BAKITA mpo?

obedson

Member
Jan 20, 2010
29
45
Leo asubuhi nimejikuta nasakiliza kipindi cha watoto kwenye radio. Nimeshangaa watoto wanavyoulizana mafumbo, methali, nahau na hata jinsi wanavyosimulia hadithi zao. Kuna nahau moja ilitolewa na na mwanafunzi wa darasa la sita alisema "kama maisha ni safari kifo ni nini? Dah nikawa najaribu kukumbukia enzi zangu wapi bila mafanikio, nikasema ningekuwa sehemu walipo wale watoto ningempa mji wa kwenda. Na kwa bahati mbaya hata wale wanafunzi wenzake hawakuweza kutoa jibu sahihi hivyo kijana akaambiwa nakupa mji uende Mwanza. Mwanafunzi akakubali kwenda Mwanza na mimi kwa hamu nikawa nasubiri jibu itakuwa nini? Alitoa jibu "Kama maisha ni safari kifo ni konyangi". Nikawa najaribu kutafakari kwa muda mrefu kidogo ili nijue huyu mwanafunzi ana maaana gani, japo bado haileti maana ila nahisi sasa hiyo safari anayoijua huyu mwanafunzi ni safari lager. Sipati picha baada ya miaka kumi sijui tutakuwa na lugha gani.
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,104
2,000
Mkuu kuna wakati huwa najiuliza haya maneno
ya lugha adhimu ya kiswahili sijui mnaita
kutohoa !!!

Mfano haya maneno :
Digital ..... Dijiti
Decoder.....Kisimbuzi(King'amuzi)
Laptop........Dadavuzimpakato
Calculator.....Kikotoo

Nikija kwenye hilo neno "Safari" lililokupa
mshangao sana nadhani huyo mtoto
katohoa kwanamna alivyoona inafaa

Ni vizuri na muhimu hao Bakita wakafanya
utararibu wa kujiunga hapa JF kwa ufafanuzi
wa baadhi ya mambo kadha wa kadha

Tunavyo vyombo baadhi vimejiunga humu
mfano ni TCRA,KURUGENZI YA HABARI(CDM)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom