Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili ndiyo moja wapo la tatizo la waziri kuwa mbunge pia.
Waziri yeyote atataka afanye walau kitu cha maana jimboni mwake ili apate cha kusema wakati wa kuomba kura. Ila pia waziri ana takiwa kufanyia kazi watanzania wote. Sasa waziri achague nini, kupendelea jimbo lake ili apate kura au kuli tumikia taifa zima? Atasema bora kupendelea jimbo lake maana ndiyo wanaompa kura na si Tanzania nzima.
Hii system yetu mara nyingi inaleta conflict of interests na ndiyo chanzo cha matatizo yetu mengi.
Najuuuuuuuuuuta kuifahamu hii sirikali. Najuuuuta. Kuna mikoa TZ lami hawaijui Rukwa na Kigoma kwa uchache. Kuna wilaya ambazo kwa uchumi wake zapaswa kuunganishwa kwa lami lakini bado mavumbi tu lol. Aliyenacho kweli ataongezewa.
Kwa kweli inashangaza kufanya upendeleo wa wazi. Hebu tujaribu kufikiria hili, Bagamoyo kunatarajiwa pia kujengwa Bandari. Ni umbali usiozidi 6okms kutoka bandari ya Dar. Bandari ya Dar inashindwa kufanya kazi kwa ufanisi hadi JK anafunga safari za mara kwa mara bandarini hapo ili angalau mambo yaende. Bandari ya Tanga iliyo umbali usiozidi 300Kms kutoka Dar, hakuna msaada wowte wa kuifanya iwe mmbadala wa ile ya Dar. Itaingiaje akilini kuanzisha bandari mpya Bagamoyo wakati hizi mbili achilia ya Mtwara ziko hoi bin taabani. Au kwa kuwa Kawambwa na JK wanatoka huko! Kuna nini hasa kikubwa cha kukuza uchumi hapo Bagamoyo kushinda Korosho za Mtwara, Mahindi ya Ruvuma na Rukwa? Tusishangae kusikia hata upanuzi wa Uwanja wa Ndege Dar ukahamishiwa Bagamoyo.Ni kweli Mkuu Magufuri knows the answer,
Lakini kama ulisha wahi pita barabara ya Tabora kwenda Kigoma.. ambayo kimsingi ni muhimu sana kwani inauunga mkoa wa Kigoma kwa sehemu nyingine hivyo kuharakisha maendeleo yake,
[SIZE=3]I mean kama umepita huko hasa wakati wa mvua, leo hii ukaja ona mabilioni yanatengwa eti kutengeneza barabara kama ya msata and whatever.. haingii akilini kabisa! Huu ni uhuni na ubinafsi wa hali ya juu![/SIZE]
Na sidhani kwamba ni busara kuipendelea sehemu moja ya nchi wakazi wake wapate maisha mazuri ili hali wengine ni fukara wa kutupwa! Wakati kodi unazifata huko huko kwa mafukara hao bila huruma.
Kwa kweli inashangaza kufanya upendeleo wa wazi. Hebu tujaribu kufikiria hili, Bagamoyo kunatarajiwa pia kujengwa Bandari. Ni umbali usiozidi 6okms kutoka bandari ya Dar. Bandari ya Dar inashindwa kufanya kazi kwa ufanisi hadi JK anafunga safari za mara kwa mara bandarini hapo ili angalau mambo yaende. Bandari ya Tanga iliyo umbali usiozidi 300Kms kutoka Dar, hakuna msaada wowte wa kuifanya iwe mmbadala wa ile ya Dar. Itaingiaje akilini kuanzisha bandari mpya Bagamoyo wakati hizi mbili achilia ya Mtwara ziko hoi bin taabani. Au kwa kuwa Kawambwa na JK wanatoka huko! Kuna nini hasa kikubwa cha kukuza uchumi hapo Bagamoyo kushinda Korosho za Mtwara, Mahindi ya Ruvuma na Rukwa? Tusishangae kusikia hata upanuzi wa Uwanja wa Ndege Dar ukahamishiwa Bagamoyo.[/QUOTE]
Mkuu kwani hiyo hujaisikia? Hiyo iko mbioni na tulisha ijadili sana humu..., na si hiyo tu nasikia pia wanaweka EPZ ile tu km chache kabla ya kufika Bagamoyo mjini, na kwa taarifa yako, wale wazee wa bagamoyo wameelezwa ardhi yao wasiuze, sasa viwanja havikamatiki, kuna kitu wanaita kieneo, hawaoni haya kukutajia mil 5, kwani wameambiwa mji wahamia huko, Bandari, uwanja wa ndege, EPZ Mungu awape nini??
Cjui masikini kule kwetu madongo kuinama nani aweza kuwa presidaa nasi tukakumbukwa katika ufalme wa Tanzania?
Nimeshangazwa sana na hili, cjui Nyerere naye angeamua kila kitu Butiama ingekuwaje?
hii ni kweli kabisa, huwezi kufikiria majimbo mengine na wapiga kura wako hujawaridhisha.
Lakini hata hivyo barabara kama ndiyo hiyo inayoongelewa (lushoto-kilosa-Mikumi) bado ni ya muhimu kwa maendeleo
ndio maana kuna umuhimu wa kuwa na utaratibu wa kuteua mawaziri nje ya bunge. mbunge anapokuwa waziri, anakosa ule uhuru wa kuisimamia serikalikwa sababu na yeye anakuwa sehemu ya serikali anayotakiwa kuisimamia.
Kama kawa TBL TCC cocacola na viwanda vya spirits jiandaeni na bonge la kodi. Ila mjua hata mpandishe Kodi vipi Bia hatuachi. Kuna maeneo mengi sana y akupata mapato ila serikali haiko creative. Hivi nchi hii kuna TUME YA MIPANGO?
Mi iwa wananiudhi hawa mawaziri wa Fedha kupandisha kodi ya vinywaji sasa sijui mnataka kutukomoa au inakuwaje?Mbona madini kule hampandishi kodi na watu wachache wananeemeka kupitia migodi. Jaribuni kuwa wabunifu nyie mawaziri wa Fedha sio vinywaji tu ndo mnako patia kodi.