Serikali ilivyojenga shule na Vituo vya Afya kwenye kila Wilaya matatizo ya watz yaliisha? Mbona leo bado mnalalamika watoto wanakaa chini? Kwani nchi nzima watoto wanakaa chini?
Kwahiyo linalowezekana kufanyika lifanyike bila kujali litagusa watu wangapi? Kumbukeni ruzuku wanayopokea Chadema ni kodi zetu kwahiyo tunahaki ya kuhoji na kushauri matumizi sahihi. Utumie ruzuku kupanga wakati una uwezo kujenga. Hayo ni matumizi mabaya ya kodi zetu.
johnthebaptist,
Davido alitoa cheki ya 100m na akapigwa picha jamaa anakabidhiwa na bado inadaiwa kuna fungu lilitengwa kujenga nalo pia lilipigwa. Kifupi ni kwamba kama hauko biased huwezi kuridhishwa na mwenendo ulio kule ndani Chadema..
Kikubwa nilichojifunza ni kwamba CDM wana Praise team kali kuliko CCM maana wakianza kutetea uozo huwaashindi
Acha kuongea uongo kwa ajili ya kutaka kujustify hoja yako. Lini makada wa CCM wamelipwa na Serikali?
Kuilinganisha ruzuku wanayopokea CCM na Chadema eti ndo hoja ya CDM kutokua na mradi wowote wa chama unakosea sana. Hoja hapa ni kila chama kifanye shughuli zake kulingana na fedha inayopokea. Mathalani CCM ina majengo ya Ofisi zake katika kila Wilaya na mkoa hata kama nyingine zilitolewa kwa msaada. Lakini CDM kwa ruzuku inayopokea ingejenga hata jengo moja tu la makao makuu yake halafu hizo Ofisi zingine waseme hawawezi kutokana na ruzuku kuwa ndogo, atleast watu wangewaelewa.
Lakini hao hao CDM wana magari kibao ya M4C wanajua walipoyapata, sasa wameshindwa kutumia hizo njia walizonunulia kujenga Ofisi ya makao makuu yao?