Hukumsikia Mbowe au alikuwa anadanganya!Akina nani walikuJa kuwaomba UKUTA?
Nyani Ngabu umeongelea matukio mawili ambayo yamenifanya nisiamini uongozi wa Chadema. Nafuatilia siasa sana hasa za hapa kwetu lakini bado sijashawishika kuchukua kadi ya chama chochote. Chadema niliwashangaa sana mwaka jana, lakini sikuwanyima kura kwasababu ya CCM aliyokuwa ameiacha Jakaya. Lakini bado mambo ya ngosha yameanza kutia kinyaa nikadhani kama kweli Chadema wako madhubuti watamkomalia ngosha hadi aelewe nini maana ya demokrasia na vyama vingi. Hiki cha leo nimekiita kinyaa. Best solution wangezuia watu wasiandamane then wangeendelea na mikakati yao mengine. Leo wameprove kuwa ni waoga sana, hata kukamatwa tu kulala sero imewatia uwoga usio kifani. Mbowe aachie uongozi tu waje wenye maoni mapya.Hawa CHADEMA ndo basi tena.
Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.
Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.
Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.
Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.
Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.
Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?
Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.
Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.
Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?
Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.
Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.
Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Tuliona na imani na CHADEMA unataka tuamini chama gani na kwanini?
Wakati wewe ukionesha dole gumba?Nyie endeleeni kuzungusha mikono tu.
Anamuona Genius kwa Kuwa Amesema Yale Yampendezayo!Ni Kitu gani kinakufanya umuone kuwa ni one of the philosophers na ni well educated hapa JF kuliko watu wengine?
Huu sasa ni unaa na unafiki, we si kutwa nzima ulikuwa unakataza wasiandamane leo wasitisha umebadili gia unafiki mtupuWell said Ngosha,kusema ukweli watakaoendela kuwaamini CHADEMA basi wana hitilafu kwenye
Frontal lobe yao.Watu wazima Adrenaline zao zimepanda kwa mwezi mzima,leo mwishoni kabisa wanaambiwa their workdone is equal to zero.Halafu wanapewa siku 31 zingine tena,bado wamo tu,itabidi wapimwe akili kwa kweli.
Nyie watu wa ajabu kweli,mtu akifanya kosa si anachukuliwa hatua za kisheria?mmeshindwa nini kumshtaki kwa kosa kubwa kama hilo la ufisadi,wakati mnavyombo vyote vya kisheria?Tatizo kubwa la CDM ni kwamba ukiwaambia walifanya makosa kumsimamisha Lowasa Kama mgombea Wao wanakuita CCM, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa like lilikuwa ni kosa kubwa, migogoro iliyopo CUF, NCCR na CDM yenyewe chanzo chake kikuu ni Hilo kosa.
Wewe ni lini nimewakataza wasiandamane?;hata kama ,inakuwaje intruder abadilishe uamuzi wao?Huu sasa ni unaa na unafiki, we si kutwa nzima ulikuwa unakataza wasiandamane leo wasitisha umebadili gia unafiki mtupu
Nilijua tu kuwa lazima watafunga breki shimoni. Lakini pia siyo mara yao ya kwanza kufanya hivyo.
https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1105908/Hawa CHADEMA ndo basi tena.