Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Tumezoea kila mwaka wa fedha unapoanza bajeti ya serikali hutegemea mapato kwa kuongeza kodi kwenye vileo na sigara au vnywaji baridi. Je mwaka huu itakuwaje? Je misamaha ya kodi kwenye madini itaonolewa au kiini macho kitachezwa? Je mashirika ya dini yakiwekewa kodi shule na mahosipitali ya kidini tutayamudu kwa gharama mpya baada ya kuwekewa kodi? Nina hofu sana juu ya hili. Waan JF mnasemaje?
 
It is high time mashirika ya dini yalipe kodi!

Maaskofu wanaishi maisha ya kifahari na mashangingi ya nguvu kama mawaziri..ni kwa nini wasamehewe kodi!

Wote walipe kodi!

Hizo hospitali na shule wanaweza kuomba ruzuku ya serikali..ila kodi walipe!

Ya Kairasi mpeni Kaisari!!!
 
Kama kawa TBL TCC cocacola na viwanda vya spirits jiandaeni na bonge la kodi. Ila mjua hata mpandishe Kodi vipi Bia hatuachi. Kuna maeneo mengi sana y akupata mapato ila serikali haiko creative. Hivi nchi hii kuna TUME YA MIPANGO?
 
Hata hivyo, hoja hizo zilipingwa na wabunge wawili ambao ni Dk Omari Mzeru (Morogoro Mjini-CCM) na Dk Abdallah Kigoda (Handeni-CCM), ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya fedha na uchumi.

Dk Mzeru alifafanua kwamba hakuna mantiki watu kuhoji ujenzi wa barabara ya Msata-Bagamoyo wakati ndiko anatoka Rais Kikwete, ambaye anapaswa kupita katika barabara salama yenye lami.

Kwa mujibu wa Dk Mzeru, hajaona duniani sehemu ambako wananchi hawathamini heshima ya rais wao na kuongeza kuwa eneo hilo ni la kiuchumi kwani litafungua utalii.

.

Hivi huyu mzeru ni dr wa nini vile? Nyerere (japo jina hili linawatia baadhi ya watu kichefuchefu) mpaka anastaafu hakukuwa na barabara ya lami kwenda Butiama. Mkapa pamoja na ufisadi wake hakujenga barabara kuto Ntwara hadi kijijini kwake.
 
It is high time mashirika ya dini yalipe kodi!

Maaskofu wanaishi maisha ya kifahari na mashangingi ya nguvu kama mawaziri..ni kwa nini wasamehewe kodi!

Wote walipe kodi!

Hizo hospitali na shule wanaweza kuomba ruzuku ya serikali..ila kodi walipe!

Ya Kairasi mpeni Kaisari!!!
Mzalendohalisi,

Are you serious? Atakayeumia ni nani? Serikali itakusanya kodi ya kiasi gani kwa maaskofu? Na kama serikali imeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wachache wa vyuo vikuu wataweza kutoa ruzuku ya kutosha kuendesha mahospitali na mashule yanayoendeshwa na mashirika ya dini. Mashirika ya dini yatozwe kodi kwa kupeleka miradi ya maji vijijini? Fikiria tena!
 
Kweli kabisa, mashirika mengi ya dini ni ya kuwatajirisha watu tu. Watoe general tax exemption kwa ajili ya shule na hospitali.
 
Kama kawa TBL TCC cocacola na viwanda vya spirits jiandaeni na bonge la kodi. Ila mjua hata mpandishe Kodi vipi Bia hatuachi. Kuna maeneo mengi sana y akupata mapato ila serikali haiko creative. Hivi nchi hii kuna TUME YA MIPANGO?

Ipo.Ipo mazee.Kipindi hiki inaongozwa na RA na wenzake.....
 
Bajeti itazingatia zaidi uchaguzi mkuu ujao. Mengine yote ni baadaye.

Kulipisha mashirika ya kidini kodi ni kosa. Tusiharibu. Uwadai kodi kisha uwape ruzuku? Huo ni mpira usio na magoli.

Kuna Askofu na Askofu. Wako watu wengi wamejipachika cheo cha Askofu wenyewe. Hao wadai kodi. Lakini mtu aliyeteuliwa kwa namna zinazofahamika na kukubalika kuwa Askofu, apewe heshima yake. Kwa mfano, Askofu wa Kikatoliki ana fedha za Kanisa, sio fedha zake. Ni fedha anazotumia kusomesha watoto wako, na kukutibu unapougua. Utamdai kodi ya pato lipi? Utamwambia achukue baadhi ya fedha za kuwalipa waalimu wa Marian College akulipe kodi? Si utaonekana ni ngumbaru wa kutupwa?
 
Hili ndiyo moja wapo la tatizo la waziri kuwa mbunge pia. Waziri yoyte ata taka afanye walau kitu cha maana jimboni mwake ili apate cha kusema wakati wa kuomba kura.
ndio maana kuna umuhimu wa kuwa na utaratibu wa kuteua mawaziri nje ya bunge. mbunge anapokuwa waziri, anakosa ule uhuru wa kuisimamia serikalikwa sababu na yeye anakuwa sehemu ya serikali anayotakiwa kuisimamia.
 
Episode Finale subject to 2010, tutakomaaaaaaaaaaaaaaaaa na kujuta kuwapigia kura. Si unaona hata kodi ya majengo sasa TRA ili iweje jamani?
 
Na ifahamike kuwa ongezeko lolote la kodi anaeumia ni mlaji wa mwisho. Wewe na mimi. Hata mkisema Makanisani walipe kodi waumini ndio watazitoa. Mimi nadhani kuna haja ya kuangalia critically juu ya matumizi ya serikali kwa ujumla. Mpaka tuone mashangingi na safari zisizo za lazima na matibabu kwa wakuu zinapungua. Sera mpya (???) ya madini itekelezwe.
 
Bajeti itazingatia zaidi uchaguzi mkuu ujao. Mengine yote ni baadaye.

Kulipisha mashirika ya kidini kodi ni kosa. Tusiharibu. Uwadai kodi kisha uwape ruzuku? Huo ni mpira usio na magoli.

Kuna Askofu na Askofu. Wako watu wengi wamejipachika cheo cha Askofu wenyewe. Hao wadai kodi. Lakini mtu aliyeteuliwa kwa namna zinazofahamika na kukubalika kuwa Askofu, apewe heshima yake. Kwa mfano, Askofu wa Kikatoliki ana fedha za Kanisa, sio fedha zake. Ni fedha anazotumia kusomesha watoto wako, na kukutibu unapougua. Utamdai kodi ya pato lipi? Utamwambia achukue baadhi ya fedha za kuwalipa waalimu wa Marian College akulipe kodi? Si utaonekana ni ngumbaru wa kutupwa?

Wako wanaofanya biashara kibinafsi kama Kakobe, Geo Davy, Rwekatale et al Wako wanajishughulisha na jamii kwa ujumla eg KKT, RC, Pentekoste nk.

Wa kundi la pili ukiwatoza kodi utakuwa umeshemsha big time. Lakini ukimtoza Geodavy au Kakobe ni sawa maana wanakusanya fedha toka kwa waumini na wanazitumia wenyewe.
 
Mzalendohalisi,

Are you serious? Atakayeumia ni nani? Serikali itakusanya kodi ya kiasi gani kwa maaskofu? Na kama serikali imeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wachache wa vyuo vikuu wataweza kutoa ruzuku ya kutosha kuendesha mahospitali na mashule yanayoendeshwa na mashirika ya dini. Mashirika ya dini yatozwe kodi kwa kupeleka miradi ya maji vijijini? Fikiria tena!

Mtuwamungu,

Kimsingi ni jukumu la serikali kutoa huduma za afya na shule kwa wananchi wake..hili jukumu lisiachwe kwa dini!

Serikali ikusanye kodi kutoa hizi huduma: yes inawezekana..hizo shule/hospitali za dini waombe ruzuku!! Kimsingi hospitali zote za Mikoa/Wilaya ziwe mali ya serikali..dini may supliment huduma kama wanapenda! Jukumu la kimsingi ni la serikali!

Hiki kiwingu cha mashirika ya dini kutolipa kodi..eti wanatoa huduma bure..siafikiani nacho!!

Je wewe unaona maisha ya kifahari..maaskofu wa RC, Anglicana na Lutheran wanayoishi?? Umeona magari mashangingi wanayotumia?? Je ni kwa nini wasamehewe kodi?
 
Hilo muulize "mchapakazi" Magufuli

Ni kweli Mkuu Magufuri knows the answer,

Lakini kama ulisha wahi pita barabara ya Tabora kwenda Kigoma.. ambayo kimsingi ni muhimu sana kwani inauunga mkoa wa Kigoma kwa sehemu nyingine hivyo kuharakisha maendeleo yake,

I mean kama umepita huko hasa wakati wa mvua, leo hii ukaja ona mabilioni yanatengwa eti kutengeneza barabara kama ya msata and whatever.. haingii akilini kabisa! Huu ni uhuni na ubinafsi wa hali ya juu!

Na sidhani kwamba ni busara kuipendelea sehemu moja ya nchi wakazi wake wapate maisha mazuri ili hali wengine ni fukara wa kutupwa! Wakati kodi unazifata huko huko kwa mafukara hao bila huruma.
 
Basi tuangalie ramani ya Tanzania. Kuna Barabara ya lami inayotaka kujengwa kutoka Handeni kupitia Kilosa, Mikumi, mpaka Iringa. Barabara hiyo inapita jimboni kwa Mkullo, lakini inapita majimbo mengi. Lakini vile vile sehemu ya barabara muhimu kwa sababu itarahisisha usafiri.

Barabara kubwa iliyopo Bagamoyo ni ya kutoka DSM kwenda Morogoro na Arusha. Hii barabara ni kiungo muhimu kwa taifa. Kwa barabara hii pesa nyingi ni lazima zitengwe tu. Kwanza ilitakiwa kuwa 4 lane.

Diallo anatakiwa kutuonyesha ni barabara gani maana barabara zingine ni muhimu kwa taifa.

Na kama kulivunja bunge, richmonduli was a perfect timing.
I would say perfect reason. The right time is now. At least to the MPs
 
kuwa mbunge wa Tanzania ni lazima uwe na vision mbili

uwe na uwezo wa kuteuliwa kuwa waziri ili upeleke upendeeo wa maendeleo jimboni kwako

au uwe na uwezo wa kifedha aidha za ufisadi au madawa ya kulevya au kwa vyovyote vile utumie hayo mapesa kumwaga misaada kibao ili uendelee kuwa mbunge

KWA HIYO HAKUNA HAJA YA UBUNGE WA KUTUMIA AKILI NA VIPAJI KUHAMASISIHA WANANCHI KUJILETEA MAENDELEO ENDELEVU, HUU NDO UBUNGE WA TZ NA HAO NDO WABUNGE WETU
 
Ni kweli Mkuu Magufuri knows the answer,

Lakini kama ulisha wahi pita barabara ya Tabora kwenda Kigoma.. ambayo kimsingi ni muhimu sana kwani inauunga mkoa wa Kigoma kwa sehemu nyingine hivyo kuharakisha maendeleo yake,

I mean kama umepita huko hasa wakati wa mvua, leo hii ukaja ona mabilioni yanatengwa eti kutengeneza barabara kama ya msata and whatever.. haingii akilini kabisa! Huu ni uhuni na ubinafsi wa hali ya juu!

Na sidhani kwamba ni busara kuipendelea sehemu moja ya nchi wakazi wake wapate maisha mazuri ili hali wengine ni fukara wa kutupwa! Wakati kodi unazifata huko huko kwa mafukara hao bila huruma.

Kwa kuongezea tu, tena anaejengewa barabara wala halipi kodi (Rais).
 
Hadithi tu hizi...Dialo anatafutia mahali pa kuanzia ili wapiga kura wamkumbuke! Tangu lini tangu hili bunge la vyama vingi limeanza wamewahi kuelezana ukweli? Kutuzuga tu na kutafuta kujulikana!! Watasema weeeeeee! dk zote alizopewa atakuwa anaipinga bajeti na kutoa maoni yake namna ya kuiweka sawa... ikifika pale ambapo ndipo anatakiwa kuonyesha kwanini alichaguliwa kuwakilisha jimbo lake..."hata hivyo naunga mkono hoja"! Aaaaagh! Ndio hao hao! Sasa kaona Mkullo anapeleka kwake anakuja juu km zile za kwao zote zingepata mgao angemkumbusha? Mh. umeteleza...? Vipi kule madongo kuinama?
 
Kweli nyani haoni ... Dialo wakati akiwa waziri wa maliasili alichagua watu wake wa karibu kwenye bodi ya Tanapa watu wakawa kimya sasa kaona uchaguzi unanukia anabwabwaja kujipendelea watz muhimu kwani watu wa ilemela ndio watakaomchagua Mkulo akirudi kwao watamuuliza umetufanyia nini na hii ndio lalasalama kalakabaho Dialo hata wewe ungekuwa waziri tena wewe ungejipendelea kwa sana halohalo
 
Tuliona pia wakati wa Mramba barabara za lami zikapelekwa Rombo kule Kilimanjaro!

Je sasa ni wakati wa upendeleo Kilosa kwa Mkulo??

Pia nimepita Chalize- shirika la nyumba limejenga nyumba ya gorofa kule tena porini kabisa kuelekea Moro: na hakuna hata mtu anaishi pale (White elephant!). Sii utumiaji mbaya wa pesa za Watz? Why Chalinze kule porini???

Sasa kama kila mtu anavutia kwake- maeneo yasiyo na mawaziri itakuwaje?

Hatuwezi kuiga hata kidogo msimamo wa mwal. Nyerere kutopendelea Musoma?

Nyumba za chalinze wanaishi watu na zimekwisha pangishwa toka zamani hakuna hata nafasi.
 
Back
Top Bottom