BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Je, wakodishaji wa pikipiki kama taxi watavaa helmets ili kukinga vichwa vyao kama itatokea ajali?
Bunge limepitisha muswada wa Sheria ya Marekebisho katika Sheria mbalimbali wa mwaka 2008 ambao umegusa marekebisho ya sheria 11, ikiwamo ya leseni za usafirishaji ambayo sasa itatoa leseni za usafiri kwa pikipiki za bajaj na pikipiki za kawaida na hivyo kutambulika kisheria.
Akiwasilisha muswada huo ili usomwe kwa mara ya pili na ya tatu, jana bungeni Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, alisema pia sheria hiyo inakataza matumizi ya baiskeli katika maeneo ya mijini na kuruhusu zitumike vijijini chini ya usimamizi wa halmashauri za wilaya.
Hata hivyo, baadaye wakati akijibu hoja za wabunge, Mwanasheria Mkuu alikiri kuwa bado hakuna sheria katika halmashauri hizo, ambayo itasimamia baiskeli hizo na kuahidi kuwa katika marekebisho ya muswada huo, kifungu cha sheria hiyo nacho kitaongezwa.
Pamoja na sheria hiyo, pia alisema katika sheria ya vizazi na vifo, sasa itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kujiandikisha tangu anapozaliwa hadi kufa. Mwanyika pia alisema katika sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, sheria hiyo sasa imewaingiza madiwani wote wa kata ambao si wabunge kutibiwa kupitia Mfuko huo, pamoja na watumishi wa umma wastaafu kuendelea kutibiwa nao.
Kwa upande wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu muswada huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, George Lubeleje, alishauri katika sheria ya leseni na usafirishaji ni muhimu kuzingatia uwezekano wa baiskeli kutumika kama chombo cha usafirishaji wa kibiashara, kwa kuwa hutumiwa na wananchi wengi hasa vijijini.
Katika michango yao juu ya sheria hiyo, wabunge wengi walitaka katika marekebisho ya muswada huo uzingatie umuhimu wa kuruhusu baiskeli, nazo zitambulike kisheria kwa kuwa ndizo zinazotumiwa na wananchi wengi wanamudu kuzinunua kuliko pikipiki na bajaj.
Mjadala huo ambao ulichukua muda mrefu kutokana na malumbano hasa katika kipindi cha kupitisha vifungu, ulitokana na ukweli kuwa wabunge wengi walionyesha kutaka baiskeli nayo itambuliwe kisheria. Akiwasilisha hoja zake, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema itakuwa ni vyema iwapo baiskeli nazo zitatambuliwa kisheria, kwa kuwa watu wa kawaida kama wakulima, wafanyabiashara wadogo na wafugaji ndio wanaozitumia sana.
Nitashangaa kama Bunge hili litakataa kuunga mkono utolewaji wa leseni za baiskeli, kwani ukweli ni kwamba wabunge wote hapa tumepanda baiskeli, isitoshe itadhihirisha kuwa Bunge hili pia ni la watu wa kawaida, alisema Cheyo.
Aidha Cheyo, alisema katika Sheria ya Marekebisho ya Bima ya Afya, aliomba kifungu cha 27, kifanyiwe marekebisho ili madiwani watakaopewa huduma ya tiba kupitia Mfuko huo, wapate huduma hiyo hata pale watakapostaafu.
Naye Mbunge wa Magu, Festus Limbu (CCM), alisema waendesha baiskeli ni wajasiriamali ambao wanatafuta kipato chao kwa uhalali, hivyo kutopewa leseni ni uonevu na pia italeta matatizo makubwa hasa kwa vijana ambao wengi wanatumia baiskeli.
Nadhani baiskeli zitamkwe waziwazi kwenye sheria hii, kwani Bangladesh wanatumia baiskeli tena za miguu mitatu na ndizo zinatumika sana, iweje sisi tushindwe? Alihoji. Alitoa rai kuwa wenye baiskeli wasibughudhiwe na vyombo vya Dola kwani wanajitafutia malipo halali kwa kazi halali, hivyo wasajiliwe na halmashauri ziwatambue.
Naye Mbunge wa Nkasi, Ponsiano Nyami (CCM), alipongeza marekebisho ya sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, lakini pia alipendekeza uangaliwe na uwezekano wa kuwaingiza wabunge katika matibabu hayo. Pia alizungumzia suala la sheria ya uchawi, ambako alitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuhusu imani hizi za ushirikina, ambazo sasa zinazidi kwani tayari kuna tetesi kuwa pamoja na albino, pia watu wenye vipara, viganja vyenye alama ya M na akinamama wenye ndevu nao ni mali.
Bajaj, pikipiki ruksa kuwa teksi
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Thursday,January 29, 2009 @21:15