasisi ya Serikali?

BAKWATA ni taasisi ya Serikali?

Bakwata imeundwa Nahao wajuu wa serikali ndio maana waislam wanaoelewa mambo wala hawakubaliani nao
 
Waislamu wanapunguzwa nguvu kidogo kwa lugha nyingine watakuwa wanapewa maagizo na serikali maana kama vile bunge, mahakama, na tahasisi zingine bado sasa wakristo sijui wataongwa nini
Watazidi kujazwa serekalini kupitia teuzi mbalimbali
 
Makonda kama mwanamchi wa kawaida atasaidia kupatikana kwa kiasi husika kujenga hilo jengo...!

Ninge shangaa kama Bawacha na roho za husda lingewapita hili..
Kwanini huo mchango asinunulie madawati anayoomba tumchangie?

Kwanini asinunue vitanda vya pale hospitalini Temeke ama hospitali za Ilala?
 
duniani kuna chama tawala ambacho hakiongozi serikali?
Ndio, inategemea matokeo ya uchaguzi. Inweza kuongoza kwa wingi wa viti lakini viakuwa havitoshi kuunda serikali bila kuungana na vyama vingine.

Makubaliano yanaweza kufikiwa na kumfanya mtu kutoka chama kidogo akaweza hata kuunda serikali. Mfano mzuri yae yaliotokea anzibar. ZPPP chama kidogo kilitoa Waziri mkuu, Moh'd Shamte baada ya kukabiliana na chama kikubwa ZNP
 
Si hii nchi haina dini kabisa?

Na vyombo vya dini vinatakiwa kuwa huru kabisa?

Sasa Rais anakwenda kwenye baraza la Iddi anatoa briefcase yenye pesa taslimu...why? kuna nini?

Sasa mkuu wa mkoa anakuja na mradi wa kujenga makao makuu ya BAKWATA.Mradi wa bilioni 5.....

Je, haya yote yanafanyika kwa mapenzi mema au kuna kitu?

Hiko kitu ni nini hasa?

Serikali inajaribu ku achieve nini kwa 'kuisaidia huku' BAKWATA?

Uhuru wa BAKWATA kuikosoa na kuikemea serikali kama zilivyo taasisi zingine za dini ndo 'umeshakwenda'?

Nani muathirika wa haya yoote?
10.jpg

Aidha, Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amemkabidhi Rais Magufuli hundi ya Dola la Marekani Elfu Hamsini na Tatu (USD-53,000) sawa na Shilingi Milioni 116 za Kitanzania kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shule mbalimbali hapa nchini na pia amekabidhi hundi ya Dola za Marekani Elfu Ishirini na Moja (USD-21,000) sawa na Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Mambo haya yananoga na kunogeshwa!

Link Rais akutana na Kiongozi Mkuu wa Dawoodi Bohra na Mufti Mkuu wa Tanzania
 
Kuna vipaumbele vingi vya Jiji la Dar na hili la kujenga makao makuu ya BAKWATA kamwe haliwezi kuwemo katika vipaumbele vya Jiji.

Huyu Makonda naye ni debe tupu, alipewa sifa nyingi alipokuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni kumbe utendaji ni ZERO. Hizi pesa ni kutoka hazina za kuwanunua hawa wasiojitambua ili waendeleze unafiki wao kuhusu dikteta uchwara.

Si hii nchi haina dini kabisa?

Na vyombo vya dini vinatakiwa kuwa huru kabisa?

Sasa Rais anakwenda kwenye baraza la Iddi anatoa briefcase yenye pesa taslimu...why? kuna nini?

Sasa mkuu wa mkoa anakuja na mradi wa kujenga makao makuu ya BAKWATA.Mradi wa bilioni 5.....

Je, haya yote yanafanyika kwa mapenzi mema au kuna kitu?

Hiko kitu ni nini hasa?

Serikali inajaribu ku achieve nini kwa 'kuisaidia huku' BAKWATA?

Uhuru wa BAKWATA kuikosoa na kuikemea serikali kama zilivyo taasisi zingine za dini ndo 'umeshakwenda'?

Nani muathirika wa haya yoote?
 
Na ubwabwa pia Patience123

Hao Bakwata walishatekwa siku nyingi.
Ni lini ulishawahi kusikia wakiikemea serikali zaidi ya kuwasifu na kuwaombea dua?
Kumbuka yule mbunge aliyesema bakwata ni tawi la CCM,hakukosea, ndio maana wenzako wanapewa' viburungutu' vya hela.
 
Amani,
Mahakama ya Kadhi ilikuwapo toka nyakati za ukoloni.

Zilikuja kufungwa mwaka wa 1963 na serikali huru ya
Tanganyika.

BAKWATA ilianzishwa na serikali baada ya ''mgogoro''
wa EAMWS wa mwaka 1968.

Unaweza kuupata mkasa wote hapo chini:
Mohamed Said: BAKWATA SEHEMU YA KWANZA

Hizo ni series unaweza ukajifunza mengi...
Wee mchanganishi wa siasa za udini salaam
 
Makubaliano yanaweza kufikiwa na kumfanya mtu kutoka chama kidogo akaweza hata kuunda serikali. Mfano mzuri yae yaliotokea anzibar. ZPPP chama kidogo kilitoa Waziri mkuu, Moh'd Shamte baada ya kukabiliana na chama kikubwa ZNP
Duu, Kiswahili kigumu namna hii?

Hatuongelei vyama vikubwa na vidogo hapa.

Chama gani kilikuwa kinatawala lakini hakiongozi serikali?

Nyinyi watu wa pwani si mnafagiliwa sana kwamba mnajua Kiswahili?

Sasa eleza, chama gani duniani kinatawala lakini hakiongozi serikali.
 
Duu, Kiswahili kigumu namna hii?
Nakubali kuwa kiswahili ni kigumu. Bado hujaelewa kamaa 1+1=2. NImekutolea mfano ZNP ndio chama kiliokuwa tawala serikali ilikuwa inaongozwa na ZPPP
 
Si hii nchi haina dini kabisa?

Na vyombo vya dini vinatakiwa kuwa huru kabisa?

Sasa Rais anakwenda kwenye baraza la Iddi anatoa briefcase yenye pesa taslimu...why? kuna nini?

Sasa mkuu wa mkoa anakuja na mradi wa kujenga makao makuu ya BAKWATA.Mradi wa bilioni 5.....

Je, haya yote yanafanyika kwa mapenzi mema au kuna kitu?

Hiko kitu ni nini hasa?

Serikali inajaribu ku achieve nini kwa 'kuisaidia huku' BAKWATA?

Uhuru wa BAKWATA kuikosoa na kuikemea serikali kama zilivyo taasisi zingine za dini ndo 'umeshakwenda'?

Nani muathirika wa haya yoote?

Nyerere alikuwa na mbinu nyingi.
Nyerere aliwahi kusema msicheze na waisilamu watakuweka pabaya.
Nyerere alitaka kuwadhibiti waisislamu na ndipo akaja na wazo la BAKWATA.
Bakwata ina endeshwa na Serikali
Serikali ndio inayochagua mkuu wa Bakwata "Serikali ndio inayo chagua mufti au shekhe mkuu wa waisilamu"

Waisilamu hawajaachiwa kuchagua Mtu abaye wanahisi kuwa anawa faa kuwa shekhe wawo.
Serikali i natafuta mtu ambaye na wawo wataweza kumdhibiti.

Hapa ndio kosa lakini system ndio ipo hivyo. haitaki kuwapa mwanya waisilamu kujiamulia mambo ya wenyewe kama madhehebu mengine.

Mapdri wakubwa wote Tanzania huwa hawachaguliwi na serikali
Hapa kuna siri kubwa na watu wajiulize iweje
 
Kuna kosa gani Makonda kujenga - kwani majengo yameandikwa Mkuu wa Mkoa? Kama ni hivyo mbn mnashabikia Makonda kulipa kodi ya makontena

Makonda kama sehemu ya jamii lzm ajishughulishe na usaidizi ktk taasisi za dini
 
Back
Top Bottom