Je, umewai kujiuliza kwanini hutosheki?

Je, umewai kujiuliza kwanini hutosheki?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
770
Reaction score
1,781
Simu: Mwaka jana, iPhone 16 ndiyo ilikuwa "ndoto" ya kila kijana. Leo, iPhone 17 imetoka na ile ya zamani inaonekana kama takataka.
Teknolojia: TV ya inchi 50 uliyonunua juzi, leo inaonekana ndogo kwa sababu kuna inchi 75 yenye "4K Ultra."
Mavazi: Nguo uliyopiga nayo picha mwezi uliopita, leo huwezi kuivaa kwa sababu "imeshachuja" machoni pa watu.
Huu ni mtego wa kisaikolojia. Huwezi kuishinda kampuni inayolipa mabilioni ya dola kwa wataalamu wa akili ili wakushawishi kuwa "Huna thamani mpaka ununue bidhaa mpya." Ni njaa ambayo haishibi, ni kiu inayozidi kadiri unavyokunywa.

Kafara ya Kisasa:
Katika hadithi za mtaani, watu wanasema Freemason wanachukua kafara za watu. Lakini kwenye uhalisia wa kiuchumi, kafara inayotolewa ni MUDA WAKO NA UHURU WAKO.
Ili uonekane wa kisasa:
Unachukua mishahara (Salary Advance) kununua simu.
Unachukua Mkopo wa Benki kununua gari la kifahari ambalo huwezi hata kulifanyia service.
Unajiingiza kwenye Madeni yasiyolipika ili tu uwaridhishe watu ambao hata hawakupendi.
Hii ndiyo kafara ya kweli: Unatoa miaka 30 ya uhai wako (kufanya kazi unayoichukia) ili kulipia bei ya vitu vinavyochakaa ndani ya miezi sita. Wewe si mmiliki wa hizo bidhaa; wewe ni mtumwa wa mfumo uliokupangia namna ya kutumia jasho lako. Yaani upo programmed tofauti yako na roboti ni pumzi tu.

Unapokimbizana na toleo jipya la simu au gari kwa kutumia mikopo, unatoa kafara ya miaka ya maisha yako kulipa riba (Interest) inayozidisha utajiri wao. Hawahitaji kukung'ang'ania; wanakupa tu "Pingu za Dhahabu" (Bidhaa za Anasa) ambazo unazivaa mwenyewe kwa hiari, huku ukibaki kuwa mtumwa wa madeni yao maisha yako yote.
Pia, mtego huu wa kutaka "Vitu Zaidi" unakuweka bize kiasi kwamba huna muda wa kuhoji nani anamiliki rasilimali za dunia. Unapokuwa na njaa ya iPhone 17, unakuwa mteja mtiifu badala ya kuwa mshindani kwenye meza ya maamuzi. Unapoteza utambulisho wako wa asili na kuanza kujitambulisha kwa "Brand" (Nembo) za makampuni yao. Hapo ndipo ushindi wao ulipo: wao wanajenga himaya za kudumu, huku wewe ukitumia jasho lako lote kununua takataka zinazochakaa ndani ya miezi sita.

Siri ya utajiri si kujiunga na "Chama cha Siri," bali ni kuwa na Nidhamu ya Siri. * Acha kushindana na teknolojia inayobadilika kila sekunde.
Tambua kuwa furaha haitoki kwenye duka la bidhaa (Mall), bali inatoka kwenye uhuru wa kutodaiwa.
Miliki mali (Assets) zinazokuingizia pesa, badala ya kumiliki bidhaa (Liabilities) zinazokula pesa yako.
Mtego umeshawekwa, na mlango uko wazi. Je, utaendelea kukimbiza kivuli cha iPhone mpya, au utachagua kuwa "Mjenzi" wa uhuru wako wa kweli?

Huwezi kuwa huru kama mfuko wako unatawaliwa na hamu ya "Kuhitaji Zaidi."
Je, unadhani ni kwanini tunajikuta tukinunua vitu tusivyohitaji hata kama tunaona kabisa madeni yanatuzidi koo?
 
Back
Top Bottom