Bajeti ya 2009/2010 Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nsaji Mpoki, Apr 17, 2009.

 1. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni kipindi cha maandalizi ya kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2009/2010. Pilika pilika zimeanza ambapo Wizara na Mikoa zitatakiwa kupeleka makisio yao kwa ajili ya mapitio kabla Kamati za Bunge hazijakaa na kupitia na kisha Bw. Fedha wa Taifa Mustafa Nkullo atawasilisha kwenye Bunge la Juni. Huo ni mchakato ambao huanzia kwa Wizara na Mikoa kupewa ceilings za fedha kwa matumizi ya kawaida (Other charges) na fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo (development fund). Kwa maka ujao wa fedha kila Wizara, Idara ya Serikali, Mikoa na Halmashauri imetakiwa kupunguza bajeti kwa asilimia 20 kwa maelezo kuwa hali ya uchumi kidunia si nzuri. Tuache hayo; nina hoja mbili za msingi kuhusu bajeti hii; Moja; ni kama Waziri Mkuu anakumbuka kama kipindi hiki ni cha bajeti na anatakiwa kuhakikisha kuwa bajeti hizi zinalenga katika kutatua matatizo ya wananchi vijijini na si kutenga fedha za mikutano, safari holela na kongamnao. Wote mtakumbuka jinsi alivyokuwa mkali mwishoni mwa mwaka jana kuhusu namna fedha zinavyopotea kwenye matumizi yasiyo na msingi. Wakati ni huu hana haja ya kusubiri kufanya 're-allocation' mwezi desemba, 09 au kutafuta kisingizio cha kutojua nini Wizara zimefanya. Hadi sasa hatujaona kama kuna serious thinking kuhusu hili.

  Hoja ya pili kubwa inayonisukuma kuandika ni namna tunavyoendelea kugawana resources kupitia bajeti ya seriakali. Wote mnafahamu kuwa serikali inaendelea kupeleka shughuli/huduma kwenye ngazi za chini (D by D). Mfano inaimarisha elimu (ya msingi na sekondari) katika ngazi ya kijiji na kata. Kuna kundi kubwa la walimu wa sekondari ambao sasa wanapangiwa kufanya kazi kwenye sekondari za kata maarufu kama St. Kata. Tumeanza pia kujenga vituo vya afya kila kata na zahanati kila kijiji. Watumishi na huduma hizi zote zinatakiwa kusimamiwa na Sekretarieti za Mikoa zikishirikiana na Halmashauri za Wilaya. Hii ina maana kwamba kunatakiwa resources zaidi kwenye ngazi hiyo ya Mkoa na Halmashauri. Lakini ukiangalia Ceilings za bajeti ambazo Mikoa na Halmashauri imepewa unaweza kulia. Bado tumeendelea na traditional thinking ya kujaza fedha wizarani. karibu asilimia 80 ya fedha zote za uendeshaji imeachwa kwenye wizara na mikoa na Halmashauri imepewa asilimia 20 tu. Kwa hali ilivyo sasa na kwa kuzingatia ukumbwa wa mahitaji ya wananchi vijijini ilipaswa Wizara zibakie na asilimia 10 ya fedha zote zinazotengwa na asilimia inayosalia iende waliko wananchi, yaani vijijini. Kwa kufanya hivyo tungechochea kile 'wenzetu' wanachokiita kazi ziko kwenye kilimo. Ingawa hatuna hata kiwanda kimoja cha kuzalisha majembe ya mkono. UFI ilizikwa zamani.

  Nimeona tuanzishe mjadala huu mapema kuwakumbusha viongozi wetu wa siasa hasa wabunge waaanze sasa kuingilia kati na si kusubiri kupiga mayowe mwezi juni. Kinachofanyika wakati uke wa bunge la bajeti kwa tunaofahamu mchakato wenyewe huwa ni usanii. Waheshimiwa wanatoa machozi ya kujisafisha kwa kushindwa kwao kujua ni wapi na wakati gani walipaswa kupiga kelele. Miongozo ya bajeti imetolewa kwenye kila wizara na kila Mkoa waitafute sasa ili wakabiliane na Waziri wa Fedha vizuri. Vinginevyo haya matatizo ya madai ya watumishi, nchi kukumbwa na njaa kila leo na umaskini uliokithiri hautatokomea.

  Mwisho, inasaidia nini kuendesha kulundika fedha wizarani wakati Maafisa Tarafa, kata na Watendaji wa vijiji ambao ndio wahangaikaji wakuu kule kwenye grassroot wanatembea maili kwa maili kwa miguu au juu ya pikipiki wakipigwa mvua kuhamasisha maendeleo. Niliwahi kufika Ludewa na Makete Iringa. Na nilibahatika kutembelea tarafa ya Masasi iliyo kando ya ziwa nyasa na makao makuu yake ni Lupingu utawaonea huruma watumishi walioko kule. Kama si uzalendo wengi wangekwisha kimbia. Nilifika pia Kijombo kwenye tarafa ya Ukwama Makete. Milima na hali ya mvua kwa mwaka huwezi kumpa mtu pikipiki. Achilia mbali kule tunduru, Mpanda anakotoka PM, Kigoma na kwingineko. kama kweli akina Prof. Mwalyosi, Dr. Binilith Mahenge, Zitto kabwe, Anne Kilango mna uchungu wahini sasa.
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mod budget is among economic issues please could you move this thread to Economic Forum
   
 3. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Moderator: tafadhali hamishia kwenye economic matters kama ilivyoshauriwa. Pole kwa usumbufu na nawaomba radhi wasomaji kwani nilidhani mada hii ina political implications hasa kwakuwa tunaelekea kwenye Uchaguzi wa seriakali za mitaa na uchaguzi mkuu
   
 4. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Moderator: tafadhali hamishia kwenye economic matters kama ilivyoshauriwa. Pole kwa usumbufu na nawaomba radhi wasomaji kwani nilidhani mada hii ina political implications hasa kwakuwa tunaelekea kwenye Uchaguzi wa seriakali za mitaa na uchaguzi mkuu ndiyo kisa nikaiweka hapa.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Bila kutarajia, Anthon Diallo alitinga katika kamati ya fedha na Uchumi wakati Mkulo alipokuja kuwasilisha bajeti atakayoisoma wiki ijayo (Diallo si mjumbe wa kamati hii lakini mbunge yeyote anaruhusiwa kuhudhuria).

  Baada ya Mkulo kuwasilisha, wakati wa kuchangia ndipo Diallo alipohoji ni kwa nini fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya barabara zilizomo jimboni kwa Mkulo, Kawambwa (Bagamoyo) na kwa mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi (Abdallah Kigoda). Alihoji ni kwa nini barabara hizo, ambazo nyingine zina lami zimetengewa fedha nyingi wakati kuna barabara nyingine hazipitiki kabisa na aidha zimetengewa fedha kidogo au hazijatengewa fedha kabisa?

  Waliolalamikia hali kama hiyo ni pamoja na Sitaju kaboyonga na Sadiq Murrad.

  Mwisho, Diallo alimuonya Mkullo kuwa iwapo hiyo ndiyo bajeti atakayoipeleka Bungeni wiki ijayo basi serikali ijiandae kwa uchaguzi mkuu mapema kabla ya wakati wake kwa sababu itakataliwa na bunge litavunjwa
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Right on!
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ha ha ha wanapo chezeana mchezo mchafu wenyewe kwa wenyewe wako shapu sana kukosoana lakini tanzania inapochezewa mchezo mchafu kupitia miakataba mibovu wanakaa kimyaaaaaaaa.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Cheche za bunge huru hizoooooo!!!!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kama mheshimiwa Diallo atafanya kweli itakuwa nzuri sana; iweje mawaziri wajipendelee kwao tu?

  Pia ni vizuri kama bunge litakuwa na makali ili hawa mawaziri wababaishaji wabanwe.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yangu macho mie
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tuliona pia wakati wa Mramba barabara za lami zikapelekwa Rombo kule Kilimanjaro!

  Je sasa ni wakati wa upendeleo Kilosa kwa Mkulo??

  Pia nimepita Chalize- shirika la nyumba limejenga nyumba ya gorofa kule tena porini kabisa kuelekea Moro: na hakuna hata mtu anaishi pale (White elephant!). Sii utumiaji mbaya wa pesa za Watz? Why Chalinze kule porini???

  Sasa kama kila mtu anavutia kwake- maeneo yasiyo na mawaziri itakuwaje?

  Hatuwezi kuiga hata kidogo msimamo wa mwal. Nyerere kutopendelea Musoma?
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Basi tuangalie ramani ya Tanzania. Kuna Barabara ya lami inayotaka kujengwa kutoka Handeni kupitia Kilosa, Mikumi, mpaka Iringa. Barabara hiyo inapita jimboni kwa Mkullo, lakini inapita majimbo mengi. Lakini vile vile sehemu ya barabara muhimu kwa sababu itarahisisha usafiri.

  Barabara kubwa iliyopo Bagamoyo ni ya kutoka DSM kwenda Morogoro na Arusha. Hii barabara ni kiungo muhimu kwa taifa. Kwa barabara hii pesa nyingi ni lazima zitengwe tu. Kwanza ilitakiwa kuwa 4 lane.

  Diallo anatakiwa kutuonyesha ni barabara gani maana barabara zingine ni muhimu kwa taifa.

  Na kama kulivunja bunge, richmonduli was a perfect timing.
   
 13. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2009
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hawa mawziri wamezoea kujipigia cross kipindi cha mwisho karibu na uchaguzi. Na hata wakati huu utaona kodi zitaelekezwa kule kule kwenye BIA, soda wines na sigara as if hakuna other sources of revenue katika nchi. Hakuna usawa katika upelekaji wa maendeleo TZ. Diallo Keep it up
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wanasubiri mpaka uchaguzi unukie ndiyo wanatoa stunts zao.Kipindi hiki lala salama hata kama uko sincere unatupa question mark tu, ulikuwa wapi miaka yote hiyo?
   
 15. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Diallo keshakuwa hero sasa, Diallo nae anasafishika. Hiyo bajeti itapita kama inalia ain't jack is gon break up.

  Tanzanians are the easiest people to fool. Diallo? Hivi kesha rudi kwenye biashara kama alivyo ahidi?
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hili ndiyo moja wapo la tatizo la waziri kuwa mbunge pia.

  Waziri yeyote atataka afanye walau kitu cha maana jimboni mwake ili apate cha kusema wakati wa kuomba kura. Ila pia waziri ana takiwa kufanyia kazi watanzania wote. Sasa waziri achague nini, kupendelea jimbo lake ili apate kura au kuli tumikia taifa zima? Atasema bora kupendelea jimbo lake maana ndiyo wanaompa kura na si Tanzania nzima.

  Hii system yetu mara nyingi inaleta conflict of interests na ndiyo chanzo cha matatizo yetu mengi.
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wabunge waipania bajeti ya Waziri Mkulo waonya inaweza kuvunja bunge

  *Waikataa kabla ya kufikishwa bugeni, wengine walipuana kuhusu heshima ya Rais


  Na Ramadhan Semtawa

  BAJETI ya serikali kwa mwaka 2009/2010, imekaa vibaya na inaonyesha kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo, atakuwa na wakati mgumu wakati atakapoisoma bungeni Juni 11 kutokana na baadhi ya wabunge kutangaza dhahiri kutoa shilingi huku wakionya kuwa huenda hata bunge likavunjwa.

  Onyo la wabunge hao ambao wengi ni kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kusini, limekuja baada ya Mkulo kuwasilisha Sura au Mwelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2009/2010, mbele ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, ambayo inatarajiwa kuwa ya Sh9.5trilioni ikilinganishwa na Sh7.3 trilioni za mwaka 2008/09.

  Mwelekeo huo wa bajeti ya 2009/2010, unaonyesha serikali inatarajia kukusanya Sh9.5 trilioni ambazo kati ya hizo, Sh5.1 trilioni ni mapato ya ndani, Sh3.2 trilioni ni misaada na mikopo kutoka kwa wahisani na Sh1.2 trilioni, ni mapato mengine, huku matumizi ya kawaida yakitarajiwa kuwa Sh6.7 trilioni na maendeleo Sh2.8 trilioni.

  Wabunge kutoka kamati mbalimbali nje ya Fedha na Uchumi, pamoja na baadhi ambao ni wajumbe wa kamati hiyo, walianza kuchambua mwelekeo huo wa bajeti kwa kumlipua Mkulo mbele ya jopo la wataalamu kutoka wizara hiyo na idara zake, hasa katika kipengele cha ujenzi wa barabara.

  Walienda mbali zaidi kwa kusema kila waziri anajipendelea kwake, akiwemo waziri huyo wa fedha.

  Mbunge Anthony Diallo (CCM-Ilemela), ndiye aliyeweka msimamo akimtahadharisha Waziri Mkulo kwamba bajeti hiyo kama ilivyo katika mwelekeo, haitaweza kupita bungeni na kuonya kuwa inaweza kuandika historia kwa bunge kuvunjwa.

  "Nakwambia kama ndugu yangu, bajeti hii ikija kama ilivyo haitapita bungeni, Iam telling you my brother (nakwambia kaka yangu)... sikufichi, haipiti hii bajeti," alizungumza Diallo kwa msisitizo.

  Diallo alisema karibu Sh100 bilioni zimetengwa katika barabara zile zile, huku maeneo mengine ya nchi yakiwa hayana barabara za lami.

  Alisema haingii akilini kuona sehemu ya barabara ya lami kutoka Same hadi Korogwe inatengewa fungu la Sh44 bilioni.

  "Ukiangalia, karibu Sh100 bilioni ni barabara zile. Utakuta ni Morogoro, Dares Salaam na Iringa. Nasema kwa mara ya kwanza bunge linaweza kuvunjwa," alionya Diallo kabla ya kubeba mkoba wake na kuondoka.

  Naye mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni alionya bajeti hiyo inaweza kuigawa nchi kutokana na kuruhusu maendeleo makubwa katika baadhi ya maeneo huku mengine yakiwa na umasikini wa kutisha.

  Dk Chegeni alifafanua kwamba, kitendo cha kukarabati barabara ya lami kati ya Chalinze-Segera-Tanga, haina mantiki wakati kuna maeneo hayana kabisa miundombinu ya lami.

  Mbunge huyo wa moja ya majimbo ya kanda ya ziwa, alidiriki kusema: "Hata barabara ya Msata Bagamoyo haikupaswa kupewa kipaumbele zaidi kama kuna nyingine hazina lami. Labda kwa sababu anatoka Waziri wa Miundombinu (Dk Shukuru Kawambwa)."

  Dk Chegeni alihoji barabara hiyo kuzidi kutengewa fedha wakati tayari nyingi zilichukuliwa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

  Akitoa mfano kuhusu hoja yake ya mawaziri 'kujimegea bajeti', Dk Chegeni alidai kuwa hata Basil Mramba akiwa Waziri wa Miundombinu alihamisha mabilioni ya fedha ya ujenzi wa barabara ya Usagara- Geita na kuzipeleka Rombo, ambako aliweka viwango ya Sh900 milioni kwa kilomita moja, kitu alichosema: "Kwa wakati ule haikuwezekana ni fedha nyingi."

  Alisema pia haingii akilini kuona uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya, ukitengewa tena Sh15 bilioni wakati uliwahi kutengewa Sh 30 bilioni, kitu alichosema si sahihi kwani kuna uwanja wa ndege wa Mwanza unahitaji kukarabatiwa au kujengewa eneo jingine (Terminal).

  Mbunge wa Mvomero, Suleiman Saddiq (Mvomero-CCM), alitishia kwenda Ikulu kuonana na Rais Jakaya Kikwete kama barabara alizoahidiwa hazitakuwemo katika bajeti hiyo.

  Hata hivyo, hoja hizo zilipingwa na wabunge wawili ambao ni Dk Omari Mzeru (Morogoro Mjini-CCM) na Dk Abdallah Kigoda (Handeni-CCM), ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya fedha na uchumi.

  Dk Mzeru alifafanua kwamba hakuna mantiki watu kuhoji ujenzi wa barabara ya Msata-Bagamoyo wakati ndiko anatoka Rais Kikwete, ambaye anapaswa kupita katika barabara salama yenye lami.

  Kwa mujibu wa Dk Mzeru, hajaona duniani sehemu ambako wananchi hawathamini heshima ya rais wao na kuongeza kuwa eneo hilo ni la kiuchumi kwani litafungua utalii.

  Dk Kigoda alihoji mantiki ya wabunge wenzake kushambulia ujenzi wa barabara ya Chalinze- Segera- Tanga, wakati ujenzi wa barabara ya Mwanza ni wa muda mrefu.

  Hoja ya Dk Mzeru kuhusu heshima ya Dk Kikwete, ilipingwa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF), ambaye alisema jambo la msingi si kuangalia nani anatoka wapi, bali barabara zinapaswa kujengwa kwa kuangalia matokeo na faida kiuchumi.

  "Napenda kupingana na hoja ya Dk Mzeru kuhusu ujenzi wa barabara ya Msata-Bagamoyo. Asiseme kwa sababu anatoka Rais basi ijengwe, tuangalie Economic impact (umuhimu wake kiuchumi), sasa ikiwa hivi kwingine ambako Rais hatoki itakuaje," alihoji Rashid.

  Akifanya majumuisho ya hoja ya bajeti hiyo, ambayo inaonekana kurejesha kero zile zile za kodi, Mkulo alisema suala la ujenzi wa barabara hizo mbili unaweza kukwamishwa kwa chuki dhidi ya Dk Kawambwa.

  Alisema barabara ya Chalinze-Segerea inajengwa na Denmark ambayo ndiyo imetoa fedha na kuchagua miradi yao hivyo, si rahisi kwa serikali kuipanga vinginevyo wangekataa na kuondoa fedha zao.

  Akizungumzia bajeti yenyewe, Mkulo alisema mwaka 2009/2010, sera za mapato zinalenga kukusanya mapato ya ndani yasiyopungua Sh5.1trilioni sawa na asilimia 16.4 ya Pato la Taifa (GDP), ikilinganishwa na mapato ya asilimia 15.9 kwa mwaka 2008/09.

  Mkulo aliongeza kwamba pamoja na msukosuko wa kiuchumi wa dunia, serikali imeongeza nguvu katika kukusanya mapato ya ndani ya nchi.

  Mchanganuo huo unaonyesha, mapato ya mikopo na misaada ya nje (MDRI/MCA -T) ni Sh3.2 trilioni, mapato ya halmashauri (Sh132 b), mapato yatokanayo na mauzo ya hisa (Sh 15 b) na mikopo ya ndani (Sh1.2 trilioni).

  Akitaja mchanganuo wa bajeti hiyo kisekta kwa kujumuisha mishahara kwa mwaka 2009/2010, ambayo inaonyesha kupungua maeneo ya vipaumbele na kurejesha kodi, Mkulo alisema elimu itatengewa Sh1743.9 bilioni ikilinganishwa na Sh1,430.4 bilioni kwa mwaka 2008/09.

  Kuhusu upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima na wafugaji, sekta ya kilimo kwa ujumla imetengewa Sh666.9 bilioni ikilinganishwa na Sh513.0 bilioni za mwaka 2008/09, sawa na ongezeko la asilimia 30.

  Kwa upande wa miundombinu, Mkulo alisema kipaumbele kitakuwa ni kukamilisha miradi ya barabara inayoendelea, hivyo kwa ujumla imetengewa Sh1,096.6 bilioni ikilinganishwa na sh 973.3 bilioni za mwaka 2008/09, sawa na ongezeko la asilimia 12.7.

  Sekta ya Afya, alisema kipaumbele ni kuendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM), kuimarisha ubora na upatikanaji wa huduma za uzazi na mtoto na kuimarisha uwezo wa rasilimali watu katika ngazi zote.

  Kwa ujumla, Mkulo alisema sekta ya afya imetengewa Sh963.0 bilioni ikilinganishwa na Sh910.8 bilioni mwaka 2008/09, sawa na ongezeko la asilimia 5.7, huku huduma za maji umuhimu utawekwa katika kuboresha umwagiliaji na matumizi ya kawaida, ambayo mwelekeo unaonyesha itatengewa Sh347.3 bilioni ikilinganishwa na Sh231.6 bilioni za mwaka 2008/09.

  Katika nishati na madini, Mkulo alisema kwa ujumla sekta hiyo imetengewa Sh285.5 bilioni ikilinganishwa na Sh378.8, sawa na upungufu wa asilimia 24.6.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  You are right. These are all stunts & the start of campaigns. Lakini hizi question marks ni kwa both sides. Kwa nini Mkullo apendelee shuguli za maendeleo kwa jimbo lake kwa wakati huu(labda ana taka barabara zionekani wakati aki kampeni mwakani)? na kwa nini Diallo siku zote alikua kimya ni leo tu ndiyo ana jitokeza?
   
 19. M

  Maskini Mimi Member

  #19
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mwanafalsafa, hivi ndivyo wabunge wanavyofanya kazi, inapokaribia wakati wa kula huwa wanaamka na siku zote hawasemi. What good Diallo has done to the nation while he was a minister!!!!
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hilo muulize "mchapakazi" Magufuli
   
Loading...