Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,931
- 31,175
Rais wa kwanza wa nchi ya Ivory Coast Marehemu Felix Houphouet Boigny aliufanya mji aliozaliwa wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa ivory Coast badala ya Abidjani.Zoezi la kuufanya mji wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa Ivory Coast liliambata na matumizi makubwa ya fedha za nchi kuelekezwa Yamoussoukro kwaajili ya ujenzi wa miundombinu na maofisi ya wizara mbali mbali ambayo tayari ilikuwepo Abidjani.Uwanja wa ndege,mabarabara makubwa,mahospital na lile kanisa kubwa [ Basilica of our lady of peace of Yomoussokro] lilijengwa kwa gharama ya U$ 300 million peke yake.
Rais Jakaya M Kikwete tangu alipochaguliwa kuingia madarakani mwaka 2005 kumekuwa na juhudi kubwa sana za kuuendeleza Mji Bagamoyo kwa kutumia kodi za wananchi au kutumia mikopo au misaada.Kuna mpango wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa,kuna mpango wa kujenga bandari sijui kwanini tusijenge bandari kubwa Tanga au Lindi,kumekuwa na juhudi za chini chini za kujenga kituo cha mikutano cha kimataifa badala ya Arusha,Kumekuwa na juhudi za kujenga kijiji cha michezo badala ya ule mpango wa kukijenga sambamba na uwanja wa taifa Dar es salaam,ujenzi wa barabara nne kutokea Chalinze hadi Segera wakati barabara ipo tena tusisahau kuna sehemu nyingi Tanzania hazijawahi kuona barabara ya lami,ujenzi wa barabara msata hadi Bagamoyo.
Baba wa taifa Julius alikuwa Rais wa JMT kwa miaka 24 lakini hakuwahi kufikiria kuijenga Musoma / Butihama kwa kutumia rasilimali chache za nchi kama anavyofanya Muungwana katika kipindi kisichozidi miaka 4 tu.Najaribu kutafakari tukimpa tena miaka 5 mingine Bagamoyo itakuwaje ?.