Uchaguzi 2020 Bagamoyo msirudie mlichokifanya kwa CHADEMA leo

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,200
27,244
Habari wanajf, kuna suala ambalo sio la kawaida limejitokeza siku ya leo pasipo kutegemea.

Na kama ilivyo kawaida kwa kamanda mimi huwa sifumbi wala sifichi matatizo, nayamwaga ili kuwepo kujirekebisha kwa wahusika.

Siku ya leo ilikuwa siku ya kampeni ya mgombea wetu wa chadema katika mji wa bagamoyo.

Kama kawaida matangazo ya hapa na pale yalipita karibu sehemu nyingi kuwakumbusha watu juu ya kuhudhuria shughuli hiyo na ratiba ilionyesha mgombea wetu wa chadema angeanza kampeni pale muda wa saa 4 hadi saa 5.

Cha kushangaza ni kuwa hadi kufikia muda wa saa 3 asubuhi hakukuwa na mtu yoyote eneo la tukio, tukavuta subra kufika hadi saa 4 napo bado, kufika saa 5 napo bado.

Wakatokea baadhi tu ya viongozi wa CHADEMA wilaya ya Bagamoyo, nadhani lengo ni kuangalia muitikio kama kuna watu ili mgombea wetu aje amwage sera zake.

Lakini pengine kutokana na nature ya eneo la Bagamoyo watu wake pengine bado hawana muamko na upinzani, basi hadi sasa hivi saa saba hii inaenda saa nane mchana HAKUNA WATU KABISA.

Hali iliyopelekea mgombea wetu kutoonekana hapa viwanjani na pengine anaweza kuhairisha hili zoezi siku ya leo kutokana na kupuuzwa huko.

Niwaombe wananchi wa bagamoyo wasirudie tena walichokifanya leo kwa mgombea wetu na chadema kwa ujumla.

IMG_20200910_130606.jpg
 
Huwa nawashangaa sana wanasiasa, unawakusanya Watu muda wa kazi kwasababu zipi hasa.
Kwanini wanasiasa wasiambiwe muda wakukusanya watu uwe kuanzia saa 10? Kama unahoja mbona saa moja linatosha kuwaambia watu wakakuelewa.

Watanzania tuache uvivu na kupenda kukusanyika hovyo mida ya kazi tunajidhalilisha na wanasiasa wanatuona sisi tupo tu tunawasubiri wao muda wote waje kutupigisha stori.
 
Bagamoyo wanapaogopa sio utani

Uhuru wa Tanzania ulitokea pale mti wa uhuru bagamoyo na udongo ule ambao Nyerere na Karume waliuchanganya kuunda muungano wa sasa huu wa serikali mbili ambao udongo ulichukuliwa Zanzibar na Tanganyika udongo uliotumika kufunga huo muungano kwa Tanganyika ulichotwa bagamoyo ukasomewa dua nzito na wazee wa bagamoyo akapewa Nyerere akachanganye na ule wa Zanzibar uliosomewa madua na wazee wa Zanzibar

Mvunja muungano au mwenye nia ya kubomoa muungano huu wa serikali mbili kiboko yake iko bagamoyo hata Lowasa alikimbia kufanya kampeni na UKAWA wake bagamoyo anapajua alisepa
 
Longolongo la rumumba, yaani mnapata mawnge na kuweweseka kwa upepo tuu wa TL, subirini mafuriko yawapitie
Mkuu, nipo Bagamoyo eneo la Ukuni na ofsi zangu zipo magomeni karibu kabisa na viwanja vya shule ya msingi Majengo, anachoripoti jamaa ni kweli

Asubuhi wazee wa mji wanauliza Tu, Nani aende Kwa msaliti?

Hili swala la usaliti limekuzwa Sana na kuvuma mno na nadhani wengi wanasema sema tu bila hata kufahamu maana yake au dhana nzima ya huo usaliti

Watu hawajaenda kabisa, tofauti Kabisa na alipokuja Mama Samia
 
Back
Top Bottom