Bajeti za wizara zote zichunguzwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti za wizara zote zichunguzwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CAMARADERIE, Jul 19, 2011.

 1. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Inaweza kuwa alilofanya Jairo wenziye wa wizara nyingine hulifanya....hivyo wote wachunguzwe....mimi nilikuwa sielewi watu woote kujazana Dodoma wakati wa bunge kumbe ndio hili?......no wonder foleni zimepungua Dar!
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ni wizara zote zenye taasisi nyingi za UMMA zinayafanya haya. Tumshukuru Jairo kalifanya kwa MAANDISHI kabisa. Beatrice( kwa uchungu wa mambo mengi) kayaanika haya bungeni. Mawaziri na wizara nyingine zinayafanya haya kwa usiri mkubwa na wakati mwingine mapema zaidi hata kabla ya kikao cha bajeti. Huu ni mfumo uliohalalishwa wa rushwa.
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hapo nimekupata
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  wakati wa bunge ni wakati wa mavuno, serikali ina pesa za kuchezea yaani 1b kuwalainisha wabunge, hii ni kashfa zaidi ya Richmond.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Imagine wizara 30....ndio maana Shibuda kaingia matatani manke kwa kuvuta hafai
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni common practise ila si unajua za mwizi arobaini
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Yalikuwa yanafanyika hata wakati mumewe ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini. Hakuyasema.
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huenda sasa mgao ukaisha
   
 9. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wote waliopokea hiyo Rushwa wafukuzwe- tuingie kwenye uchaguzi mdogo.
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  January Makamba kafanya vizuri kumuangusha yule baba. Haya ya Beatrice yasingekuwepo.
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi Takukuru wanasemaje kuhusu hii issue sababu hii ni Grand Corruption..., inabidi tuone mtu au watu wanafikishwa mahakamani
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Halafu ni rahisi kweli kulichunguza hili. Unaanzia pale kwenye akaunti ya Chuo cha Madini A/C No:5051000068 NMB-Dodoma.
   
 13. k

  kayumba JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo nakubaliana na wewe kuwa si Jairo pekee anayetegemea njia ya kuwalainisha wabunge. I can bet my hand on this! Lakini sasa, utawaona wabunge wetu walivyo watendaji wa kuwavizia watu fulani fulani watakubali yaishie hapa.

  Ukipima kwa makini utagundua kuwa, si msukumo wa uzalendo uliyosababisha Jairo kukomaliwa na Ngeleja kurudishwa na bajeti yake kwa sababu nimekuwa nikifuatilia hata bajeti zilizopita zilikuwa na mapungufu mengi kama ya hiyo ya Ngeleja. Wapinzani wakiyaongelea CCM wanawazomea. Leo hii uchungu umewapata. UNAFIKI MTUPU....!

  Lakini nawapongeza hata kama ni kwa unafiki, taifa litafaidika kwa kutokuwa na watendaji wanaoendekeza rushwa. Wito wangu kwa wabunge; Undeni kamati mchunguze hiyo pesa kapewa nani? na je wizira nyingine hazikupitia mlango huo????
   
 14. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndo maana wanakazana kugonga meza na kuzomea wapinzani! Kumbe wanapokea hela eh? Wanaangalia maslahi ya kwao wakati mamilioni ya watanzania nyuma yao wanakosa huduma muhimu.
   
 15. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Bajeti zote zikichunguzwa Bunge litavunjwa.
  Haya majitu ya ccm yanapenda sana rushwa.
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Na bado wanatetea posho ati za kugawa ''nauli'' kwa wapiga kura
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Yaani. Wee acha tu. Haya mambo "yamekuzwa" na Beatrice tu. Ilishakuwa sehemu ya maisha kwa Wabunge na wanasiasa wetu. Hamkumbuki hadi juzi tu kila bajeti ya wizara yoyote ikishapita tu ilikuwa inaangushwa "party" ya nguvu na kugawana bahasha wazi tu.
   
Loading...