Bajeti 2017/2018: Ukweli kuhusu kiasi kilichoongezwa kwa lita baada ya road licence kuondolewa

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,426
Nimeona mitandao ya kijamii inapotosha hasa kwenye ukurasa wa UKUTA.
Upotoshaji: Kuna ongezeko la shilingi 300 kwa kila lita. UKUTA

USAHIHI: Kuna ongezeko la shilingi 40 kwa kila lita soma kipande cha hotuba ya Waziri hapo chini.
Jiridhishe kwa kusoma Hotuba ya Waziri sehemu ya 69(ii)
Myatake: Tunapotosha ili iweje?

Screenshot_20170609-072902.png
 
View attachment 521534
Ukweli kuna unafuu mkubwa mfanio kwangu mimi natumia lita 60 kwa mwezi (TZA 120,000) ina maana road license ni TZS 40 x 60 x12 = 28,800 badala ya TZS 200,000. Hata hivyo napata shida kwani nililipia road license 29/5/2017 ambayo itaisha 28/5/2018 hivyo kwangu mimi imekula.

Kuna uwezekano vile vile wa magari mabovu yaliyopaki muda mrefu kurudi barabarani na hii itaongeza ajali za barabarani.
 
Hata kama ni upinzani, inafaa sana kama tutapinga vitu vya msingi vyenye tija. Kama kwenye bajeti imeandikwa kabisa Tsh 40 kwa lita, iweje mtu adanganye umma kwamba ushuru wa barabara ni Tsh 300?

Nilichoelewa mimi, awali katika kila lita moja, ushuru wa bidhaa (bila ushuru wa barabara) ulikua ni Tsh 339, kwa bajeti mpya, baada ya kuongeza ushuru wa barabara, ushuru mpya wa bidhaa utakua Tshs 379. Ikumbukwe hiyo Tsh379 ni jumla ya kodi zote sio barabara peke yake.

Tujaribu kuwa makini yunapotaka kupost jambo japo nakubali kama binadamu kuna kupitiwa, tukiweka ushabiki pembeni tunaweza kujadili mambo kwa tija.
 
Back
Top Bottom