Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Ukiangalia mzani wa faida na hasara za kuiahirisha UKUTA utakuta faida ni nyingi zaidi ya hasara. Hakuna mshindi kwenye hili hata kama kuna watu watabeza sana. Nina imani kutakuwa na maelewano flani kabla ya 1st October
 
Wote hamjamuelewa nyani ngabu jamaa ameumia sanah kuahirishwa kwa hichi kitu... Ila nyani nadhan ni busara piah kuahirisha kwa faida ya wengine alafu inapokuwa viongozi wa dini wanaingilia kati si busara kupinga.. Me naamini bado hili swala laweza suruhisha bila kumwaga damu kwa faida ya sisi wote
 

Unaona sasa...hiyo ndo projection ninayoizungumzia.

Tatizo ulilonalo wewe unaliona kwa wenzio.

Wewe ndo hujanielewa halafu unajifanya umenielewa huku ukinyoosha kidole kwa wenzio kuwa wao ndo hawajaelewa!

Kazi ipo.
 
Umesahau na ile ya kulinda kura walivyowaacha watu hewani na kuna baadhi waliathirika sana na hilo.
Hii tabia ya ukigeugeu, ya kutosimia maamuzi thabiti....
Inawafanya watu kutosimama nawe kwani wanafahamu utawatosa dakika ya mwisho wakati washakiona cha moto na kuathirika.
Kesho ni nani atasimama nawe ukipiga la mgambo??

Lakini kitu kibaya ni kuwa inaua ule moyo wa kijasiri, moyo wa kizalendo wa watu kupigania haki na mustakabali wao. Kesho itakapotokea haja na nia thabiti ya kupambana kwa ari ya "nationalism" na "patriotism" watu watashindwa kuwaamini na kushikamana na viongozi wao na wataungana kwa kuchelewa wakati kila kitu kimeharibika (when it is too late).
Hii inatokana na upuuzi wa viongozi wasio na maono na weledi.

Hili sio tatizo la chadema tu, litakuwa tatizo la nchi nzima kwa tatizo la kama hapo juu.
 
Unaona sasa...hiyo ndo projection ninayoizungumzia.

Tatizo ulilonalo wewe unaliona kwa wenzio.

Wewe ndo hujanielewa halafu unajifanya umenielewa huku ukinyoosha kidole kwa wenzio kuwa wao ndo hawajaelewa!

Kazi ipo.
Mkuu binafsi nadhan nchi ikiingia kwenye machafuko yeyote ni doa kubwa sana.. Kuja kuiweka Sawa na hapo kugombana wenyewe kwa wenyewe Ndio Ugaid unapoanzia na tutayumba kwa uchumi nadhan bado kuna nafasi ya kumaliza kwa mazungumzo kwaajili ya usalama wa watanzania...
 
Mkuu wachache sana watakuelewa na wengi watakutukana japo ulichosema ni kweli tena kweli kabisa.
 
Baada ya tamko la CDM BBC kipindi cha jioni waliendesha mjadala kuhusu demokrasia katika nchi za kiafrika.Kwa hapa kwetu alishiriki Baregu na Mwigulu lakini pia walikuwepo wa Rwanda na Kenya.
Nirudi kwenye swali lako na jibu la moja kwa moja ni kuwa bado Chadema ina wafuasi.waziri Mwingulu amekariri kauli ya mkubwa wake ya kuwawabunge katika majimbo yao,madiwani na wenyeviti wanaruhusiwa kuendesha siasa.Pia alienda mbali kuwa wangewaza sana ikiwa watu wangetaka kuandamana kwa ajili ya kukosa dawa na mahitaji muhimu.Kwa ujumla alikuwa akijitahidi kuonyesha kuwa hakuna political threat lakini hakueleza maonyesho ya polisi ambayo hajawahi kutokea yalikuwa ya nini.
Kwa ujumla serikali bado haitaki kuweka wazi kinachogombewa na wapinzani na kwa mantiki hiyo ni suala la muda tu lakini litaibuka tena hasa ndani ya bunge.
 
Sasa usiwe na imani na chadema utakuwa na imani na chama gani sasa hapa TZ? Labda Yanga au simba xx.
 
Hebu tukumbushe malengo ya UKUTA halafu utuelezea ni kiasi gani yamefikiwa.
 
Kwan mkuu shida yako ww nin hebu tuache na chama chetu! Kama unatuhurumia ni vyema ukachangie damu sokoutoure
 
Ccm ndio imeangukia pua mgongoni mwa hao unaowaita vijana wa ngosha, tena nadhani wewe hukusoma hata elimu ya uraia maana ungejua yakuwa kwamba ngosha hana vijana bali vijana hao ni mali ya wananchi wa Tanzania yeye akimaliza miaka yake mitano ya hapo alipo atarudi kuwa mwananchi kama wengine.

Chadema wamethibitisha udume wao kwa kuwahenyesha hao vijana maana wamewabadirishia ratiba za kazi zao za kila siku lakini kuwapunguza vitambi vya tangia awamu zilizopita.
Katika hili nahisi hata ngosha kafurahi hasa ukizingatia yeye ni bingwa wa pushups hivyo kuwa na vijana wenye vitambi haiswihi.
Hili ccm hawawezi kuamrisha hawa vijana kubadiri ratiba hata kidogo!
 
Oktoba 1 zoezi la usafi litaendelea!
 
hahaaaaaaaaaaaaaaa si afadhali hakuna maandamano,watu watajikalia nyumbani,JE HAO MAPOLISI WALIOJIANDAA NA MITUTU,MABOMU huoni hao ndio wamefanywa makanya boya Zaidi hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa embu nicheke mie,nchi ina maigizo hii hakuna.

mie sina Imani na chadema.nina Imani na LOWASA peke yake,lol huyo baba angejitoa kwenye hilo kundi la chadema/ukawa,sio la hadhi yake,infact angeandaa chama chake mwenyewe kuelekea 2020,hivi sasa wanamtia madoa tu.

CHADEMA km upinzani umewashinda,its time to work na government na sio against,pale serikali inapokosea muikosoe ila ikifanya mazuri pia muipongeze,i think if you really want chadema iendelee,leteni solution ama alternatives za mambo mbali mbali yanayoikabili elimu,afya,usafi etc
 
WAPO ni kama wew ulivyo na imani na ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…