Wazo la kufungua matawi ya CHADEMA kwa njia ya mtandao katika ofisi za umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo la kufungua matawi ya CHADEMA kwa njia ya mtandao katika ofisi za umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by miradibubu, Jan 20, 2012.

 1. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  WAZO LA KUFUNGUA MATAWI YA CHADEMA KWA NJIA YA MTANDAO KATIKA OFISI ZA UMMA

  Ndugu wanajamvi hasa wapenzi na wanachama wa CHADEMA nianze na kuwapa pole ya msiba mzito wa Mbunge na mpiganaji wetu Regia Mtema, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina!

  Nianze kwa kujitambulisha kuwa mimi ni mtumishi katika moja ya ofisi za umma. Kutokana na taratibu za kiutumishi haturuhusiwi kushiriki siasa sehemu za kazi. Hali hii imesababisha watumishi wengi katika ofisi za umma kubaki kuwa mashabiki na wapenzi wa CDM tu. Kwa maana kwamba wanashindwa kushiriki ipasavyo katika shughuli za chama kupitia matawi.

  Hali hii haitokani na uoga wa kuonwa na waajiri(hususani walio vibaraka wa ccm) bali ninadhani walio wengi kazi zao haziwapi fursa ya kutosha ya kwenda katika matawi na kujua nini kimejiri. Kukosa muda wa kuhudhuria katika ofisi za matawi inatokana na ukweli kwamba kwa baadhi ya watu wanafanya kazi kwa masaa mengi sana kiasi kwamba wakati mwingine wanajikuta hawana cha jumapili wala jumamosi.
  Licha ya ubize huu hawa watu huko kazini wanafahamiana kimitazamo na kimielekeo ya kisiasa katika huohuo ubize wao. Watu kama hawa ninaona hawatendewi haki kwa kudhaniwa kuwa hawapo pamoja na watu waliojitoa katika kusimamia ukombozi wa Watanzania.

  Ndugu zangu ubize huu unasababisha hawa watu wasionekane katika matawi na matokeo yake tunakosa mchango wao wa hali na mali.

  Nigusie usalama wa matawi haya katika mitandao: Ninadhani watu watakaopewa uanachama ni wale tu wanaofahamika itikadi zao za vyama kwa maneno na matendo, lazima mtu atume maombi ya kujiunga kwa watakaoridhiwa na makao makuu ya chama kuanzisha tawi katika eneo ofisi husika ya umma. Ninajua kuwa kunabaadhi ya mamluki watajiunga kwa ajili ya kutafuta umbeya hilo isiwe tabu tutazidi kupeana mawazo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.Kuwepo kwa matawi haya haimaanishi kuwa ninasema wafanye siasa kazini, bali itasaidia kuwaweka pamoja na kutoa mchango wao kwa chama kwa uhuru zaidi na kwa kuaminiana.

  Rai yangu kwa chama makao makuu wapime faida na hasara za hoja hii. Ila kwa upande wangu ninaona faida ni nyingi zaidi ya hasara hasa katika kipindi hiki ambacho chama hiki kinajiandaa kukamata dola . Hivyo basi tutumie njia zote za kuunganisha nguvu zetu pamoja sio wengine waendelee tu kuwa mashabiki na wapenzi, tunataka tuwe na wanachama wengi zaidi tuwezavyo ni muhimu sana.

  Hoja hii ichukuliwe kwa uzito na chama isiwe kama lile wazo la kuandikisha wanachama kwa matandao ambalo ninaona kama halisimamiwi ipasavyo. Ninashawishika kuona kuwa kuanauzembe kutokana na ukweli kwamba nimesajili vijana kadhaa unachama sasa imepita miezi kadhaa lakini sijajibiwa . Hii inashusha hadhi ya website ya chama ningeomba wahusika wajirekebishe.

  Ninakaribisha maoni kutoka kwa wanachadema(wanachama, wapenzi na mashabiki tu).

  Nimalizie kutoa pole kwa wanaarumeru wote kwa msiba wa mbunge wao, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA!
   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  watumishi wa uma huwa hawaoneshi ushabiki wa chama chochote kutokana maadili ya kazi.
   
 3. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Likwanda ninaomba tuwe wakweli hivi ni lini watumishi wa umma wameacha kuonesha mapenzi kwa vyama vya siasa au unataka kusema hauruhusiwi kuwa upinzani?
   
 4. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Matawi ya kwenye mitandao yanaweza pia kuhusisha watu wa sehemu nyingine kama vile ofisi binafsi sokoni n.k
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Kwa sheria, sera na mfumo wa sasa tulio nao,pamoja na TCRA wanavyofanya kazi zao, hayo matawi yatajulikana haraka sana na kusababisha disaster kubwa sana kwa hao wafanyakazi wa umma. Kikubwa hapa ni kuendelea kuipenda CDM toka MOYONI na sio kutoka MTANDAONI
   
 6. L

  Lsk Senior Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...thread imebeba wazo chanya.
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema hamna mbinu zingine? Naona mnapita nyia ya CCM ya mambo ya matawi
   
 8. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mawazo yako mazuri mkuu ila hawa Magamba wana hila mbaya hawa wewe acha tu lakn kwangu la msingi sana ingawaje nitakua mtumishi wa umma daima mapenzi yangu dhidi ya CDM hayatayumba kamwe,naipenda CDM ninaendelea kutengeneza vijana na hakika mawazo yao yanaendelea kubadilika na kuelewa umuhimu wa CDM
   
 9. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Wazo zuri, jumanne nilienda ofisi za tanesco kurasini kulipia bili, nilivaa skafu ya CDM so kuna dada teller wa pale aliponiona akaniuliza unaenda kuaga mwili wa marehemu Regia nikamwambia ndio, akaniulizia about skafu wapi anapoweza kuipata na bei, nikamueleza. So watumishi wa umma wengi wanakubali CDM
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Guda idea! But kwan ni dhambi ku2mia njia ya matawi?
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mwalimu Nyerere alijiuzulu kazi ya ualimu akaanzisha harakati za ukombozi.Je sisi kama wazalendo wa kweli tunangoja nini? simaanishi muache kazi zenu la hasha but namaanisha kwa sasa kuna fursa nyingi za kutumia ili kueneza harakati za ukombozi sambamba na kuimarisha chama!
   
 12. Ngatele

  Ngatele JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ni wazo zuri lakini utekelezaji nafikiri uwe tofauti. Mimi sijawahi kuingia mtandao wa CDM lakini napendekeza kuwa katika mtandao wa CDM kuwepo na jinsi ya kujiandikisha uanachama ampapo anayetaka atajaza form kwenye mtandao na kuituma na baadaye kulingana na eneo aliloonyesha kuishi katika form ataelekezwa kwenda kuchukua kadi ya uanachama kwenye ofisi ya eneo lake pindi itakapokuwa tayari, baada ya kuchukua ili uingizwe kwenye main register ya head office utaelekezwa ui-scan copy ya kadi ya uanachama na kuituma kwa address ya CDM utakayopewa na baada ya hapo uandikishaji utakuwa umekamilika na mawasiliano ya kimtandao ya chama yatafanyika baina ya CDM na wewe kupitia particulars utakazokuwa umezitoa kwenye form yako. Kama wasomi na watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu na wenye lengo la kuitwaa dola mwaka 2015 watajitoa kufuata utaratibu huu, CDM itaweza kupata wanachama wengi na hakutawa na haja ya sisi wafanyakazi kuonekana sana kwenye matawi kwani tutaweza kuwasiliana kwa mitandao.
  Nawaomba tuendeleee kuboresha wazo langu ili mwaka 2015 tuikomboe nchi yetu.
   
 13. zululima

  zululima Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni wazo zuri sana ila resarch makini inahitahijika. hima chadema. viva chadema. peopleeeeeeeees power. hadi kieleweke makamanda
   
 14. Kidafani

  Kidafani Member

  #14
  Jan 21, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Nahisi umeandika kabla ya kufikiri, kanusha kwa kubainisha hiyo unayoita nyia ya ccm, au thibitisha kuwa sasa ndo umefikiri kwa kuwa kutoandika.
   
 15. m

  mbukoi JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 253
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mimi ni mwanachama wa CDM lakini siungi mkono hoja ya kufungua matawi ofisini kwani hilo linaweza kuadhiri utendaji na hivyo kuzubaisha maendeleo ya nchi yetu. Ila ni vizuri mwanachama yeyote wa CDM akatumia muda wake wa baada ya kazi kukijenga chama bila kuathiri utendaji wake au kumwonea mtu kwa kuzingatia itikadi za kisiasa au kufanya uzembe kazini kwa kudhani anaikomoa serikali ya CCM kumbe analikosea taifa kwa ujumla.
   
 16. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda sana hyo mkuu,naomba nami nijuze naweza kuipata wapi hiyo skafu ya CDM,ni kweli watumishi wa umma ni wengi mno wanaopenda CDM,na sababu kuu nafikiri ni kutokana na kuelimika,hawawezi kuendelea ku support madudu..naomba nijuze wapi skafu naweza kupata na kwa kiasi gani mkulu
   
Loading...