Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Teh teh! Makujifariji
 
Ukitaka kujua angalia kama mazoezi ya majeshi yataendelea au la. Na jiulize operesheni ya Makonda na vikosi anavypita vyake ilihali ni vya Watanzania kwa nini imekuwa extended.
 
Ulitaka ajenge 'spirit' ya uoga na kujipendekeza kama huko kwenu lumumba. Poleni.
 
Mimi naammini hasira dhidi ya ccm na serikali yake inazidi kuongozeka, hii ni kwa mujibu wa vijiwe ninavyotembelea tu. Sijasikia watu wakikata tamaa na CHADEMA.
 
Ni sawa na Lucifer kujifanya anamshauri malaika wa Mungu namna ya kumpenda Mungu
 
Nisipokuwa na imani na CDM niwe na imani na chma gani sasa?

CDM IS DA ONLY HOPE LEFT
 
Kwa wanaojua sayansi ya siasa, hiki walichokifanya chadema ni mafanikio makubwa sana kwao, kwa jinsi tulivyoona hadi mwanasheria mkuu akiwa kwenye press, inamaanisha kwa sasa serikali itabidi ijiridhishe sheria zinasemaje kabla ya kufanya jambo. Siamini kwamba hawajui na ndio maana wametumia kila njia kushambulia hii operation.
 
Tukose imani kwa sababu ya kuahirisha maandamano, akili gani hizi!!?
 
Ulitaka ajenge 'spirit' ya uoga na kujipendekeza kama huko kwenu lumumba. Poleni.
Angalau atumie akili na kutambua kuwa greda au tingatinga linaweza kuvunja ukuta ndani ya muda wowote ule.
Unapowajengea watu spirit ya kuwa na kiburi, kumbuka kwamba unapambana na mamlaka ambayo inaweza kukudhuru anytime.
Kosa la huyo ambaye akipiga chafya watu kama nyinyi mnapatwa na mafua ya muda mrefu, ni kwamba hajui kwamba tactics za mapambano huenda zikibadilika, hazipaswi kubakia ni zile zile.
 
Nchi inaongozwa kwa katiba, na sio matamko. Mengine hayo hatuyahitaji.
 
Nchi inaongozwa kwa katiba, na sio matamko. Mengine hayo hatuyahitaji.
Kuongozwa na katiba sio kigezo cha watu kuendelea kuishi maisha ya kukariri.
Wakati masikini anapoishi kwa shida wakati uhalisia wa mambo ni kwamba anayemuibia haki yake ni msomi aliyesomeshwa kwa kodi ya masikini huyo huyo tena anayoilipa kwa shida, katiba inakuwa kazini kama kawaida.
Wakati mkurugenzi analifisi shirika la ndege mpaka nchi inazidiwa na kina Ethiopia, Kenya na Rwanda, katiba inakuwa kazini kama kawaida.
Punguzeni kuishi kwa kukariri kama vile mwanafunzi anavyokariri ili aweze kufaulu mitihani ya darasani.
 
Hizo hadithi za kutunga. Wakati wa kuapa hakutumia hizo hadithi, alitumia katiba. Kitaeleweka tu bado kitambo kidogo tu na nyie mtafumbuka macho. Mungu awabariki. AMEN.
 
Hizo hadithi za kutunga. Wakati wa kuapa hakutumia hizo hadithi, alitumia katiba. Kitaeleweka tu bado kitambo kidogo tu na nyie mtafumbuka macho. Mungu awabariki. AMEN.
Katiba aliyoapa kuitumia ndio hiyo ambayo imeuvunja UKUTA. huwezi kuishi kwa kutegemea kificho cha demokrasia, ukawa na uwezo wa kupambana kiuchumi na wanaokuzunguka. JK aliwapa uhuru mkubwa sana wa kuongea, matokeo yake mkaishia kumtusi na kumdhalilisha.
Mnapozimwa tangu mapema maana yake imeshagundulika kwamba hamna shukrani hata kidogo.
Na mtu asiye na shukrani siku zote huishi kwa kutegemea fadhila inayotokana na uvumilivu wa mtu.
Mmekariri maisha, ufike wakati wa kubadilika, na muwe tayari kuyapokea mabadiliko. Vinginevyo mtaishia kulalama na kulialia bila ya kuwa na nguvu zozote za maana za kubadilisha chochote kile.
 
Nadhani umeanza kuota.Nenda kaisome, hakuna popote panapozuia siasa kwa wengine isipokuwa yeye tu. Kapumzike.
 
Nadhani umeanza kuota.Nenda kaisome, hakuna popote panapozuia siasa kwa wengine isipokuwa yeye tu. Kapumzike.
Wewe ndiye uliye ndotoni. Sijakataa juu ya uhuru wa katiba. Naongelea umasikini unaotuzunguka na juuya utatuzi wake licha ya uhuru mkubwa ulio ndani ya katiba.
Uhuru wa kuwakilisha hisia zako ulio ndani ya katiba unakuwa na faida zipi ikiwa hauwezi kuongeza pato lako na langu?.
Sifa za nchi kuitwa ya kidemokrasia zina faida gani, ikiwa hakuna ubunifu wa kutafuta maisha yenye neema miongoni mwa raia wake?. Ambao bila ya hata wanatembea na nguo zenye viraka lakini wapo huru?.
 
Katiba iko wazi, hayo mnayochomeka ndio tatizo lenyewe, kwa malengo yenu maovu. Over and out
 
Katiba iko wazi, hayo mnayochomeka ndio tatizo lenyewe, kwa malengo yenu maovu. Over and out
Katiba kuruhusu siasa haimaanishi nchi iwe na anarchy. JK aliwapa uhuru mkubwa sana, bahati mbaya miaka yake kumi mkashindwa kuuthamini. This time around you will be dancing according to the song that is played by our current leadership.
Nchi sio mahali ambapo kila mtu awe na sauti kwa kisingizio cha demokrasia. Uhuru unayo mipaka yake, na kote duniani sio hapa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…