Bajeti ya Elimu: Kinana hajui au anaongopa?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Elimu: Kinana hajui au anaongopa?!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyambala, Sep 12, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  In about 2 days Kinana anazungumza kwamba kama Chadema itatekeleza suala la elimu bure basi hiyo itakuwa sawa na 70% ya bajeti ya serikali as of now. Wakuu are we that poor? Au takwimu hizi zimechakachuliwa kama kawaida yao akina kinana, CCM and the apologists.

  Lets do a bit of a homework:

  Bajeti as of current ni 11 trillion Tshs. 70% ya hiyo ni kama 7.70trilioni Tshs. Ok tukija kwenye suala zima la uchangiaji wa elimu, I believe more than 90% ni kutoka elimu ya juu.

  Tunaambiwa kwamba tuna wanafunzi elimu ya juu about 100,000. Lakini I am sure wanaolipiwa na serikali kwa asilimia 100 hawafiki 50%. Let us assume all 100,000 wanalipiwa na serikali kama CHADEMA inavyosuggest. At about 3,500,000 average kama ada ya elimu ya juu kwa mwaka unapata Total of 350 billioni Tshs. Does this represent anything near 70% of the budget???????????

  350billion Tshs is just about some 5% of 7.7trillionTshs ok say 10% uki include na ada za vijana wa sekondari, hiyo 70 % inatokea wapi???????

  Na je Kinana anaamini vyanzo vya mapato vya serikali vitaendelea kuwa vilevile traditional yaani bia, sigara, soda, PAYE, VAT???????

  Nna wasiwasi na takwimu hizi za kinana, CHADEMA mnaweza kufuatilia hizo heasabu za CCM tuziasses kama hazikuchakachuliwa?????????????

  Nawasilisha!!!!
   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Masahihisho kidogo, 70% ya trillion 11, ni trillion 7.7.

  Unajua siku zote CCM huwa ni wakurupukaji. Kama unakumbuka hata JK alipohutubia wazee wa Dar mwezi Mei, alisema kwamba akipandisha kima cha chini, ni kwamba bajeti yote itaishia kulipa mishahara. Yule Mtaaluma wa Mzumbe University akakokotoa mahesabu na kumtoa nishai.

  Achaneni na hawa watu, walishalewa ufisadi.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Kaka usiumize kichwa.

  CCM ni chama cha vilaza.

  Hawaoni tabu kumbatiza mtu hadhi ya Dokta eti kwa sababu anasafiri sana nje ya nchi kuomba misaada........
  .........
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa hapa ni ww ambae nkilza aba, hivi unadhani PHd wanatoa CCM?

  kwa kweli sera za chadema ni za kwa ajili ya uchaguzi na hazitekelezeki, huwezi kusema elimu na afya bure kwa makusanyo tulionayo


  kwanza mngetuonesha mtakusanya vipi hayo makusanyo na mnyambue ba hio budget, viko wapi vianzio vya mapato vitavyotufikisha kwenye malengo hayo ?

  ukweli ni malengo ya kiuuchaguzi kwa mtu ambaye anababaisha
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  have u done ur homework mkuu????????
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  PhD za CCM zipo nyingi mkuu

  Nchimbi Emmanuel PhD

  Matayo David PhD

  Kamala D PhD

  Mary Nagu PhD

  Jakaya Mrisho Kikwete PhD

  Makongoro Mahanga PhD

  Makamba Yusuf PhD

  Lisiti ni ndefu rejea Makala ya Msema Kweli
   
 7. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mtu wa Pwani,

  Yani unadhihirisha jinsi ulivyo mvivu wa kufikiri...... Yani tukiacha kunywa bia hata posho CCM itakosa.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu thanks for your comment ngoja nabadilisha kwenye main post........
   
 9. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mtu wa Pwani unapenda kubisha sana, do you know that that our government spend a lot of money on political related issues that donot help normal Tanzanians? ask youself what is a logic behind the MP's salaries?do they produce to deserve that kind of payments?
   
 10. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ni bahati mbaya kwa watu kama Mtu wa Pwani(ila wa pwani bwana!!!!).

  Gross enrollment kwa higher education Tanzania ilikuwa 1% 2004 na sasa imepanda kidogo inakaribia 2% lakini maajabu wanafunzi tertiary institutions ndio wanakaribia 60,000, about 25% wakiwa Private Universities. Wakati huo huo Namibia, Botswana walikuwa na enrollment ya over 6%, Zimbabwe na matatizo yote walikuwa na 4% na ndugu zetu kenya 3%.

  2007 tulikuwa na wanafunzi 49,000 vyuoni (varsities and colleges), about 10,000 walikuwa wanasoma private colleges and universities. Loan Board walifadhili kwa kiwango cha Tshs 74.7bn/- ambayo ni kiduchu kwenye national budget. Wenzetu Malaysia wanatenga 23% ya national budget kwa elimu( na hii ni mwaka jana). Kama serikali ikitenga 12% ya 11tn/= tutakuwa na Tsh 1.32tn/= ambayo ni mara kadhaa ya pesa inayopangwa na serikali. Hivi haiwezekani, na hapa bado tunabaki na kiasi kingi cha kutosha kuhudumia afya? Kwa mahesabu ya Tshs 3.5m kwa mwanafunzi Chuo Kikuu tunaweza kusomesha wanafunzi 377,000, ambao hatutakuwa nao. Tukifanya mahesabu ya wanafunzi laki moja, na tunabakiwa na fedha ya kutosha kutoa elimu bure kwa kila mwanafunzi wa secondari na primary zaidi ya 970,000 kwa gharama ya Shs 1,000,000 kila mmoja! Je inatushinda?

  Bado hatujawashika hao wazungu kwenye miaraba ya madini, acha tu inawezekana! Kinana asilete zake hapa!
   
 11. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Here's one source of revenue.

  Hebu tuambie wewe (kama unayo) au mafisadi wote au wananchi wenye nyumba za kupanga wanalipia kodi kiasi gani hizo nyumba zao za biashara?

  Be creative my friend, don't just be a end-user.
   
 12. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 929
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Jambo zuri kwa Dr. Slaa ni kuwa kwa miaka 3 mfululizo, yeye na wenzake wa CUF bungeni, wamekuwa wanatoa altenative budget inayoonyesha wanavyoweza kupata na kutumia, lakini ndugu zangu wa CCM wanaziba masikio. Kwa hiyo, ni bangi kudai ahadi za Dr. Slaa kuhusu elimu ni kwa ajili ya uchaguzi.

  Worse still ni hii tabia ya CCM kukosea mahesabu kila wanapoulizwa data. Nilidhani baada ya Prof wa Mzumbe kumuumbua JK wangeacha, sasa Kinana amerudia jana.

  Imefikia mahali wataalam wetu walio maofisni wanalazimishwa kupeleka Dodoma bajeti za wizara ambazo hazikubalance kabisa na bunge la CCM linapitisha tu. Kama kuna mtu wa Wizara ya Miundombinu humu aseme wazi tutamlinda -bajeti yao ya mwaka huu imepitishwa ikiwa na deficit ya bilioni 30! Waziri alipoambiwa akasema, "Twende tu, tutajua mbele ya safari".
   
 13. Sakoyo

  Sakoyo Senior Member

  #13
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! nilimsikia jana huyo msomali nikashindwa kumUelewa japo mi' nimesoma hesabu za MSINGI, ZILE ZA KATI na PIA ZA JUU, basi nikahusianisha tu na zile takwimu za mwenyekiti wake kuwa wafanyakazi wakilipwa 315,000/= na wapo laki tatu na nusu, hela yote ya pato la nchi itakwenda kwenye mishahara!!!!
   
 14. Sakoyo

  Sakoyo Senior Member

  #14
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angalia sasa, sio PHd ni PhD. Halafu; Kenya wana-kipi zaidi yetu waTZ na wanatoa elimu bure toka chekechea, hujafanya utifiti, sasa kwa taarifa yako ukifuatilia taarifa za CAG zaidi ya asilimia 60% ya pato la taifa linatumika kuendesha serikali ya JK asilimia zilizobaki ndo zinakwenda kwenye shughuli za maendeleo zikiwemo, afya, elimu n.k. Therefore, we respond to you by saying "YES WE CAN"

   
 15. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asanteni kwa kutuwekea vitu wazi ! Kinana kilaza kaama mgonjwa wetu tu.
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Elimu na Afya bure, siyo sera za CHADEMA pekee, CUF wameenda mbali zaidi, wao walisema elimu ni bure kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu. CHADEMA wanasema wanasema mpaka kidato cha sita.

  Miaka 2 au 3 iliyopita Kambi ya Upinzani chini ya Hamad Rashid walishawahi kuainisha vyanzo vya mapato. Lakini kwa kuwa viongozi wa serikali ni wadau kwenye biashara hizo waligoma. Kuna vyanzo vingi sana vya mapato ambavyo hakuna mtu anakusanya mapato na hasa kwenye rasilimali za nchi au fees wameweka ndogo zaidi.

  Ukija kwenye ukusanyaji wa kodi kuna wafanya biashara wengi sana wanakwepa kodi na wengine wanasamehewa kodi. Gazeti la Raia Mwema liliandika kwa urefu sana kuhusu waarab fulani ambao wamekuwa ma-agent wa kukwepa kodi.

  Baada ya hilo sakata kuna vigogo walisimamishwa kazi ili wachunguzwe kuhusiana na sakata hilo. Lakini ukichunguza sana bado hata huo uchunguzi hauwezi kufanya lolote kwa kuwa serikali inawakingia kifua maana hao vigogo wa TRA wanaagizwa tu na vimemo. Mwisho wa siku hakuna mtu ataenda kumhoji Rais au Waziri wa fedha.

  Kuna potential kubwa sana ya kukusanya kodi lakini kwa sababu ya uongozi ambao una-mind vimilioni vya michango kwenye kampeni za CCM, ndio maana TRA wanashindwa kukusanya kodi ipasavyo na mwisho wa siku wafanyakazi wa TRA wanaamua na wao wajichukulie rushwa.

  Elimu bure na afya bure inawezekana sana ili mradi kodi ikusanywe ipasavyo na vyanzo vyote vya mapato ya ndani vitumike kukusanya mapato ya ndani. Pia ile 25% ya bajeti nzima inayopotea kwa ufisadi na wizi, inaweza ku-cover bajeti yote ya elimu na afya na nyingine zikasalia.
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Pole zenu ninyi mnaotaka kumfumbua macho Mtu wa Pwani...

  Niaminicho ni kwamba, kwa member active wa JF wa zaidi ya miaka 2 lazima atakuwa na uelewa mkubwa kwamba mapato ya serikali kwa asilimia kubwa sana yanapotelea mifukoni mwa wachache na si katika ujenzi wa Taifa letu. Uongozi ukiwa ni moja ya kikwazo kuhakikisha dosari hizi zinapungua. Lakini kama jinsi mnavyoona, hata mpige, mgaragaze, kuna Watanzania wenzetu hawapendi mabadiliko katika jamii au kumbadilisha kiongozi na wako radhi kuona uzembe unaendelea kwa kuwa tu kiongozi huyo ni dungu yao, anatoka kanda watokayo, ni kabila lao, ni dini yao, au ni chama walimo kulia!!
   
 18. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,648
  Trophy Points: 280
  By the way wanasema matumiza ya kawaida ya hii serekali 3/4 ya mapato ya kila mwezi.
   
 19. D

  Dawa ya Mjinga JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 382
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Wala Nyambala usitie shaka, hesabu hao Fisi Wenu (Nyie emu) hawazijui. Ikiwa gharama ya kusomesha watoto wote wa Tanzania ni TZS trillioni 7.7 wao wanafanyaje? Ukisoma bajeti ya serikali ya Fisi Wenu 2010 hadi 2011 wanaeleza kuwa "Elimu imetengewa shilingi 2,045.3 bilioni" sawa na trilioni 2.045. Ikiwa elimu inagharimu hizo trilioni 7.7 kama kilaza Kinana anavyotaka Watanzania wamuamini kabisa basi ili kufikia mahitaji kamili ya elimu ina maana kuwa Watanzania baada ya kuichangia serikali kwa kodi na ada mbalimbali, wanaichangia elimu tena kwa shilingi trilioni 5.7 (nusu nzima ya bajeti ya serikali ya mwaka 2010/11).
  Ukichukulia kuwa kuna wanafunzi milioni kumi kutoka chekechea hadi vyuo vikuu, basi kila mmoja kwa wastani anachangiwa shilingi 570,000/=. Hii ni ziada ya fedha zinazotolewa na serikali (trilioni 2.045). Huu ni uwongo uliokithiri. Tuna kila sababu ya kuukataa uwongo na uzandiki huu.
  Tujiulize tu kama kweli kila mwanafunzi kwa wastani Watanzania tunamchangia kiasi hicho cha fedha?
  Msingi wa hesabu zilizofanyika hapo ni kuwa mwaka huu wanafunzi wanaokadiriwa kufika laki tisa wamefanya mtihani wa darasa la saba. Huwa wanapungua wanapoenda sekondari na wanapungua zaidi vyuo vikuu (ambapo mwaka huu wanakwenda wanafunzi 35 alufu). Kwa hiyo utaona kuwa nimetumia wastani wa juu kwelikweli wa wanafunzi milioni kumi. Ukweli ni kuwa kuna wanafunzi pungufu ya hao.Ikiwa na maana kuwa ili kufikia hesabu batili za Kinana mchango kwa kila mwanafunzi unazidi hapo.
  Kama kweli Kinana ana hakika ya hesabu alizofanya atueleze ni vipi watanzania (wazazi/ walezi na watu wazima wenyewe) wanaweza kuwekeza trilioni 5.7 kwenye elimu na serikali yao itumie trilioni 2? Nini ilikuwa msingi wa hesabu zake huyu kilaza Kinana. Bila shaka baada ya kutoa elimu duni ya kuchakachua kwa miaka 49 wanaamini kuwa hakuna awezaye kuuona uwongo wao kama walivyofanya kwenye mishahara ya wafanyakazi kwa kuwaaminisha watu kuwa ukiongeza kima cha chini mara tatu basi mishahara ngazi zote inapanda mara tatu. Yaani hata wale washauri wa mkulu wao wanaonyaka US$ elfu kumi basi wataongeaewa mara tatu. Katika hali halisi haifanyiki hivyo. Kwa kawaida asilimia ya ongezeko inapungua kadri ngazi ya mshara inavyoongezeka.
  Kinana na wapinzani wote wa mfumo wa kutoa elimu bure wanapaswa kupuuzwa hasa baada ya wao wenyewe kusomeshwa bure (kwa kodi za wananchi).

  Swala lingine katika mjadala huu ni ukweli kuwa wazee wetu walitafuta uhuru kwa malengo ya kupambana na maadui watatu: Ujinga, maradhi na umasikini. Mwalimu wangu aliwahi kunieleza kuwa ukiwa na afya na elimu basi umepata silaha ya kupambana na adui umasikini. Hivi maana ya adui Kinana na vilaza wenzake wanaijua? Wakumbuke jinsi tulivyowachukulia makaburu enzi zile kama adui au nduli Idd Amini. Inabidi utumie nguvu zako zote unapopambana na adui kama kweli umepania kumshinda. Kutoa elimu na matibabu bila malipo kwa kila Mtanzania ni njia sahihi ya kuwatokomeza maadui ujinga na maradhi. Ni Watanzania wangapi ambao wanapoteza maisha yao kwa kushindwa kulipia matibabu katika nchi hii? Wangapi leo maisha yao yameharibika au yamekwama kwa kushindwa kulipa ada za kuendelea na masomo? Hata kwenye ngazi ya vyuo vikuu bado kuna watu wanashindwa kulipa sehemu ya ada ambayo hawapewi mkopo. Hivi hawa Fisi Wenu wako Tanzania kweli? Au ndio Watanzania waliopata maisha bora?
  Maana kuna mheshiwa mmoja mingoni mwao, aliwahi kuniambai kuwa unadai maisha bora kwa kila Mtanzania kwani wewe ni Mtanzania? Nikajidai kujibu ndiyo. Akauliza kama nina cheti cha kuzaliwa, nikamwambaia sina, akauliza kama nina pasi ya kusafiria, hapana, akauliza kama ninaisha maeneo yaliyopimwa, jibu langu la. Akanieleza kuwa mimi si miongoni mwa Watanzania ambao walilengwa na kauli ile. Nilishia kucheka, lakini meseji ilifika.
  Elimu na Matibabu bila malipo inawezekana. Anayetaka kupanga ikulu kwa miaka mitano ambaye hayo yamemshinda, ajitoe mapema!

  Dawa ya mjinga ni kuumia
   
 20. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa jina lake silipati vizuri ni KiNANA AU KIMAMA?:confused2:
   
Loading...