Baiskeli za swala.....ziliishia wapi?

Baiskeli za swala.....ziliishia wapi?

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,950
Reaction score
6,981
Miaka ya 1990s, TANZANIA ilikuwa inazalisha baiskeli ambazo zilinunuliwa sana na watanzania. baada ya mda zilipotea kwenye soko. mwenye kumbukumbu atujulishe yafuatayo.
1. Kiwanda chake kilikuwa wapi?
2. Kiwanda kilifisika vipi wakati walikuwa wanauza? baba yangu mdogo aliinunua baiskeli ya swala, nimeitumia, usukani wake ulikuwa bomba sana.
3. Mkurugenzi wa mwisho wa kiwanda kile ni nani na yuko wapi?
4. kiwanda kilifunguliwa mwaka gani na kilifungwa mwaka gani.

kwa wenye majibu ya kiwanda hiki watujuze sie tuliozaliwa 1980s na hawa kizazi cha mabadiliko ya kisiasa 1990s
 
Kiwanda cha National Bicycles Company NABICO) chini ya NDC kilikuwa hapa Mwenge, hii issue ukiambiwa utasikitika sana, waliuziwa wahindi nao wakaanza kuleta spare na Baiskeli za Avon wakaanza kuuza pale hatimaye wakaanza kuuza zile nyumba zoote zilizokuwa za kiwanda baadaye biashara ya Baiskeli ikaishia hapo na SWALA zikafika mwisho. Leo ni kiwanda cha madawa cha Shellys.
 
shukran sana mkuu kwa kutujuza kwa sie tuliokuwa hatuyafaham hayo.
 
mi nakumbuka Baiskeli ya watoto ya BMX kwan Dady alitununulia watoto wake wote 2lvyopokea Komunio ya Kwanza
 
Kiwanda cha National Bicycles Company NABICO) chini ya NDC kilikuwa hapa Mwenge, hii issue ukiambiwa utasikitika sana, waliuziwa wahindi nao wakaanza kuleta spare na Baiskeli za Avon wakaanza kuuza pale hatimaye wakaanza kuuza zile nyumba zoote zilizokuwa za kiwanda baadaye biashara ya Baiskeli ikaishia hapo na SWALA zikafika mwisho. Leo ni kiwanda cha madawa cha Shellys.

DUH, hawa wahindi kweli wameshiriki kutudidimiza. baiskeli za swala zilikuwa kiboko yao, inaonekana walihisi zitayumbisha soko la avon, bidhaa za luziana india. ndo wakaja na njama zao hadi kutufilisi kiasi hiki.

wakati yote yanatokea, nani alikuwa rais, waziri mkuu, waziri wa fedha na waziri wa viwanda nchini?

hawa watu ni mhimu kuwafahamu. naamini huyu FISADI WETU alikuwa waziri wa mambo ya nje, i mean ******
 
Mie nakumbuka baiskeli za CHANG SHAN.

Sie tulikuwa tunaziita shang shang, zilitoka shangai china. walikuwa wapinzani wa phonex, zote za china. laikin phonex zilikuwa imara zaidi, ndo maana hadi leo zipo madukanai.

baiskeli ni swala, baiskeli ni swalaa, baiskeli ni swalaaaaaaa. nakumbuka mbali sana.

kuna mzee alinunua baiskeli ya swla kijijini kwetu, akawa anaisifia kwa kilugha

anaimba..."tambula bhukebhuke swala wanje, tambula bhukebhuke swala wanje
 
Miaka ya 1990s, TANZANIA ilikuwa inazalisha baiskeli ambazo zilinunuliwa sana na watanzania. baada ya mda zilipotea kwenye soko. mwenye kumbukumbu atujulishe yafuatayo.
1. Kiwanda chake kilikuwa wapi?
2. Kiwanda kilifisika vipi wakati walikuwa wanauza? baba yangu mdogo aliinunua baiskeli ya swala, nimeitumia, usukani wake ulikuwa bomba sana.
3. Mkurugenzi wa mwisho wa kiwanda kile ni nani na yuko wapi?
4. kiwanda kilifunguliwa mwaka gani na kilifungwa mwaka gani.

kwa wenye majibu ya kiwanda hiki watujuze sie tuliozaliwa 1980s na hawa kizazi cha mabadiliko ya kisiasa 1990s

Hii ndiyo Tanzania ya kubinafsisha kisha KUFISHA!!! Baiskeli yenye jina SWALA ilipotea kwa style ileile ya KANGA za MWATEX; mikate ya SIHA na unga wa NMC....Nikitaja vichache vilivyokuwa vinazalishwa na viwanda vyetu hapa nchini.
 
..itakuwa mafisadi walishagawana mtaji mapemaaa

tuwatafute tuwajue, waliotuingiza katika shida hii ambpo kila kitu sasa tunaigiza toka china na nchi nyingine.

sisi huwa hatuthamini vya kwetu, kazi zetu kudharau wanavyofanya waza. UDSM miaka fulani, kuna njemba ilikuwa inasoma coet, katika kufanya utafiti wake, akaibuka na teknolojia rahisi ya kukusanya samaki ili uwavue kwa urahisi. aliomba chuo na serikali wamfadhili ili aweze kutengeneza mashine hizo, ikiwezekana zianze kuuzwa kwa watanzania, hakusikilizwa mpaka alipochukuliwa na wajerumani. mpaka leo, hajawi kurudi.

kuna madogo wanauwezo wa kutengeneza vituo vya kurusha matangazo ya masafa mafupi kupitia FM, wanachokifanya ni kuwakamata na kuwafungulia mashitaka kurusha matangazo bila vibali. kwa nini wasiendelezwe?

kuna njemba zina viwanda vya kutengenza bunduki, wakikamatwa tu, jela wanasota, kwa nini wasiendelezwe tuanze kufikiria kutengeneza zana za kivita tukia nchini kwetu?

CCM wananikera sana, kwa kuwa hawana uzalendo
 
Hii ndiyo Tanzania ya kubinafsisha kisha KUFISHA!!! Baiskeli yenye jina SWALA ilipotea kwa style ileile ya KANGA za MWATEX; mikate ya SIHA na unga wa NMC....Nikitaja vichache vilivyokuwa vinazalishwa na viwanda vyetu hapa nchini.

Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Kingunge, ni maadui wa tanzani
 
Phoenix ilikuwa na mwamba mmoja na Swala zilikuwa na myamba miwili.
I mean kwenye Top chassis
 
Back
Top Bottom