Bajeti ya mwaka huu itashindwa kutekelezwa kwa sababu ya Political risk inayoikumba Tanzania kwa sasa, Prof. Mpango anajua ila kaogopa kuliongehili

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Kwanza niisifu bajeti ya Jana kwa sababu Tu inaenda kuniongezea Ka mshahara kangu angalau kwa sh. 100,000.

Msishangae eti nasifia bajeti "Binadamu asili yake ni ubinafsi, siku zote husifia pale kwenye maslahi yake Tu" Ndo tulivo binadamu.

Nikienda kwenye mada ya bajeti ya Jana, kuna Jambo ambalo nimeliona na ninahisi linaweza kupelekea bajeti hii ambayo watu dizaini wanaiona ni nzuri isiweze kutekelezeka.

Kuna hili swala la kudorora kwa demokrasia na hali ya kisiasa nchini kwenye huu utawala wa Magufuli. Ukiangalia kwa Malini Sana, Tanzania kwa sasa haipo kwenye good terms na viranja wa dunia kama US, EU, Scandinavian Countries na UK.

Hili Jambo linaweza kutupeleka pabaya Sana watanzania. Kwa sababu hizo nchi zina historia ya kutoa misaada kwa Tanzania, tusijidanganye kabisa, Tanzania hatupo self sufficient.

Nnachohisi ni kwamba huko mbeleni, miezi michache ijayo kwa hali inavokwenda, Tanzania dizani itasusiwa na hao mabepari. Na hii moja kwa moja itaenda kuathiri mapato ambayo serikali imepanga kuyapata kutokana na mikopo na misaada.

Tukifikia hapo inaonekana kuna dalili utekelezaji wa hii bajeti utakuwa dhaifu kwa sababu bajeti haiwezi kutekelezwa bila pesa. Na ki ukweli kabisa serikali ya Magufuli ina crisis ya Cashflow. Cashflow ipo tight Sana hatuwezi ku survive bila misaada ya Mabepari wa nje.

Nadhani Jana prof mpango alisema Meno kwamba Tanzania ipo kwenye vita vya kiuchumi, utakuwa kuna action zimeshaanza kuonekana

Na haya ndio mojawapo ya madhara makubwa ya kudorora kwa mazingira ya demokrasia nchini.

Inawezekana kuna mengi Sana yanakuja. Huu uchaguzi wa mwaka huu ndio turning point ya kubadilisha mwenendo wa nchi yetu.
 
Well said mkuu, kwa dalili za kiburi na majigambo plan za ccm rejea kauli zao Bungeni na nje ni kutokuwa na uchaguzi huru na haki. Hali itakuwa ngumu sana ukizingatia miradi mingi mikubwa ipo ngazi ya msingi bado kumalizia,Maji,umeme,afya,madaraja nk.Mfani mdogo garama xray moja yaweza fikia garama majengo kituo cha afya. Ccm bado mna muda JPM anaweza kushinda kihalali kidemocrasia, ila mnachopanga sifa za kijinga eti kupita bila kupigwa kwa mbinu !? Tutajuta pamoja.
 
Kwani hatujui impact yake,Tatizo Magufuli anachezea pabaya.

Ananikumbusha Enzi za President Reagan,Prime Minister Margaret Thatcher Vis President Nyerere.
Hao unaowakejeli leo,kesho wakiamua kwa pammoja hatuwezi kutoboa hata kidogo.

Sasa hivi bado wana haya machoni lakini siku wakiamua hapatoshi.Huo mchezo umemshinda Russia ya Putin ,Venezuela ya Maduro.
 
Pole mkuu, hakuna nyongeza hapo, hicho ni kiwango cha kukata kodi. Bajeti iliyopita mtu mwenye basic ya 170 alikuwa hakatwi ila kwa sasa mtu ambae ana basic ya 270 hatakatwa kodi.

Maana yake ni kwamba basic ziko palepale isipokuwa tu wenye punguzo ni wale wenye basic kuanzia 170-270 kwa maana kuwa aliyekuwa na basic ya kuanzia 171-270 alikuwa analipa kodi ila kwa sasa mtu yuleyule mwenye hiyo basic hatakatwa kodi

Upo hapo!?.
 
Well said mkuu, kwa dalili za kiburi na majigambo plan za ccm rejea kauli zao Bungeni na nje ni kutokuwa na uchaguzi huru na haki. Hali itakuwa ngumu sana ukizingatia miradi mingi mikubwa ipo ngazi ya msingi bado kumalizia,Maji,umeme,afya,madaraja nk.Mfani mdogo garama xray moja yaweza fikia garama majengo kituo cha afya. Ccm bado mna muda JPM anaweza kushinda kihalali kidemocrasia, ila mnachopanga sifa za kijinga eti kupita bila kupigwa kwa mbinu !? Tutajuta pamoja.
Ukiona walivotupania, yaani huu uchaguzi ukija na mengi lazima mababeru watushungulikie. Sasa CCM hizi njama zao za kuleta mambo kama ya serikali za mitaa, zitawatokea puani
 
Pole mkuu, hakuna nyongeza hapo, hicho ni kiwango cha kukata kodi. Bajeti iliyopita mtu mwenye basic ya 170 alikuwa hakatwi ila kwa sasa mtu ambae ana basic ya 270 hatakatwa kodi.

Maana yake ni kwamba basic ziko palepale isipokuwa tu wenye punguzo ni wale wenye basic kuanzia 170-270 kwa maana kuwa aliyekuwa na basic ya kuanzia 171-270 alikuwa analipa kodi ila kwa sasa mtu yuleyule mwenye hiyo basic hatakatwa kodi

Upo hapo!?.
Oooh salaale.. kumbe
 
Nilidhani una jipya kumbe yaleyale tu ya siku zote ambayo nyie vijana wa ufipa huwa mnayaongelea,endeleeni kuota hizo ndoto zenu.
 
What is the effect of political polarization to Economic development? we have western and Eastern pact if one disturb us we go for the other, we are non Aligned country
 
Back
Top Bottom