BAKWATA ifuate mfano wa KKKT

Katika Taasisi zenye kuwarudisha nyuma waislamu katika azma yao ya kupata usawa katika jamii hii ni BAKWATA.

Viongozi wakubwa wa BAKWATA wakishapata vimaslahi vichache kutoka kwa watawala basi hawajali kabisa mustakbali mpana wa waumini wa dini yao nchini.

BAKWATA kazi wanayoifanya ni kuwapa watawala moral authority hata pale wanapopaswa kunyooshewa vidole kwa matendo ya udhalimu
 
Mliongea nao lini tarehe ngapi na wapi hao waumini wao? Minute ziko was za kikao na za majina ya waliohudhuria hicho kikao Cha kuwaunga mkono? Mwenyekiti wa kikao alikuwa Nani na katibu alikuwa Nani?

Hao waumini wa kushukiwa akili na viongozi wako wapi miaka hii?
 
Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania limetoa muongozo kwa viongozi wake wa dini waache kujihusisha na siasa.

Jambo hili ni jema haswa ukizingatia kuwa Kanisa hilo lina waumini ambao wana mrengo wa vyama tofauti vya siasa kwa hiyo siyo busara kwa viongozi wa kiroho wa kanisa hilo wakijihusisha kuwa na upendeleo maalum wa kisiasa kwa vyama fulani.

Kwa bahati mbaya, BAKWATA ya Waislamu inatia aibu. Yenyewe imejinasibisha na watawala na kwa kila ajuaye kusoma matendo, basi hatoacha kung'amua wazi kuwa BAKWATA inatumika na watawala kisiasa na viongozi wake wanatumika kisiasa kwa ajili ya manufaa ya chama tawala CCM.

Tumeona kongamano la dini eti la kupongeza utendaji wa serikali ya awamu ya tano lililoratibiwa na sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam (BAKWATA), Ni dhahiri kongamano hilo ni kampeni ya wazi ya kisiasa ya kumpigia chapuo mgombea wa CCM kupitia mgongo wa dini. Hili ni jambo lisilokubalika hata kidogo!

Nawashauri BAKWATA, kama wanataka kuheshimika mbele ya jamii na umma wa Waislamu kiujumla basi wafanye mambo kwa maslahi ya Waislamu kuliko watawala.

Kwa mfano leo hii viongozi wa dini ya waislamu wako jela takriban miaka sita na ushehe, lakini BAKWATA wapo utadhani hilo haliwahusu. Sijawahi kumsikia Sheikh Mkuu au huyo Alhadi mpenda kukaa karibu na watawala hasemi chochote. Sijawahi kusikia wakiitisha dua kuwaombea afya viongozi hao au hata kuongea na waislamu wenzao juu ya hali na mustakbali wa Waislamu wenzao walioko jela na kesi yao kupigwa danadana kila kukicha.

Swali la msingi la kujiuliza, hao BAKWATA wanapojifanya kujali maslahi ya nchi kwa kutaka upendo baina ya wananchi wao wenyewe wameounyesha vipi huo upendo kwa waumini wenzao wanaosota jela huko miaka na miaka huko bila kuhukumiwa na mahakama nchini?

Kama BAKWATA imeshindwa ku-play role kunusuru Waislamu wenzao huko jela, watajifanya vipi kuwa wao ni chombo cha maslahi kwa nchi nzima?

Nawashauri BAKWATA badala ya huu ushirika na watawala unaowatia upofu kusimama kwa ajili ya masilahi ya waislamu basi waachane na kupenda ulua au kujikurubishakurubisha kwa watawala badala yake wakemee maovu, wasimamie haki, na wawaeleze watawala kuwa jambo kadha wa kadha siyo sawa!

BAKWATA isiwe nyapara wa kuwatuliza Waislamu wanapokuwa na madai yao ya msingi juu ya serikali, au isitumike kama tambala la serikali kujisafisha pindi inapokosea waislamu au hata umma.

Kwa mfano, majuzi hapa Sheikh Ponda alizungumza juu ya teuzi nchini zilizokaa kidini, kwamba katika awamu hik ya utawala, teuzi nyingi zimelalia upande mmoja lakini BAKWATA haikemei suala hili. Sasa katika hali kama hii BAKWATA haitopata heshima stahili kutoka kwa umma wa Waislamu nchini.
Mohamed Said anasemaje juu ya kadhia hii?
Hatua gani amechukua?

cc. Mohamed Said
 
Ndie baba wa Taifa na alilenga kudumisha uzalendo kama ilivyo China, Russia au suudia dini zote zinadhibitiwa kwa maslahi mapana ya Taifa. Huyo binti uliyemuweka ktk avatar Anamengi kisa ni kushindwa kudhibiti hizi dini
Kudhibiti akili za watu sio sawa na kudhibiti mifugo
 
Mliongea nao lini tarehe ngapi na wapi hao waumini wao? Minute ziko was za kikao na za majina ya waliohudhuria hicho kikao Cha kuwaunga mkono? Mwenyekiti wa kikao alikuwa Nani na katibu alikuwa Nani?
Viongozi wao ni wanufaika waumini si wanufaika
 
Back
Top Bottom