Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Naona una majeraha ya mtima.

Pole sana.

Ndo matokeo ya kuwekeza hisia kwenye watu wasio na uaminifu,.
Ninachokiona ni mwisho wa CDM. Chama kimeshakosa dira na hakina itikadi inayokisimamia, kwa ujumla nimekosa imani na CDM, tujiandae kwa anguko kuu katika uchaguzi wa 2020
 
Hivi bado kuna mtu bado ana imani na ccm baada ya miaka zaidi ya miaka 50?
Kama wapo basi wenye imani na Chadema pia wapo.
 
Hii ni nchi yenye dola iliyo tayari kujeruhi na kuua raia katika masuala ya kisiasa. Mifano ipo ya kutosha. Ningeshangaa sana kama CHADEMA wangeshikilia msimamo wa kuandamana kesho. Kuna mambo sikubaliani nao LAKINI, hadi sasa, naiona CHADEMA kuwa chama pekee Tanzania chenye watu wenye jeuri dhidi ya utawala wa mabavu wa serikali ya CCM.

Ni dhahiri kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kufikia bei ya watu kama Mbowe, Lissu, Mnyika, Lema, Mdee, Sugu, n.k. CHADEMA inajengwa na watu wasiolingana na "stereotype" ya Watanzania wengi; ya kunyenyekea watawala kupita kiasi kwa ajili ya maslahi binafsi. Inavyoonekana serikali na CCM wanatikiswa sana na harakati za CHADEMA kwani hawajui jinsi ya kuwadhibiti zaidi ya kulilia "tishio dhidi ya amani" na kuamrisha polisi na, sasa, jeshi kujiandaa kupiga/kuua yeyote anayeshiriki harakati za CHADEMA. Kwa mazingira tuliyo nayo, nje ya CHADEMA, tunao mbadala upi wa kuiweka sawa serikali angalau iwe na adabu kidogo?
 
Mimi nina imani na CHADEMA.
Nyani Ngabu tengeneza uzi mwingine wenye vitufe vya ku vote ili research yako iwe na Maana
Huu mtego waliowekewa Chadema wangeingia mkenge ndio ungekuwa mwisho wao.

Watanzania tunaongoza kwa unafki, Nyani Ngabu yupo Marekani anataka wenzake wauwawe yeye abaki tu kwenye keyboard.

Nina imani kikao cha msajili kitapata ufumbuzi na mikutano itaruhusiwa kwa vyama vyote.

Malengo ya Chadema kisiasa yamefikiwa hakuna haja ya kutowa sadaka maisha ya watu na kusababishia ulemavu.
 
TINGATINGA linatisha wewe...!!

Hatuwahukumu chadema kwa ulaghai wa UKUTA ...bali ulaghai wao juu ya kuupinga ufisadi ilihali wanampinga mpambanaji wa ufisadi!

Pia tunawahukumu kwa ukigeugeu wao ambao tumeshaushuhudia na tutaendelea kuushuhudia(Mungu atazidi kuwaumbua inshalah)
 
Hivi bado kuna mtu bado ana imani na ccm baada ya miaka zaidi ya miaka 50?
Kama wapo basi wenye imani na Chadema pia wapo.

Ndo maana wengine hatuna vyama na wala hatukuwashabikia Lowassa au Magufuli.
 
Halafu anatuita Mashabiki wa CHADEMA wa Mtandaoni wakati kaleta hoja mtandaoni sasa sijui alitaka ajibiwe kwa platform ipi zaidi ya kwenye mtandao
 

Uliniona wapi mimi nikichagiza watu waende wakaandamane?
 
 
Nimekusoma, una hoja lakini, ukumbuke kwamba, viongozi wengi wa chadema wamekamatwa, hayo maandamano yangefanyika vipi? Nadhani alichokosea mbowe ni kutaja tarehe nyingine, vile vile naona alitakiwa kuhairisha maandamano tangu aliposikia kuna zoezi la usafi, maana wananchi walihofu hapo kwenye usafi wa jeshi.
 

Tena tunaoiamini CHADEMA ndo tumeongezeka sasa. Tukutane 101.
 
Nakubaliana na wewe kuliko watu waumizwe na vyombo dola vya serikali dhalimu, bora kutafta suluhu am sure wengi hawaelewi yanayoendelea nyuma kuhusu amani ya nchi yetu kuandika na kulaumu ni rahisi, mno ila uhalisia hawaujui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…