MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Hivi process yetu ya kufikia bajeti ipoje Tanzania? Najua nchi nyingi kama si zote duniani bajeti ya nchi inakua swala la kisiasa zaidi. Lakini je wataalamu mbali mbali wa serikalini haswa kwenye ngazi za wizara wana shirikishwa? Au baraza la mawaziri huji fungua tu sehemu na kutoka na bajeti yao kama wanavyo ona inafaa?
Samahani kwa kuuliza maana bajeti yetu ya Tanzania kidogo kwangu ni tungo tata. Sijui bajeti ina tokaje kutoka point A mpaka point B. Na je bajeti ikisha fikishwa bungeni ina pitia hatua gani? Je hupitia kwenye kamati mbali mbali au huwa kilishwa moja kwa moja na kujadiliwa na Bunge zima?
Sababu ya kuuliza ni kwa sababu karibia kila mwaka bajeti ina lalamikiwa. Badala ya kuangalia "bidhaa" iliyo kamilika nadhani ni muhimu kuangalia "bidhaa" hiyo ime pitia hatua zipi mpaka ika kamilika. Labda tatizo si kwenye bajeti inayo wakilishwa bungeni bali hata jinsi tunavyo tengeneza bajeti yetu kuanzia hatua za kwanza mpaka za mwisho.
Ushauri wangu mimi wa haraka haraka ni kwamba bajeti haswa kwenye hatua za mwanzoni zitengenezwe na wataalamu mbali mbali serikalini na kisha baraza la mawaziri ipokee draft ya bajeti. Na pia wakisha pata hiyo draft wafuate ushauri wa wataalamu. Maana ukweli ni kwamba wanasiasa wetu wana jifanya wajuaji mno na wataalamu wa mambo ambayo hata hawa yajui.