Bajeti ya harusi ya gharama ndogo

Bajeti ya harusi ya gharama ndogo

duh ww mchini nn....big up bnge la budget hyo
 
LIKUD.. sijui kama utapendelea ndoa za kiserikali?

they are less expensive..

mambo mengine mtamaliziana mnakojua ninyi..

Inawezekana pia kaka, hebu nielezee unafuu wa ndoa za kiserikali ulivyo. Asante sana
 
Inawezekana pia kaka, hebu nielezee unafuu wa ndoa za kiserikali ulivyo. Asante sana

ndoa za kiserikali nadhani zinafungiwa kwa mkuu wa wilaya.. mashahidi wasiopungua kumi ndio wanahitajika, muoaji na muolewaji wawepo.. baada ya hapo ni kusain documents hizo za ndoa halafu mwisho ni kuondoka na mkeo tayari mume na mke!

kuhusu tafrija ndogo, mtaamua ninyi sasa.. lakini ndoa ishafungwa..

nadhani sijakuudhi ndugu!
 
Kaka mimi nilishawahi kualikwa kwenye harusi ya Ki-Ghana, hawa jamaa wapo simple balaa.

Baada ya ndoa pale kanisani mnakusanyika nje ya kanisa, mnapewa bites na vinywaji halafu mnaachana.

Hakuna complications.

Aisee ngoja niku pm tuongee fresh. Hiyo nzuri sana.
 
ukiwa na milioni hamsini itakuwa vizuri sana na huku akiishi maisha ya kupanga
 
Natoa mchanganuo wa harusi tuliyofanya sisi. Ukumbu 600,000 unawekewa viti vya plastics na kupambiwa (750,000 unapata executive chairs) sisi tuliweka viti vya plastics (600,000) mapambo tulipamba simple standard kwa (600,000), usafiri wakwe tuliwapa hela 150,000 watafute usafiri wao wenyewe maharusi 300,000 wazazi 130,000, keki ndafu moja 200,000, Champaign 6 (72,000), MC na music 500,000, Picha 750,000, chakula cha watu 160 (ng'ombe mkubwa 560,00, kuku 20 kwa 100,000, kuchoma nyama kupika wali mweupe na pilau na ndizi za kuchemsha 780,000) vinywaji (1,934,00) jumla ilikua 6,800,000
 
KWENYE RED UNAWEZA PUNGUZA ZAIDI,KWA HII...
946230_405479172895736_2026173024_n.jpg
 
Habari za leo wana JF.

Mdogo wangu anatarajia kufunga ndoa mwaka huu mwezi wa sita mwishoni.

Mimi ndio kaka yake na mimi ndio msimamizi wake.

Ninataka nimsaidie aweze kufanya harusi kwa gharama ndogo kwa kadri iwezekanavyo.

Idadi ya watu watakao alikwa ni hamsini.

Ninataka gharama ya harusi iwe shilingi Milioni Tano.

Kwa walio na uzoefu na suala hili, mnadhani kwa bajeti hiyo hapo na kwa idadi hiyo ya watu, inaweza kufanyika sherehe ya harusi ambayo itapendeza?

Na je inaweza kutumika chini ya gharama hiyo hapo juu?

Ninaomba maoni na ushauri wenu please.

Njoo chemba mkuu nadhani nina ka uzoefu hapo ila nsingependa kumwaga mchele kwenye kuku wengi
 
For detail mnaweza mpata manager wa princess hall kwa number zifuatzo 0715 499195 na 0753 499195 Mr. Tajiri
 
Wakuu wekeni na mchanganuo wa kipindi hichi cha Magufuli maana hali mbaya.
 
1.Ukumbi=1,000,000

2.Mapambo=1,000,000

3.Vinywaji bia 3@=330,000

4.Chakula plate 12000=600,000

5.Mc & Music=600,000

6.Magari-
Wazazi pande zote mbili=300,000

7.Gari-Maharusi=400,000

8.Coaster(Waalikwa)=
150,000.

Daaah nlisahau hela ya keki, sasa tusiivuruge hela ya dharura; twende tuvunje pale kwenye gari ya Maharusi, chanja 200,000 hapo afu tuitupie kwenye cake, ibaki 200,000 Gari safi na simple

Jumla kuu=4,380,000
Balance=620,000(Dharura)
NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA.
Hii harusi haina picha na video?
 
Back
Top Bottom