BAE Systems yakubali kuiuzia Tanzania rada mpya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAE Systems yakubali kuiuzia Tanzania rada mpya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tungaraza Jr, Aug 30, 2012.

 1. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI ya BAE System ya Uingereza, imekubali kuiuzia Tanzania kifaa kipya cha rada ya kuongozea ndege iliyoharibika hivi karibuni.

  Taarifa za kampuni hiyo kukubali kufanya biashara na Tanzania zimekuja baada ya kuwepo taarifa, kwamba kampuni hiyo haiko tayari kufanya biashara na Tanzania, ingawa ndiyo iliyoiuzia rada hiyo wakati wa awamu ya tatu ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa.

  Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mhandisi Fadhili Manongi, alisema kuwa Agosti 20 mwaka huu, alipokea barua kutoka Kampuni ya BAE ikiwaahidi kuwauzia kifaa kiitwacho Power Supply Unit, kilichokuwa kimeharibika.

  Alisema kifaa hicho ambacho ni kwa ajili ya rada hiyo ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, kinanunuliwa kwa gharama ya pauni 9,000 za Uingereza.

  Mhandisi Manongi alisema kutokana na barua hiyo kuwahakikishia kuuziwa kifaa hicho, tayari mipango ya manunuzi inaendelea ili kifaa hicho kiweze kununuliwa na kuletwa nchini haraka.

  "Kifaa cha rada kilichokuwa kimeharibika pale uwanja wa ndege tulikipeleka Afrika Kusini ambapo Kampuni ya Tellumat imeweza kukitengeneza kwa gharama ya Dola za Marekani 2,516 na kimerejeshwa nchini na kufungwa. Hivi sasa hali ya uongozaji ndege imerejea kama ilivyokuwa awali na tunaendelea kusubiri taratibu za ununuzi wa kifaa kipya kutoka Kampuni ya BAE, napenda kuwahakikishia Watanzania wote, kwamba anga ya Tanzania ni shwari. Unajua watu wengi hawafahamu rada yetu inaongoza ndege hadi nje ya nchi, rada hii inaongoza ndege za Burundi na Rwanda ambapo sasa ufanisi katika kazi umeongezeka na hakuna athari zilizojitokeza wakati kifaa hicho kikiwa kibovu," alisema.

  Manongi alisema Tanzania na Uingereza zina uhusiano mzuri, licha ya kuwapo mvutano wa urudishaji wa chenji ya rada hiyo baada ya kubainika taratibu na sheria hazikufuatwa katika ununuzi, hali iliyosababisha Serikali ya Uingereza kuitaka Tanzania kuwafikisha waliohusika mahakamani.

  Alisema kwamba, wakati kifaa hicho kilipokuwa kimeharibika, wafanyakazi wa TCAA walikuwa makini kuongoza na kuhakikisha abiria wanakuwa salama katika safari zao, ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi wa ndege mara kwa mara.

  Aliongeza kwamba kuharibika kwa kifaa hicho kumetoa somo kwa TCAA kujiandaa kuwa na akiba ya vifaa vya rada, ili kuwa na uhakika katika shughuli zao.

  Agosti 17, mwaka huu, Mhandisi Manongi alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari, kwamba kifaa cha Power Supply Unit cha rada iliyoko JNIA, kimeharibika na kwamba wakati huo ndege zilikuwa zinaongozwa kwa simu na redio.

  Rada hiyo ilinunuliwa kutoka Kampuni ya BAE kwa pauni za Uingereza milioni 29.5, sawa na Sh bilioni 70 za Tanzania. Hata hivyo ilibainika kwamba, mchakato uliotumika kuinunua haukuzingatia taratibu na sheria, kitendo kilichosababisha mvutano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni hiyo.


  Source: Gazeti la Mtanzania
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  "Mtu akikupa ushauri wa kupuuzi, na anafahamu kuwa unafahamu huo ni ushauri wa kipuuzi na wewe ukaukubali, basi atakudharau sama." - Nyerere
   
 3. i

  iseesa JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Je hizi paundi 9,000 ni pamoja na 10% kama ilivyo kawaida yao?
   
 4. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,481
  Trophy Points: 280
  sasa mbona umeandika rada badala ya kifaa cha rada...au wewe ni mwandishi wa udaku.?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Watu wengine jamani! Sasa kama hakukuwa na athari yoyote kifaa kilipokuwa kibovu kwanini mnataka kipya wakati mlichotengeneza kinafanya kazi?
   
 6. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  When the missionaries came to Africa they had the Bible and we had the land. They said "Let us pray." We closed our eyes. When we opened them we had the Bible and they had the land.
  Desmond Tutu
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  A very interesting quotation from a bishop
   
 8. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  This is wat is seen bro just know that LAND=RESOURCES
   
 9. Imany John

  Imany John Verified User

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,782
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  hahahaha Miss Tanzania, nakupenda ila hujatulia.
  BAE KAKUPA LIMBWATA GANI?
   
 10. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,546
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Duh! Hivi tukinunua psi mpya ya ziada sawa alafu kikaharibika kifaa kingine na kingine,je tutanunua navyo na ziada yake? Au radar yetu imeundwa na kitu kimoja tu yani(power supply unit)? Kama sivyo tunauhakika gani kitakachoharibika ni hichohicho? Kama ni tahadhari haiwezi kufanywa kwa kuwa na ziada ya kitu kimoja tu la sivyo tule nyasi kwa mara nyingine tena ili tununue radar ya ziada ili ikifail hii tunakua na nyingine! Lakini nyasi nazo siku adimu labda kama tutaweza kula mchanga ndo upo kwa wingi.
   
 11. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ya wapi cjui kaka.
   
 12. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Bei za hicho kifaa mbona inatatanisha! Kile cha SA ambacho tayari kimewekwa na kinafanya kazi kimegharimu dola 2,516, wakati hicho cha UK ni paundi 9,000. Je, hapa kuna chenji nyingine inaandaliwa?
   
 13. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dodo usipoteze muda wako kuandika mashairi humu, hapa ni deal juu ya deal. Hicho chenyewe cha paund 9,000 ni fix wanataka wakkukamue mpaka ile change waliyotema wairejeshe
   
 14. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Question, do we really need this new spare part?
   
 15. m

  markj JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  ukiona hivyo 10% haikupatikana kwenye yale matengenezo, watu wanaitaka hiyo kwa njia yoyote ile, ndo mana unaona yanakuja haya sasa. Na Bado watanunua hadi visivyonunulika sasa
   
 16. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  jamani nimesoma katika ripoti hiyo kuwa kifaa kilicho haribika "Kifaa cha rada kilichokuwa kimeharibika pale uwanja wa ndege tulikipeleka Afrika Kusini ambapo Kampuni ya Tellumat imeweza kukitengeneza kwa gharama ya Dola za Marekani 2,516 na kimerejeshwa nchini na kufungwa. Hivi sasa hali ya uongozaji ndege imerejea kama ilivyokuwa awali " sasa kwa nini tunataka kununua kingine kwa $ 9000 plus usafili ujumbe wa kukagua na mengineyo mengi . pia nahisi hata kipya kingekuwa bei nafu kuliko hii

  change ya rada tutairudisha yote !!!!!!
   
 17. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dah, hizi 20% zitaua watu mwaka huu!
   
 18. z

  zamlock JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Tena kwa ghalama ndogo 2516 usd alafu wanunue kingine kwa pound 9000 cha nn ? Ni pesa wanataka hao
   
Loading...