Bajeti yawaunganisha CHADEMA na CUF.

Mgelukila

JF-Expert Member
May 27, 2012
224
43
Wajipanga kuipinga budget kupitia wabunge wao, wamechoka kuivumilia ccm Prof Lipumba kailinganisha na budget iliyopita kagundua madudu mengi, kila kona inakataliwa.
 
Ndoa ngumu jamani, kuolewa ni furaha na kutoa talaka ni huzuni.

Ndoa CUF imewashinda tayari?
 
CCM wameishiwa mbinu kabisa ..yaani huyo Dr.Mgimwa nadhani ndo atakuwa waziri wa fedha wa hovyo kuliko wote waliowahi kupita na kuhudumu cheo hicho toka nchi hii ipate uhuru..
 
Wapanga kuwatumia wabunge woa kuipinga budget sasa SUK itakuwa salama kweli? Hawajui ccm wako wengi bungeni? Wanapopambana na Cdm majukwaani hawajui wanapoteza muda, leo wanajua adui ni ccm siyo cdm, kweli wanadhamila ya dhati au kuwahi hoja mezani? Mtazamo wangu.
 
Kiongozi wa chama cha wananchi cuf mh. Lipumba atoa maagizo kwa wabunge wa chama chake kutokukubaliana na bajeti iliyosomwa juzi kwani haiwasadii wananchi wa tanzania na badala yake inawasaidia watu wachache,

swali ni je yeye kaumia kama wananchi wa huku bara au ni kwa sababu hajapata cheo serikalini kama mwenzake kule zanzibar aliyetulia? Au ndio na yeye anatafuta pakufia?

Source: mtanzania jumapili
 
Kama mwananchi anayo haki ya kutoa mawazo yake na kama kiongozi wa chama anao wajibu wa kutoa maelekezo kwa wabunge wake kuwakilisha msimamo wa cahama.
 
mke kubwa wa ccm ana maneno sana...mambo haya ni ya kuongea cumbani yataisha tu..huu ni upepo utapita tu !
 
Wanajukwaa ni jambo ambalo huwezi kuamini hasa pale chama kinapokosa kuwa na msimamo wa kuonesha dhamira thabiti kwa wananchi kuwa kina nia ya dhati ya kuwakomboa wanyonge. Leo CUF ina CCM, siku nyingine CUF na CHADEMA; hivi CUF wako upande upi hasa? Nawasilisha.!
 
Sii mara ya kwanza Lipumba kuunga mkono hoja za chama kikuu cha upinzani (CHM). Kumbuka aliwaagiza wabunge wa CUF kutia sahihi za kumwajibisha Pinda.
 
mke kubwa wa ccm ana maneno sana...mambo haya ni ya kuongea cumbani yataisha tu..huu ni upepo utapita tu !

hawa watu wanafanya watanzania bado ni watoto kwamba wanavyoongea wanapata umaarifu kumbe ni ujinga.

ikiwa mko katika gari moja halafu mmoja ni utingo na mwingine ni tandiboyi nani wa kumrekebisha mwenzake?
 
Huyu wa kumuangalia sana. Mwenzake wa Zenj baada ya kukaribishwa Ikulu kafyata majukwaani anaanzisha UAMSHO kwa chini chini, sijui huyu atakuja na lipi
 
Inapendeza sana kama wabunge wetu wanaamua kuacha itikadi zao za kisiasa na kuamua kuwa pamoja kwa maslahi ya taifa.
 
Jamani huyu Dr. mgimwa, hata mimi ni gamba orijino lakini hajanikalia sawa, maana hata presentation ya ile bajeti ilikuwa ni kichekesho. Sijui utendaji wake, lakini naona kaenda shule lakini hajaelimika.
 
Jamani huyu Dr. mgimwa, hata mimi ni gamba orijino lakini hajanikalia sawa, maana hata presentation ya ile bajeti ilikuwa ni kichekesho. Sijui utendaji wake, lakini naona kaenda shule lakini hajaelimika.

Zomba ndugu yangu sasa wewe nimeamini ni Mdini Mkulo kafanya madudu mangapi lakini ulikuwa husemi tumpe nafasi mpaka mwaka ujao kwi! kwi! ili tuwamalize
 
Wajipanga kuipinga budget kupitia wabunge wao, wamechoka kuivumilia ccm Prof Lipumba kailinganisha na budget iliyopita kagundua madudu mengi, kila kona inakataliwa.

Huyo lipumba ni kigeugeu sana haaminiki kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom