Bajeti;je ni mimi sielewi au iko sawa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti;je ni mimi sielewi au iko sawa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, Jun 15, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  waungwana naombeni msaada ili na mimi niweze kutoa mchango wangu kwenye hii bajeti ya ccm.
  nijuavyo mimi serikali imeingia madarakani baa da ya kutuomba ridhaa mwaka 2010.maana yake hawa ni wafanyakazi wa watanzania na wanastahili mishahara baada ya kufanya kazi ya kusimamia na kulinda rasilimali za bosi wao,wanatakiwa wakusanye mapato yote yaliyopo kwenye himaya ya bi=osi wao wajilipe mishahara na kuwaletea maendeleo waajiri wao.

  sasa turudi kwenye kazi wamekuja na bajeti yao kwamba katika sh 15 ambazo watakusanya kwa wananchi(na si kwenye rasilimali) sh kumi wanakula wao tano ndizo za maendeleo.pamoja na hizo kuna misaada na madeni,madeni watakuja kulipa mabosiwao siku wakijakupata.

  kitu ambacho sikielewi ni hiki.
  kwa nini mfanyakazi anachukua 75% na tajiri abaki na 25%?
  kwa nini kwenye deni la taifa mfanyakazi asiendelee kuchukua 75%badala yake bosi analipa 100%?
  je unapoongeza mishahara na kuongeza kodi kwenye bidhaa si ni sawa na unamlipa mtu haki yake mchana na kwenda kumnyang'anya usiku?
  je unapotoza kodi kubwa kwenye bidhaa za kuingia badala ya kutoza za kutoa nje ya nchi huoni unaumiza watu wako?
  je kulikuwa na haja gani ya kuongeza mikoa na wilaya kama kiama kilikuwa kinaturudia?

  naombeni tujadili kama ni kunisaidia mnisaidie.
   
 2. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni wewe huelewi. Serikali sio mabosi wa wafanyakazi ila kinyume chake.
   
Loading...